Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Mwigulu ulisomea uchumi kweli?
Mfumuko wa bei na deni la taifa kwa wakati mmoja hali inazidi kuwa mbaya sana.

Watu wanaodai madeni kama mikataba yao haikuwa na kipengele cha thamani ya pesa itakula kwao.

Wananchi wa kawaida walaji mtajua hamna viongozi sahihi ngazi za juu.
 
RAIS SAMIA: TOZO YA SHILINGI 100 KWENYE MAFUTA IRUDI, KUIONDOA HAKUTASAIDIA, KUNAINYIMA MAPATO SERIKALI......Kazi iendelee.........

RAIS SAMIA: TOZO YA SHILINGI 100 KWENYE MAFUTA IRUDI, KUIONDOA HAKUTASAIDIA, KUNAINYIMA MAPATO...jpg
 
Hehehehe na bado,,,, Lazima masikini wa hii nchi waelewe mambo yanaendaje....

U J I N G A lazima ututoke mwaka huu..
 
Leo mama Samia amesema ile tozo ya mafuta iliyotangazwa kufutwa kwenye mafuta aliaamua kuirudisha...

Ilipofutwa walisema mama kaupiga mwingi, baada ya kurudisha tozo hakuna namna tuseme mama kaupiga kiduchu Sana!
 
Yaan yeye anachofikiria ni TOZO tu alafu akizipata pesa anaenda kuzurura nje ya nchi akirudi anasema ameenda kukopa pesa
 
Hivi ni nani anaepima utendaji wa Raisi? (OPRAS)

Maana hapa tumeligwa wazi kabisa
 
Yaani ukiona Nchi inapiga kelele kwa kutaka hela za tozo tu sijui mafuta mara tozo kubwa kwenye Mpesa jua hako kanchi ni ka hovyo sana sana...watu hawana furaha kwa lundo la matozo na kila kujicha CAG anakuja na report ya wizi kwa nini msidhibiti wizi mkawapunguzia Wananchi hilo lundo la Tozo..
 
Anasema Hangaya
.
Bei ya mafuta kwa Tanzania ni ndogo ukulinganisha na nchi za Afrika Mashariki na Kati, lakini wenye sekta wapo kimya hawasemi, tunamsubiria Rais, Nani ni Rais, Rais ni taasisi.
.
Waambieni Wananchi yanayoendelea huko duniani.
.
Afrika Mashariki na kati ni Tanzania pekee ambayo bei ya mafuta bado ipo chini kulinganisha na hizo nchi nyingine.
Tupe bei za mafuta za nchi hizo bila kutia chumvi tulinganishe wenyewe
 
Wakati tozo ya sh.100 inatamkwa kwamba inaondolewa, waliitamka kwa mbwembwe kweli...kumbe tathimini zaidi haikuwa imefanyika 🤔
 
Rais yupo sawa kabisa mafuta yamepanda na yanaendelea kupanda. Isiwe maisha yenu yapo kwenye wasapu tu angalieni huko ulimwenguni kuna nini ili msiipe shida sirikali...
Putin amekubali kupokea Euro source: BBC
 
Badala ya kuzijadili ripoti wabongo tunamrushia mawe Rais, naomba kujua Hali ya Augustino Lyatonga Mrema.Mzee anafwaidi sana
 


Ebu wamsikilize na huyo shipper wa nje gharama za kusafirisha kutoka nje zimepanda ni kwa sababu ya mafuta tu au meli zina charge na downtime pia kwa mizigo ya Tanzania pekee kwa sababu ya kucheleweshwa bandarini.
 
Badala ya kuzijadili ripoti wabongo tunamrushia mawe Rais, naomba kujua Hali ya Augustino Lyatonga Mrema.Mzee anafwaidi sana
Sasa yeye si ndio kiongozi wa kila kitu, na wao ndio wametumabia hivyo kuwa raisi yupo juu ya mihimili yote. Lazima tumlaumu yeye, maana mambo yakiwa mazuri pia husifiwa yeye.utaskia mama katoa bil 200 za maji,Mara za umeme
 
Back
Top Bottom