1. Viongozi wa taasisi nyeti wote, rais anateuwa. Matokeo yake hawatendi kwa haki au Sheria bali atakavo rais!!!!
2. Ukistaafu, ccm wamehodhi mpaka mafao uzeeni, mtu hupati haki yako mpaka ufe, eti, Akiba uzeeni utachukuwa ufikapo 60....65, kazi umekatizwa at 40yrs!!!!
3. Wabunge wanalipana mamilion, majimboni hawapo, na hawaendi
A) kupitisha makodi yasiyoeleweka bungeni
B) kututungia sheria kandamizi..... mfano zakimtandao nk
4. Katiba mbovu ilimruhusu pombe, kuzuwia mishahara na madaraja kazini ya watu wasipandishiwe kibabe miaka-5, bila kujali inflation wala katiba inasemaje
5. Watu walipotezwa, kila kona, ilikuwa sawa tu..... sababu katiba inamfanya rais wa Tz kama Mungu
6. Wakulima wanadhibitiwa na kunyimwa uhuru wa mazao yao kuyauza watakavyo. Mfano korosho huko mtwara na mahindi ruvuma
Mlolongo ni mrefu sana wa kiunyanyasaji, wachangiaje tuacha mahaba hebu tupingane kwa hoja.
Katiba mpya inaweza kupunguza baadhi ya hizi kero, bila kusahau kubambikiana kesi, watu kuwekwa vizuizini muda mrefu bila kufikishwa mahakamani, utesaji, nk