Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Hakuna kitu kipya kwenye matamshi yake, hakuna kiongozi anayeteua watu wasiofuata falsafa zake...
 
Kasema ukweli.
TLS ilikuwa kama asasi ya kiraia ya kiharakati.
Ilikuwa kama wametangaza vita na mamlaka ya nchi kwa kila jambo litakofanywa na serikali.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Mhe. Rais kazungumza vitu viwili muhimu: 1. Ameendelea kudhihirisha yuko tayari kushauriwa au hata kupokea challenge za kujenga. Hivyo hakatai kukosolewa kwa nia ya kujenga (constructive criticism).

2. Ameweka very clear; maaddui hawana nafasi. Tuwe wakweli tu, unataka kuhujumu nchi au serikali bado ujumuishwe ktk uongozi?# Rais endelea mbele.🙏🙏🙏
 
Huyu mtu hata haelewi kuongoza serikali ni kitu gani.

Anafikiri ni vita.

Hawa watu wanapewa uongozi bila ya kuandaliwa vizuri.

Hawajui political economy theory, hawajui philosophy, hawajui politics.

Wanakuja kutawala by personal animosity.

Ndiyo maana hatuelewi maendeleo ni nini.

Yani achana na lengo la kuendelea, hata lengo la kuelewa kuendelea ni nini hatujalielewa.

Sasa tunategemea hili fupa lililomshinda simba hawa fisi na mbwa wataliweza?
Huelewi maendeleo ni nini wewe na Nani!?
 
Katiba mpya inakuja sawa, hiyo ha kupunguza madaraka ya Rais ili mpate kufanya choko choko kwa uhuru zaidi, sahau🤗
Sehemu muhimu ni hapo kwenye madaraka ya rais na ndio tunapopataka sie hakuna haja ya katiba mpya kama ulimbikizwaji wa madaraka hautazingatiwa kwenye hiyo mpya.
 
Sehemu muhimu ni hapo kwenye madaraka ya rais na ndio tunapopataka sie hakuna haja ya katiba mpya kama ulimbikizwaji wa madaraka hautazingatiwa kwenye hiyo mpya.
Sawa,, shida hamna watu,, labda katiba ipitishwe Washington sio Tanzania, ukweli mchungu huo
 
Back
Top Bottom