Rais Samia kuzungumza na wakuu wa JWTZ huko Tanga

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
346
Reaction score
2,968
Ni ajabu kuwa HabariLeo wameiweka hii taarifa Instagram wakaifuta haraka baada ya kupata comments nyingi toka kwa wananchi.

Mbona sio kitu cha siri?

Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, leo anakutana na viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikao cha ndani kinachofanyika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA), mjini Tanga. Kikao hicho ni cha kwanza cha Rais Samia na uongozi wa JWTZ tangu achaguliwe kuongoza nchi kwa muhula wa pili



 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anakutana katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) kwa ajili ya kikao cha ndani na Uongozi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), tarehe 15 Desemba, 2025, jijini Tanga
 
Never seen before.

Kwaiyo Tiss wamesha piga msako wa hatari yeyote kwa Skaut wetu tena na hapo 😅😅 skauti wana pitia wakati mgumu sana huu mtungo wa Polisi na Twiss uta wauwa
 
Compromised.....Military organ shame....amehonga woote makamanda hakuna anaeweza kukemea wizi wa rasilimali za nchi .....alianza bandari .....kia ngorongoro huko anasogea marerani...sukari yeye ndio supplier na pemvejeo zote ni yeye.....plus silaha eti kiziga ujinga mtupuuui......
 
Nasikitika sana nchi kuwa na Amiri jeshi anayeongeq mpaka anajishika viuno kama yuko kwenye mazoezi ya wajawazito
 
Karibu Tanga ,sisi ni ndugu zako katika imani ,tutokea kanda moja ya zenji ...Karibu sana ,Tanga ni salama hakuna makafiri wafanya fujo huko... Karibu huku ni kwako ,tunakupenda sana.

Tuna mpango wa kukifungia chama cha vurugu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga kwa ajili ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda, tarehe 15 Desemba, 2025.
IMG-20251215-WA0042.jpg
IMG-20251215-WA0044.jpg
IMG-20251215-WA0046.jpg
IMG-20251215-WA0043.jpg
 
Neno Dkt linatumika vibaya sana. Kujikweza ni kitu kibaya sana.
 
Back
Top Bottom