Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

Tupe bajeti ya kuhudumia watoto wore Tz kama ni hela chache hivo. Matatizo hayatakaa kuisha, wewe mwenyewe bundle lako tukiamua kukukosoa ungeenda kusaidia mtoto m1 masikini ambae hana sare ya shule (najua sio jukumu lako, ila huyo ni mTz mwenzako una jukumu la kumsaidia
 
RAIS wetu Msikivu tunakuomba THAMANI YA MAGOLI YA SIMBA IWE 10M kwakuwa wapo Champions League na YALE ya yanga wape 5M maaana wako kombe la Loosers hivyo Workload ni tofauti katika ushindi wao. Hongera kwa kupitia maoni yetu.
Hili nalo neno, ingawa wengine watasema ni ubaguzi
 
nchi ya kipumbavu sana
majasho ya walala hoi yanateketea kwa mambo ya kipumbavu kabisa
ukizaliwa Afrika wewe umelaaniwa
We sema ni Yanga mwenzangu,povu lisingekutoka kama hayo magoli angefunga Yanga
 
Tunajua michezo Ina umuhimu wake Kwa Taifa na mtu mmoja mmoja kiafya, na pia motisha ni muhimu. Na nikiwa kama mwanasimba nimefurahi Jana tumezichota haswa...

Lakini....kama pesa zipo...why zisipelekwe NHIF kwenye mfuko wa Bima ya Afya Kwa watoto isaidie watoto huko!?

Au niache kimbelembele...!?
Kiache
 
Hizo pesa huenda hata hatoi yeye bali wadau wake kwa mlango wa nyuma
Nani asiyependa umaarufu, mbona wapo ma DC na ma RC waliounga mkono kauli ya rais ya kutoa fedha kwa kujitangaza? Pia umesema "HUENDA"
 
Nani asiyependa umaarufu, mbona wapo ma DC na ma RC waliounga mkono kauli ya rais ya kutoa fedha kwa kujitangaza? Pia umesema "HUENDA"
Nina imani wamejipendekeza kwa Samia wengi tu kuwa watamsapoti kuchangia goli...hii ni fursa wakuu
 
Haya ni matumiz mabaya ya pesa za uma, hizo hela si zinatosha kabisa kuweza kujenga kisima cha maji mahali flan..alafu bado tunajiuliza why tuko masikini!
 
Huo utakuwa ubaguzi,na kisiasa haijakaa vizuri
Ukumbuke Wana Simba na Yanga ni watanzania hawa hawa
Waambieni na CAF pia wabaguzi.Simba ameingia robo fainali anapewa 1.5 billioni.
Anayeingia robo fainali Confederation Cup anapata milioni 800 kwa sababu hadhi za mashindano haya sio sawa.Hivyo kuwalipa sawa ni kuwanyima haki yao Simba kama unafuata hadhi za mashindano kama unataka uwe political correct ni jambo lingine.
 
Hizo pesa zingepelekwa kununua madawati na madawa.

Hao wachezaji kufunga ndio kazi yao na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

Huo ni ufujaaji wa fedha za uma.
Unadhani rais mjinga, wenzako wanazitumia hizo timu kuitangaza nchi kwenye medani za kimataifa return yake kiuchumi na kisiasa ni zaidi ya hiyo milioni 5,niambie ni rais gani ambae hakujihusisha na michezo kuanzia Nyerere aliyejenga viwanja vya mpira kwa mgongo wa ccm nchi nzima,mwinyi na kichwa cha mwenda wazimu,mkapa na uwanja wa kimataifa, kikwete na "mnashinda kwa maarifa sio ndio maana mkienda nje.."magufuli simba na yanga leteni kombe la afrika na sasa Samia.
 
Mimi nataka kufahamu je hizi pesa huyu raisi anazitoa wapi? Je ni mshahara wake au anafuja kodi (majasho) ya walalahoi?
Hili swali siyo mahala pake hapa,we twende tusherehekee ushindi huu,hela hizi tule tu.
Zawadi haiulizwi.
 
Back
Top Bottom