Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Tatizo ni moja tu, rais Samia S Hassan hana uchungu na wananchi hata kidogo,anazungumza akiwa mkavuu, kama anasema " mtakoma mwaka huu".

JPM , kwenye ishu kama hizi angezungumza kwa uchungu sana mpaka machozi yanqkaribiq kutoka. Halafu angechukua hatua ambazo wananchi tunaona kweli hapa tuna kiongozi.

Mama kama atatutupia tu mizigo tupambane nayo, haumizi kichwa,anaagiza tu wenye mamlaka sekta fulani waangalie na kuchukua hatua,kitu ambacho JPM angefanya mwenyewe kuhakikisha maamuzi sahihi yanafanywa na kwa wakati.

JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, lakini hii nafasi ya kuongoza nchi ilimfaa na kum fit ipasavyo.

Hakika tulipoteza kiongozi thabiti.
Huyu wa sasa simpendi kabisa hata kumuona.

Mkuu hii nchi acha tu. Kinachozidi kunisikitisha ni hii hapa chini ivi ni kweli kipindi cha Magu umeme ulikuwa unakatika kwenye Bwawa la Nyerere na kusababishia serikali hasara hiyo. Wacha nicheke tu ila inauma sana.

Hii inadhiirisha wazi kuwa Magufuli alikuwa kiongozi Bora kuwahi kutoka Tanzania na hata Africa. Sasa wanaangalia jinsi ya kumdhoofisha na kuwapandikiza wananchi chuki dhidi ya Magufuli
72801101-4020-4353-87f7-10ff89917d0e.jpg
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe.

Rais Samia ametaka wananchi kuambiwa ukweli kwamba nauli zitapanda na usafirishaji wa bidhaa umepanda, gharama ambazo zitaingizwa kwenye bei za vitu.

Kuhusu bei ya mafuta ya kula ameomba tathmini ya tozo iliyowekwa kwenye mafuta yanayotoka nje ili kulinda viwanda vya ndani itazamwe tena kwani viwanda hivyo vya ndani havizalishi.

========

Rais Samia: Bei zimepanda kwa bidhaa nyingi tunazoagiza kutoka nje lakini kuna upandaji wa bei za mafuta, mafuta yamekuwa yakipanda nadhani kutoka mwaka jana katikati ya mwaka.

Tukachukua hatua ya kupunguza tozo ndani ya mafuta kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi lakini mafuta yameendelea kupanda.

Kipindi hiki cha pili mafuta yamepanda kwa 156 kwa lita, waziri akaona nikitoa shilingi mia yapande kwa shilingi 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge kwahiyo kulikuwa na utata kidogo, tumekaa kama Serikali tumerekebisha.

Ile shilingi iliyotoka, nimeagiza irudishwe na tathmini tuliyofanya hata kama ile shilingi tungeitoa, kwa mwenendo wa upandaji wa mafuta duniani, bado isingekuwa na impact ila tungejikosesha kile ambacho tunakifanya, kwahiyo tumeamua shilingi irudishwe.

Wabunge wenye maeneo yenu, mawaziri mnaosimamia sekta waambieni wananchi ukweli, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na mafuta yanapopanda ndio kila kitu kinapanda.

Nauli zitapanda, usafirishaji wa bidhaa zitapanda. Sasa hivi kutoa kontena China ya bidhaa kuleta Tanzania walikuwa wanalipa kontena ya ft 40 dola 1500, sasa hivi ni dola 8,000-9,000. Hii inaenda kuingia kwenye bidhaa anazozileta kwahiyo waambieni wananchi ukweli, wasikae tu kulaumu Serikali haisemi kitu.

MAFUTA YA KULA
Rais Samia:
Nakumbuka nilikuagiza waziri wa fedha kwamba katika bajeti yetu tunayoimaliza tuliingiza kitu katika mafuta ya kula nadhani na ya nyuma yake ili kulinda viwanda vya ndani nadhani kwenye uzalishaji lakini pamoja na kuongeza hiyo kitu kuzuia mafuta ya nje yasije, viwanda vya ndani ndio vimefungwa kabisa hata huo uzalishaji wenyewe, kwahiyo naomba litizameni tena.

Kama haitusaidii ondoeni ili mafuta ya nje yaingie angalau hata kama bei itakuwa kubwa lakini wananchi wana mafuta ya kutumia. Sasa mmezuia ya nje hayaingii, ndani hayazalishwi, wananchi wanapiga kelele bila shaka mafuta yatapanda bei kwa kiasi kikubwa, nendeni katazameni vipengele vitakavyoleta unafuu kwa wananchi.

=> Kwa mfano kwenye bei ya mafuta Afrika Mashariki na kati Tanzania ndio ina bei ya chini kabisa ya mafuta lakini wenye sekta hawasemi, wamekaa tu wanajifungia.

PIA, Soma=> Rais Samia aagiza tozo za mafuta kupunguzwa
Msichanganye magunzi na betri maana wapinzani wanakwamisha maendeleo. Leo nchi nzima wabunge, madiwani, viongozi wa vijijiwapo wenyewe ccm na hali ndiyo inazidi kuwa mbaya.
 
Leo mama Samia amesema ile tozo ya mafuta iliyotangazwa kufutwa kwenye mafuta aliaamua kuirudisha.

Wengi walipongeza ile tozo kufutwa vyombo vya habari vikaandika na kama kawaida wale jamaa zetu wakasifu kuwa hii Ni hatua nzuri. Looh kumbe ilipotangazwa kufutwa, raisi aliamua kuirudisha.

Cha ajabu kabisa wale walioshangilia na kusifu tozo ile kufutwa, leo watasifu ile tozo kuendelea. Lakini walikua hawajui Kama inaendelea.

Nguvu iliyotumika kutoa taarifa ya kufutwa tozo ilipaswa pia itumike tozo iliporudishwa. Lakini kukaa kimya haikua sawa kabisa.

Lakini pia mama Samia hii Bei ya dunia ya mafuta iliyopo sasa iliwahi kuwepo 2012 lakini Bei huku haikua hii, au Kuna kitu kingine kimepandisha mafuta huku zaidi ya soko la dunia?
Tozo haikufutwa,ilisimamishwa kwa muda wa miezi 3
 
Ndugu zangu,

Kama ni kweli Januari Makamba alifanya maamuzi kwa utashi wake binafsi kama waziri kukiuka maamuzi ya Bunge na kufuta tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta ya petroli na kwa sababu Rais Samia kasema "waziri hakuangalia kwa mapana yake"

Ni afya kwa Waziri Makamba akakaa pembeni la sivyo Bunge limuwajibishe.
Ndugu Mbunge msisahau hata matumizi ya serikali yaliyokua yanafanywa na serikali nje ya bajeti ikiwemo ujenzi wa uwanja wa chato.

By the way tofauti na hizo impacts za kisiasa kwa rais na waziri wake, wewe kama mbunge huoni tu hii sh.100 jinsi inavyoenda kuleta impacts itakayoumiza zaidi wa Tz huoni sababu ya kuwasemea wananchi ??
 
Kusema kwamba kuondoa shs 100/ tayari ilikuwa kwenye budget ya mwaka; kwani ya misaada kama ya TZS 1.3tr zilikuwepo kwenye budget?

Wakati fulani ni jukumu la serikali na hata Bunge kuingilia kati hizi tuzo na hasa nyakati kama hizi vita. Kusema kwamba ikitokea vita kati nchi moja na nyingine bus mzigo wa kubeba impact ya vita hivyo, budi aubebe mwananchi, nadhani serikali nayo inabidi iwajibike.

Tuangalie mfano wa bei za mafuta kwenye nchi ambazo ni land- locked countries, mfano Malawi, Uganda, Zambia, ni bei za petrolium products zipo chini. Ni dhamira tu ya serikali hizo na mabunge yao
Hili jitu halina akili linategemea kupewa maelekezo na madume!
 
Mkuu hii nchi acha tu. Kinachozidi kunisikitisha ni hii hapa chini ivi ni kweli kipindi cha Magu umeme ulikuwa unakatika kwenye Bwawa la Nyerere na kusababishia serikali hasara hiyo. Wacha nicheke tu ila inauma sana.

Hii inadhiirisha wazi kuwa Magufuli alikuwa kiongozi Bora kuwahi kutoka Tanzania na hata Africa. Sasa wanaangalia jinsi ya kumdhoofisha na kuwapandikiza wananchi chuki dhidi ya MagufuliView attachment 2169386
Aiseee.....
 
Kama Mama atamsikiliza Mwigulu kumshauri kwenye uchumi ana kwenda kuwnguka. Ajue Mwigulu hana huruma na wananchi. Pia ajue Mwigulu ana furahia anguko la Mama maana nae ana hamu ya Urais. Sidhani na wala siamini kama tsh100 wamekosa mahali pa kuipata. Hadi tuambiwe 100 inayumbisha bajeti.
Pia Mama ajue Mwugulu ni snitch haelewani na Makamba. Huvyo uchonganishi ili mwenzake aonekane amefeli hatuta shangaa..
Issue ya mafuta ya kula, hakuna kushauriana, alitakiwa atoe tamko leo. Wasaidizi wake wengi wamejiingiza kwenye biashara. Wao ndio wana fanya huu uhaba wa mafuta uwepo. Mafuta toka nje yaruhusiwe, viwanda vya ndani wana hujumu Taifa, wana fungia mafuta ili yawe kidogo mtaani bei ipande.
 
30 March 2022
Ikulu Chamwino
Dodoma, Tanzania

Rais Samia azungumzia athari ya vita ya Russia na Ukraine kwa uchumi wa Tanzania



Rais Samia ataka viongozi wenzie pia wawaambie ukweli badala ya kukaa kimya kuhusu habari hizi za kisekta, badala ya wao viongozi kusubiri kuimba wimbo "rais kasema, rais kasema ..." amesisitiza Mh. Rais Samia Suluhu Hassan .
Source : millard ayo
 
Tatizo ni moja tu, rais Samia S Hassan hana uchungu na wananchi hata kidogo,anazungumza akiwa mkavuu, kama anasema " mtakoma mwaka huu".

JPM , kwenye ishu kama hizi angezungumza kwa uchungu sana mpaka machozi yanakaribia kutoka. Halafu angechukua hatua ambazo wananchi tunaona kweli hapa tuna kiongozi.

Mama kama anatutupia tu mizigo tupambane nayo, haumizi kichwa,anaagiza tu wenye mamlaka sekta fulani waangalie na kuchukua hatua,kitu ambacho JPM angefanya mwenyewe kuhakikisha maamuzi sahihi yanafanywa na kwa wakati.

JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, lakini hii nafasi ya kuongoza nchi ilimfaa na kum fit ipasavyo.

Hakika tulipoteza kiongozi thabiti.
Huyu wa sasa simpendi kabisa hata kumuona.
Hahahahahah kibao hiki kiwafikie wapuuzi wote waliokuwa wanashabikia kifo cha Jiwe kipenzi cha wanyonge!

Ni mwaka sasa toka afariki ila nadhani kumbukumbu zake zitarejewa kwa kasi baada ya mkeka wa Ewura.
 
Kama Mama atamsikiliza Mwigulu kumshauri kwenye uchumi ana kwenda kuwnguka. Ajue Mwigulu hana huruma na wananchi. Pia ajue Mwigulu ana furahia anguko la Mama maana nae ana hamu ya Urais. Sidhani na wala siamini kama tsh100 wamekosa mahali pa kuipata. Hadi tuambiwe 100 inayumbisha bajeti.
Pia Mama ajue Mwugulu ni snitch haelewani na Makamba. Huvyo uchonganishi ili mwenzake aonekane amefeli hatuta shangaa..
Issue ya mafuta ya kula, hakuna kushauriana, alitakiwa atoe tamko leo. Wasaidizi wake wengi wamejiingiza kwenye biashara. Wao ndio wana fanya huu uhaba wa mafuta uwepo. Mafuta toka nje yaruhusiwe, viwanda vya ndani wana hujumu Taifa, wana fungia mafuta ili yawe kidogo mtaani bei ipande.
Sasa mwigulu na makamba Wala hata haihitaji kuchongeana, wote ni mizigo.
Ukimsikiliza makamba na mwigulu ni kama kulwa na ditto. Maneno mengi alafu hamna kitu
 
Back
Top Bottom