Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Tunahitaji katiba mpya, siyo ombi bali ni hitaji la Taifa. Tume ya Warioba, kwa ushahidi, ilithibitodha kuwa Watanzania wanataka katba mpya.

Waleta chokochoko na wasiolitakia mema Taifa letu ni wale wasiotaka kutekeleza hitaji la wananchi
 
Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.

===

Rais Samia: Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge”

Rais Samia: “Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na Watoto wako na Mama Watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue Mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, Nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu

Lugha zile zile za miaka nenda rudi , hivi katiba mpya inaleta machafuko ?
 
Kwa hiyo wanaopeleka fedha bank, wajiandae siku atakapoamua kufungia account zao? Na kesi za kubambikizwa bado zipo njiani zinakuja?
"You got those that touch a little
Then there's those that rape.."

AZ- Royal Salute

Kiukweli kwa ninavyoijua thamani ya Mama,Polisi naomba mniorodheshe kwenye nguvu kazi yenu.Vijana tushachoka Usenge NEO-COLONIALISM.Wagawanye ili uwatawale ndo formula ya Wazungu Sasa Mama Samia Piga kazi vijana wengi tz tupo nyuma yako Mama yetu.Polisi nawashauri,hasa Mijini ambako waanzisha chokochoko ndiko wanakong'ang'ania kuliamshia dude.Polisi piteni Kitaani kuandaa Nguvu ya akiba Mapema msiwaache waanzisha chokochoko wasambaze ujinga na nyie msaidieni mama njoo mchukue namba zetu za simu.Tunaonyanyua Jimu tupo wengi ili tuwasaidieni kiwatuliza watukutu uchwara hawa.
Acha kuwatisha watu wazima nyau..

Kama kudai Katiba mpya ni haki ya mwanachi mwache aidai as long as havunji sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.

===

Rais Samia: Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge”

Rais Samia: “Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na Watoto wako na Mama Watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue Mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, Nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu

Uchawi ni pamoja na kupinga mchakato wa katiba mpya, haswa ile ya Jaji Warioba
 
Bavicha ndio wanaotaka kuleta vita, lala nao mbele hao hawana maana
"lala nao mbele" maana yake nini?
Huyo unayemwambia "lala nao mbele" ni nani na hao wa "kulaliwa mbele" ni akina nani!!??
Hizi lugha za kuudhi nilijua zimezikwa na mwendakuzimu,kumbe watoto wa ibilisi mnaziendeleza!!!
 
Wapinzani wanashindana kisayansi. CCM inatumia nguvu bila akili.

Marehemu pamoja na kutumia maguvu yote, lakini hakuna alipoongoza kwa amani. Kila alipotumia nguvu kuthibitisha ana uwezo aliangukia pua. Hakuna alichokikamilisha, hakuna alichofanikiwa.

Baadaye akaishia kudhibiti vyombo vya habari ili wananchi wasijue jinsi alivyoshindwa kila eneo.

Mama Samia, awe makini, achuje nini cha kusema na nini cha kuacha. Katiba ni hitaji la wananchi, ndivyo Tume ya Warioba ilivyothibitisha. Ajitenge mbali na uropokaji kama ule waarehemu.

Anayedai katiba haleti chokochoko bali anaikumbusha serikali kuteke hitaji la wananchi.
 
Lugha zile zile za miaka nenda rudi , hivi katiba mpya inaleta machafuko ?

..hawahawa wapinzani tunaoambiwa ni WAOGA ndio wavunje amani ya Tanzania?

..na ukitaka kujua kuwa anaongea lakini hamaanishi anachokiongea ni matumizi yake ya neno " vijichokochoko. "

..that means there is nothing to worry about. Hakuna hatari yoyote ile.
 
Back
Top Bottom