Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Ni jambo jema

Ndio sababu tunasema Vyama vya Upinzani vya Tanzania ni lazima visupport Serikali vinginevyo vinawekwa pembeni!
No. Tatizo CCM bado hawajazielewa au kukubali siasa za vyama vingi. Ndiyo maana wengine tu naona kama ndivyo hivyo basi CCM watangaze wazi ili tujue Tanzania ni kama China, North Korea au Cuba.

Hii yawadanganya Watanzania kuwa tuna siasa za vyama vingi wakati hawataki..... Ni UHUNI.
 
Maza anaongoza nchi kama bendi ya taarabu,anataka yeye awapashe ila yeye asipashwe.
Kwani serikali ya nchi ni mali yake?
Kweli Wazanzibara yametukuta safari hii,tuchutame tu,kha!🤣🤣🤣🤣
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Hii ndiyo sababu hawaipendi katiba kwani inaweza kumzuia kumbar, ukiwa mkweli unaonekana ni mwamaharakati.
 
No. Tatizo CCM bado hawajazielewa au kukubali siasa za vyama vingi. Ndiyo maana wengine tu naona kama ndivyo hivyo basi CCM watangaze wazi ili tujue Tanzania ni kama China, North Korea au Cuba...
80% ya watanzania walikataa vyama vingi, endapo japo45 % wakikubali, maana yake hata bungeni ingekuwa 50 kwa 50
 
Back
Top Bottom