Rais Samia ni Mkakamavu na Shupavu Utafikiri Ametoka Kumaliza na kufuzu Mafunzo ya Ukomandoo

Rais Samia ni Mkakamavu na Shupavu Utafikiri Ametoka Kumaliza na kufuzu Mafunzo ya Ukomandoo

Ndugu zangu Watanzania,

Nchi na Maendeleo ya Nchi yoyote ile yanaanza kwanza kujengwa kichwani na ndipo yawekwe katika karatasi na hatimaye utekelezaji. Hata nyumba inajengwa kwanza kichwani kabla ya kuwekwa tofali. Hata dereva anaye endesha gari anapaswa kupita kwanza yeye kiakili na ndipo chombo kipite. Kwa hiyo ukiona Taifa lina maendeleo na limepiga hatua za kimaendeleo ujue kuwa kuna viongozi ambao waliwaza kichwani na kuwa na picha kubwa na ndipo wakaleta maono hao katika utekelezaji.

Ukiona mtu anakufa kwa kiu akiwa katikati ya ziwa au mto basi ujue tatizo lipo ni kichwani na siyo kifo kwa sababu kama kifo kingezuiwa ikiwa angewaza kichwani juu ya kunywa maji yaliyomzunguka. Maendeleo Makubwa ya Taifa letu ni matokeo chanya ya akili za viongozi wetu. Ndio sababu Taifa linapaswa kuongozwa na watu wenye akili kubwa na walio timamu kiakili na kimwili na wenye maono ya miaka mia mbele na wenye kuishi mbele ya wakati.

Rais akiwa mdhaifu kiakili na mwenye akili ndogo na upeo mfupi wa kuona mbele ,ni ngumu sana Taifa hilo kuwa imara na lenye nguvu kiuchumi na kila nyanja. Kwa kuwa Akili na maono ya Rais ni muhimu sana katika kuchagiza na kusukuma mbele ajenda zenye maslahi na maendeleo kwa Taifa .

Tanzania tumebahatika kupata Neema ya Kuwa na Rais Samia Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ambaye ni akili kubwa na mwenye ushupavu wa akili na mwili. Kiongozi mkakamavu na madhubuti kwelikweli Utafikiri Ametoka Kumaliza na kufuzu mafunzo ya Ukomandoo.

Ndio maana tunaona akiwa na maono ya miaka mingi ijayo,Mipango yenye kuliletea Matunda Taifa letu yatakayoliwa na kunufaisha kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Hii ni kwa kuwa ni Rais Mwenye akili za juu sana. Ni muhimu sana kwa Taifa letu hususani CCM kuendelea kuteua na kupitisha viongozi wenye akili kubwa na maono makubwa kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Hata mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua za kimaendeleo kwa sababu ya kuwa na viongozi na watu wenye akili kubwa. Ukiwa na Taifa lenye kila aina ya rasilimali lakini likakosa viongozi wenye akili na upeo mkubwa matokeo yake yatakuwa ni rasilimali kugeuka laana kwa Taifa na wananchi kufa katika dimbwi la umasikini huku watoto wakifa kwa njaa na utapia mlo.

Kwa sababu Taifa likiongozwa na viongozi wajinga wasio na akili kubwa na maono ya mbali .matokeo yake itakuwa ni viongozi kushindana kuficha pesa nje ya Nchi,kuiba mali ya umma,kuhonga vyeo kwa wapiga kelele,kuteua watu wa kulinda maslahi yao binafsi,kuacha watu wenye akili kubwa na upeo nje ya mfumo kwa hofu ya kuzidiwa ushawishi au kuogopa kupokwa vyeo vyao na nafasi zao.

Ndio Maana siku zote husema kuwa Rais Samia ni zawadi kubwa sana kwetu watanzania tuliyopewa na Mungu tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana. Huyu Mama ni Akili kubwa,ni kiongozi kwa kuzaliwa aliye na Karama ya uongozi.Tumtunze sana kimaombi Rais wetu. Na tuendelee kumuunga mkono sana Mama yetu.View attachment 3240198View attachment 3240199View attachment 3240200

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Comando gani anaogopa mende?
 
Wewe kenge lini utamsifu mama yako au wewe chokora...huoni aibu Abuduli yupo kimya tuu.
Mimi sisifii bali naongea uhalisia na ukweli. Mama yangu siyo Rais wala hana serikali. Nampongeza Rais Samia kwa sababu kazi zake zimegusa hadi Maisha ya wazazi wangu ambao ni wakulima kama mimi. Kazi na mikono ya Rais Samia imegusa Mamilioni kwa mamilioni ya watanzania. Kwani ni wapi ulisikia mama yangu ametoa na kusomesha bure watoto wa watanzania bila kujali itikadi za kisiasa? Wapi ulisikia mama yangu mzazi ametoa ajira kwa vijana? Wapi ulisikia mama yangu mzazi ametoa pesa za kukamilisha mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere lenye kuzalisha megawati 2115 ? Wapi ulisikia mama yangu amewapandisha madaraja na mishahara watumishi wa umma?

Sasa kwanini nisimpongeze Rais Samia ambaye amefanya hayo yoote na kuleta tabasamu na matumaini kwa mamilioni ya watanzania
 
Back
Top Bottom