Rais Samia ni Mkakamavu na Shupavu Utafikiri Ametoka Kumaliza na kufuzu Mafunzo ya Ukomandoo

Comando gani anaogopa mende?
 
Wewe kenge lini utamsifu mama yako au wewe chokora...huoni aibu Abuduli yupo kimya tuu.
Mimi sisifii bali naongea uhalisia na ukweli. Mama yangu siyo Rais wala hana serikali. Nampongeza Rais Samia kwa sababu kazi zake zimegusa hadi Maisha ya wazazi wangu ambao ni wakulima kama mimi. Kazi na mikono ya Rais Samia imegusa Mamilioni kwa mamilioni ya watanzania. Kwani ni wapi ulisikia mama yangu ametoa na kusomesha bure watoto wa watanzania bila kujali itikadi za kisiasa? Wapi ulisikia mama yangu mzazi ametoa ajira kwa vijana? Wapi ulisikia mama yangu mzazi ametoa pesa za kukamilisha mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere lenye kuzalisha megawati 2115 ? Wapi ulisikia mama yangu amewapandisha madaraja na mishahara watumishi wa umma?

Sasa kwanini nisimpongeze Rais Samia ambaye amefanya hayo yoote na kuleta tabasamu na matumaini kwa mamilioni ya watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…