Rais Samia: Kuna mtu kakopa benki zetu 5 katoweka

Ndio imeisha hiyo, wizi mkubwa wote unaanzia serikalini.
Hicho kitu hakipo. Kuanzia mwakani pilika za uchaguzi zinaanza, hapo ndani ya chama ni kushikamana na kushirikiana, pia kuhakikisha pesa ya kutosha inaanza kuandaliwa, hakuna kugombana.
 
Kwanza nashangaa rais analalamika badala ya kuwachukulia hatua, kwanza hapo anapoongea alitakiwa kuwaagiza polisi kuwashughulikia wahusika kuanzia muda huo.

Haya mambo ya kulalamika na kubembelezana ndo yameifikisha nchi hii hapa.
 
Tanzania ni nchi rahisi sana kuipiga hela ukiwa smart kichwani yaani hutumii nguvu sana.. Huyo mfanyabiashara ametisha..
 
===
Your old lies destroy your New truth! (Somali's proverbs)
Uongo wako wa Zamani uharibu Ukweli wako Mpya (tafsiri isiyo rasimi).
 
Leo Rais Samia akipokea ripoti za Takukuru na CAG ameongelea mikopo chechefu kwenye benki za Serikali akitolea mfano wa mfanyabiashara aliyekopa mabilioni kila benki kwenye benki tano tofauti na kuondoka nchini huku dhamana alizoweka zikionekana ni feki.

Rais Samia amesema kuna ushirikiano wa wanaoenda kukopa na maafisa wa benki na wahusika wapo lakini wanatizamwa tu na wanajua walichokifanya.

Huyu mfanyabiashara ni nani?
 
Hili nalo mkaliangalieni vizuri.

Haya mambo sio ya kufumbia macho Wala kutamka kimafumbo. Kama Benki zipo waliohusika ni watumishi, sahihi zipo, pesa zikiingizwa akaunti gani na ya jina la nani kwenye Benki gani mahali gani? Na zilihamishwaje Kuna haja gani kuogopa kuwapatia wahusika?

Au ndio Shamba la bibi linazidi kupakuliwa?

MaChawa mpo?!
 
Kila mtu analalamika, nani wakuchukua hatua sasa.

Hapo amri ni moja tu, kamata wote tupa ndani, uhujumu uchumi na money laundering mahabusu 20yrs, hukumu 100yrs. Na mali zote mali ya serikali.

Ukifanya hivi x 10 tu kila mtu ataogopa mali ya umma..

JPM alikomaa na wale matycoon wa Unga wakalambwa mvua za kutosha, kuanzia wauza mirungi, bhangi na unga woote ukijaa nyavuni unakula mvua wote wakaiogopa dola...Sasa hivi imeshakuwa oya oya wauza powder wameanza tena kutamba.
 
Kinarudishwa kile cha "miaka 6"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…