Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Hili ninalielewa vyema kabisa, na siyo hoja yangu ninayoiwasilisha hapa.

Yeye akijaribu kuyatumia madaraka makubwa hayo, haina gurantee kwamba atapata matokeo sawa na yale aliyoyapata mtangulizi wake.

Awe mwangalifu sana anapoyatumia haya madaraka makubwa, kwa sababu yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ambayo hata yeye hakuyategemea kabisa.

Mara hii, katika muda mfupi huu baada ya Magufuli, kujaribu kutumia njia zile zile akitegemea matokeo yaleyale ni kama kucheza kamali.
 
Mtu kama hawajui anaweza dhani ni kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app

..and that is what i was thinking too.

..sielewi kwanini Rais SSH anadai wapinzani wanataka kuhatarisha amani.

..Tz tuna wapinzani ambao kila mtu anajua ni WAOGA, sasa kwanini Rais atoe kauli ile?

..huenda Rais SSH anatafuta sababu ya kutumia rungu la DOLA na akianza kulitumia hakuna atakayebaki salama.

..mtakumbuka jinsi Magufuli alivyokuwa akiwatesa hata wana-CCM wenzake.
 
Huwezi kula urojo n pweza ukawa na akili,macho kumchuzi ni mweupe sana kichwani nae ni mropokaji tu
 
Huoni mantiki eeeeee???

Nyinyi kazi yenu kuwaponza wenzenu tu. Yakishawakuta mnabaki kupiga kelele tu mitandaoni hata mahakamani hamtokei kudaadeki.
 
Sawa tunakusubiria front sio kwenye mitandao kama hivi,eti wengi na ww utakuwemo au wewe ni motivational speaker? πŸ˜†πŸ˜†

Barabarani mbona nipo daily boss. Mumlete na Mangula akae mbele ili aikatae vizuri hiyo katiba mpya. Au nyinyi mtakuwa kwenye keyboard mkiwatazama vyombo vya dola vikiwatetea nyie mmbaki na katiba outdated?
Sawa tunakusubiria front sio kwenye mitandao kama hivi,eti wengi na ww utakuwemo au wewe ni motivational speaker? πŸ˜†πŸ˜†
 
Hapa ndipo atakapokuja kupotezea lengo.

Njia yake ya rahisi kabisa ilikuwa ni kuendelea na danganya toto, huku siku zikienda.

Kikwete alimudu sana njia ya kuwapoza wapinzani, na hakuna lolote lililoharibika kwa upande wa CCM.

Huu "uoga" wa wapinzani mwishowe utaanza kupungua watakapoanza kuona dalili za wananchi wakiwapa moyo wa kusonga mbele.

Uoga wa wapinzani siku zote unatokana na kukosa alama za wazi za kuungwa mkono na wananchi katika hayo wanayoyapigania.

Unaweza kujikumbusha hilo jinsi Mbowe alivyoachwa solemba pale Kinondoni, ikiwa kama mfano mzuri.
 
Jidanganye Kapteni Komba alishaimba CCM ni ileile.Cha moto utakipata. Shughulika na kina Halima Mdee & Co achana na rais.Siku anaaapishwa ulifurahia ukidhani atacheka na maujinga yenu.Kazi iendeleee bwasheeee
 
Huoni mantiki eeeeee???

Nyinyi kazi yenu kuwaponza wenzenu tu. Yakishawakuta mnabaki kupiga kelele tu mitandaoni hata mahakamani hamtokei kudaadeki.
Ni vigumu sana kwangu kujibishana na wewe, kwa sababu huna tofauti na wale waliokuwa wakimpigania Magufuli humu JF. Sasa umeingia wewe na huyo mtu wako, kwa hiyo nakuachia uwanja.
 
Matusi gani kusema utanyolewa kwa wembe ule ule ni matusi?
 
Hivi ni lini CDM mtaacha ujinga? Wakati CCm wanazunguka tz nzima kuongea na wananchi nyie mmejifungia Ufipa kuongea ujinga, and mnaamini mtashinda uchaguzi 2025!
Labda washinde ndondo cup lakini siyo uchaguzi.Yaani nchi iachwe kwa kina mkudu
 
Sijaona mahala popote vurugu, kama ni maandamano ya kudai katiba mpya ndadhani maandamano yapo kisheria as long wapate kibali, kama ni mikutano ya siasa katiba imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano

Anaevunja katiba ndie anaechochea vurugu
Yaani nyie ngamia nyie.Hiiiiiiiiiii
 
Hili ninalielewa vyema kabisa, na siyo hoja yangu ninayoiwasilisha hapa.

Yeye akijaribu kuyatumia madaraka makubwa hayo, haina gurantee kwamba atapata matokeo sawa na yale aliyoyapata mtangulizi wake...
Nilikua nakukumbusha tu maana inawezekana ukawa umesahau kwamba Kwa hapa nyumbani ukiamua kwenda na Rais ujue unakwenda kukutana na mtu wa aina gani.

Hata kama hataki kuyatumia vibaya ila madaraka yenyewe yatajilindia kwa kupitia njia zote hizo nilizozitaja.

Hivyo mkubwa Leo aliposema hivyo tambua tu kasema katika capacity ipi.
 
Vitendo vinavyofanywa na vyama halali vya Upinzani haviwezi kuitwa chokochoko.
Haviwezi kuitwa vitendo vya kichoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…