Rais Samia kuondoka Februari 24, 2022 kuelekea Dubai kushiriki maonyesho ya Expo 2020

Katibu mkuu wa Wizara ya Uwekezaji aliyeko Dubai amesema Rais Samia ataondoka Tanzania kuelekea Dubai kushiriki maonesho ya Expo 2020

Wawekezaji wengi sana wameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania, amesema Katibu mkuu.

Chanzo: TBC

Daah kwani hatuna ubalozi uko?!

Mashine za Kuscan Muhimbili hazifanyi kazi watu wanakwea mapipa tu…tutaelewana tu
 
Katibu mkuu wa Wizara ya Uwekezaji aliyeko Dubai amesema Rais Samia ataondoka Tanzania kuelekea Dubai kushiriki maonesho ya Expo 2020

Wawekezaji wengi sana wameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania, amesema Katibu mkuu.

Chanzo: TBC
Huyu mama na JK kwa kusafiri ninawapongeza
 
Yaani ni awamu ile, wahuni walimpangia safari JK ya mwaka mzima, anakaa huko wiki 2 akiridi anazuga ziara ya kikazi mkoa mmoja ama 2 anatoweka tena hivyo hivyo.

Na huyu mama mtindo ndio huo huo.

Tusubiri tuone.
Tukisubiri tuone, tutakuwa tumechelewa sana. Ni wakati wa kuchukua hatua, azuiwe atake asitake.
 
Haya maonesho mama anayoenda kushiriki yana faida gani kwetu?
Mkuu wangu Nyboma ukimsikiliza vyema balozi wetu wa nchini China mh.kamarada Mbelwa Kairuki utaelewa alimaanisha nini Tanzania kuhitajika kuongeza kilimo cha zao la kahawa.....nje inatakiwa zaidi ya kiwango tunacholima na kusafirisha!

Siempre JMT
 
SSH anajua kujishusha. Mtazamo wake upo very positive, ni rahisi kusikilizwa na akaeleweka.
 
Wanasema eti anaupiga mwingi!
 
SSH anajua kujishusha. Mtazamo wake upo very positive, ni rahisi kusikilizwa na akaeleweka.
Ndio maana namkubali anawapuuza wajinga anachanja mbuga na alishasema wazi atasafiri kokote kutafuta pesa,haendi kuuza sura huko Duniani alishasafiri Sana kabla hajawa hata mbunge.

Hajawahi fanya safari ya hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…