Nipo Mwanza kwenye msiba. Mazungumzo makubwa ya watu ni kuuzwa kwa bandari.
Kuna jamaa, watu wanasema ni kada mwaminifu wa CCM, alikuwa akiongea kwa sauti kubwa, akawa anasema, "mimi na Mbowe mbalimbali lakini kama watasimama kupinga huu uporaji wa bandari zetu, kwa mara ya kwanza nitasimama kwa uwazi kuiunga mkono CHADEMA". CHADEMA, wasituangushe.
Alipotoka watu wakawa wanasema, 'kama na huyu amefikia kutamka haya, basi hili jambo litakuwa limewakwaza sana watu. Huyu ungemwambia nini kuhusiana na kiongozi wa CCM akusikie. Haya kweli ni mabadiliko makubwa'.
Kwa jinsi watu walivyoudhiwa na jambo hili, yeyote akiitisha maandamano kupinga, inaonekana watu hawataangalia ameitisha nani. Sijawahi kuona mshikamano mkubwa dhidi ya huu uamuzi wa kijinga uliofanywa na hawa washenzi wa bungeni.