Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza hayo baada ya Simba kushinda magoli 7-0 dhidi ya Horoya katika mchezo wa Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwenye Uwanja wa Mkapa.


c92fabf8-dd90-4f2d-9a82-872ae2bacd9a.jpg

b622bf7a-db06-4b0f-a724-f27b217a4daf.jpg
 
RAIS wetu Msikivu tunakuomba THAMANI YA MAGOLI YA SIMBA IWE 10M kwakuwa wapo Champions League na YALE ya yanga wape 5M maaana wako kombe la Loosers hivyo Workload ni tofauti katika ushindi wao. Hongera kwa kupitia maoni yetu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo ameviambia vilabu vya Simba na Yanga viendelee kufunga magoli kwani pesa bado anazo na ataendelea kuwapa ili kuendelea kutoa motisha kwa timu hizo katika mashindano ya Kimataifa.

" Pesa zipo msiwe na wasiwasi, maana jana niliona utani mtandaoni eti nikimtaka Msigwa amwambie refa amalize mpira, huo ni utani tu. Wachezaji waongeze bidii ya kuweka mpira nyavuni ili waendelee kupata pesa" aliongeza Rais Samia.

My take:
Rais Samia ongeza dau kuelekea hatua ya robo fainali walau kila goli liwe milioni 15 au 20
 
Hizo pesa zingepelekwa kununua madawati na madawa.

Hao wachezaji kufunga ndio kazi yao na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

Huo ni ufujaaji wa fedha za uma.

Pesa za wadau akina Rostam Aziz, sio za serikali punguza makasiriko.
 
Back
Top Bottom