Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Tunahitaji katiba mpya, siyo ombi bali ni hitaji la Taifa. Tume ya Warioba, kwa ushahidi, ilithibitodha kuwa Watanzania wanataka katba mpya.

Waleta chokochoko na wasiolitakia mema Taifa letu ni wale wasiotaka kutekeleza hitaji la wananchi
 
Lugha zile zile za miaka nenda rudi , hivi katiba mpya inaleta machafuko ?
 
Kwa hiyo wanaopeleka fedha bank, wajiandae siku atakapoamua kufungia account zao? Na kesi za kubambikizwa bado zipo njiani zinakuja?
"You got those that touch a little
Then there's those that rape.."

AZ- Royal Salute

 
Acha kuwatisha watu wazima nyau..

Kama kudai Katiba mpya ni haki ya mwanachi mwache aidai as long as havunji sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi ni pamoja na kupinga mchakato wa katiba mpya, haswa ile ya Jaji Warioba
 
Bavicha ndio wanaotaka kuleta vita, lala nao mbele hao hawana maana
"lala nao mbele" maana yake nini?
Huyo unayemwambia "lala nao mbele" ni nani na hao wa "kulaliwa mbele" ni akina nani!!??
Hizi lugha za kuudhi nilijua zimezikwa na mwendakuzimu,kumbe watoto wa ibilisi mnaziendeleza!!!
 
Wapinzani wanashindana kisayansi. CCM inatumia nguvu bila akili.

Marehemu pamoja na kutumia maguvu yote, lakini hakuna alipoongoza kwa amani. Kila alipotumia nguvu kuthibitisha ana uwezo aliangukia pua. Hakuna alichokikamilisha, hakuna alichofanikiwa.

Baadaye akaishia kudhibiti vyombo vya habari ili wananchi wasijue jinsi alivyoshindwa kila eneo.

Mama Samia, awe makini, achuje nini cha kusema na nini cha kuacha. Katiba ni hitaji la wananchi, ndivyo Tume ya Warioba ilivyothibitisha. Ajitenge mbali na uropokaji kama ule waarehemu.

Anayedai katiba haleti chokochoko bali anaikumbusha serikali kuteke hitaji la wananchi.
 
Lugha zile zile za miaka nenda rudi , hivi katiba mpya inaleta machafuko ?

..hawahawa wapinzani tunaoambiwa ni WAOGA ndio wavunje amani ya Tanzania?

..na ukitaka kujua kuwa anaongea lakini hamaanishi anachokiongea ni matumizi yake ya neno " vijichokochoko. "

..that means there is nothing to worry about. Hakuna hatari yoyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…