Rais Samia: Machifu simamieni Maadili ya vijana wa Kitanzania
My Take
Serikali imekuwa na lugha nyingi sana za kujichanganya.

Juzi tuu hapo Rais alisema mahindi na Mpunga yamekuwa ni mazao ya biashara Kwa Ajili ya Nchi kupata Fedha za Kigeni tofauti na hapo awali,Sasa Leo anapinduka tena.

Kauli za kuchanganya changanya zinaua ari ya Kilimo,mkulima anavutiwa na Kilimo.kama bei ikiwa nzuri.
 
Ukinitajia wakulima 20 wanaouza mazao nje ya nchi mods wanitwange ban ya 12hrs!! Hao wanaouza nje ya nchi SIO WAKULIMA
Na huu ndio ukweli na hali halisi ambayo baadhi ya watu hawaifahamu. Wengi wanaouza hizo nafaka nje ni wafanyabiashara ambao wengi wao waliyanunua tangu yako shambani, nina mfano hai wa mkoa ninaoishi. Wanaanza kuvuna mwezi huu lakini kiuhalisia mazao si yao mpaka sasa. Wanaofaidika ni wafanyabiashara na watu wao wa kati (madalali), na si hawa wakulima wa chini na wa kati
 
Sawa. Bei tu ndo isiwe ya kijamaa huku gharama za pembejeo zikiwa juu.
 
Sawa. Bei tu ndo isiwe ya kijamaa huku gharama za pembejeo zikiwa juu.
Ni ujinga sana wa viongozi wa ccm Huwa hawajielewi wanataka nini na sijui Kwa nini hakuna coordination

Kwamba Rais anaongea anachojiskia harafu kina disrupt muelekeo wa sera ya Kilimo..
 
Na huu ndio ukweli na hali halisi ambayo baadhi ya watu hawaifahamu. Wengi wanaouza hizo nafaka nje ni wafanyabiashara ambao wengi wao waliyanunua tangu yako shambani, nina mfano hai wa mkoa ninaoishi. Wanaanza kuvuna mwezi huu lakini kiuhalisia mazao si yao mpaka sasa. Wanaofaidika ni wafanyabiashara na watu wao wa kati (madalali), na si hawa wakulima wa chini na wa kati
Haya ndo mambo vijana wa ovyo hawataki kusikia. Chakula kikipanda bei, wakulima wadogowadogo ambao ndo wengi Tanzania ndo wanateseka.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiri Tamasha la Utamaduni la Bulabo katika uwanja wa Redcross Ngomeni Kisesa mkoani Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2023.



Akizungumza kwenye Tamasha hilo linaloashiria Mwanzo wa mavuno, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewashukuru kwa mwaliko huo wa kujumuika na machifu wenzie, yeye akiwa chifu Mkuu (Chifu Hangaya).

Ameungana na wakulima hao kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake kwa kuwezesha wakulima hao kupata mavuno ya kutosha kwenye nyakati hizi mbaya za mabadiliko ya Tabianchi. Ulimwengu kwa sasa unakabiliwa na upungufu wa chakula unaoweza kusababisha mfumuko wa bei kwenye chakula na matarajio ya ulimwengu ni kuwa mfumuko huu wa bei ungekuwa 5% lakini tofauti na ilivyotarajiwa dunua inakabiliwa na mfumuko wa bei unaofikia 10% na zaidi.

View attachment 2656216
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akitembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza

Kuhusu Kilimo, Serikali imesema ilichukua baadhi ya hatua ikiwemo kuiongeza matumizi kwenye bajeti ya Wizara hii kwenye bajeti za kila mwaka ili wananchi walime zaidi, wavune zidi na wauze zaidi. Hii ni pamoja na kufanya usajili wa wakulima ili kufahamu idadi yao, kutoa ruzuku, kuongeza thamani ya mazao, ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya skimu za umwagiliaji badala ya kutegemea msimu mmoja wa mvua.

Pia, kwenye mwaka huu wa fedha, Serikali imetoa kibali cha kununua mazao ya nyongeza ili kuongeza akiba ya chakula kutoka tani laki 2 zilizopo sasa hadi laki 5 lakini pia watu wanapaswa kutunza chakula kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Kwa mujibu wa Sensa iliyopita, Vijana ndio kundi kubwa la watu waliopo kwenye nchi hii hivyo machifu hao wanapaswa kusimamania maadili ili vijana wasiharibiwe na maisha ya kisasa.

View attachment 2656223
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akimsikiliza Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Renatus Nkwande kuhusu Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

View attachment 2656224
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu na akiwa amekaa kwenye kiti cha Kifalme cha Watemi wa Kisukuma katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

View attachment 2656226
Mtoto Goziberti Bwele wa kikundi cha Ngoma za Asili ca Utandawazi Theater Group (Matwigachallo) kutoka Ukerewe akionesha umahiri wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023.

View attachment 2656228
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza mtoto Goziberti Bwele (14) wa kikundi cha Ngoma za Asili cha Utandawazi Theater Group (Matwigachallo) kutoka Ukerewe kutokana na umahiri wake wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023. Tamasha la Bulabo huleta pamoja shughuli za Utamaduni na zile za dini.
View attachment 2656229
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Machifu wakati alipohudhuria Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

Mambo ya Machifu na upuuzi mwingine weka pembeni tujadili mambo ya msingi kuhusu usalama wa Taifa letu .
 
Ni ujinga sana wa viongozi wa ccm Huwa hawajielewi wanataka nini na sijui Kwa nini hakuna coordination

Kwamba Rais anaongea anachojiskia harafu kina disrupt muelekeo wa sera ya Kilimo..
Ili ufanikiwe kwenye huu mfumo wekeza kwenye taarifa, kujua next move ya kisiasa kabla haijatokea otherwise utapoteza pesa nyingi kwenye uwekezaji.
 
Back
Top Bottom