Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

Mimi nataka kufahamu je hizi pesa huyu raisi anazitoa wapi? Je ni mshahara wake au anafuja kodi (majasho) ya walalahoi?
Mama alishasema, yeye na Mwendazake ni kitu kimoja.

Uzuri wa Mama hafanyi maigizo kama Mwendazake, kaahidi ukipata goli unapata hela, usipopata goli hupati hela.

Mwendazake aligawa kwa maigizo, eti mtoto anaibuka kwenda kuibua changamoto za madarasa, eti ananunua jogoo, maigizo tena kwa kuwasimanga wapinzani mara nyingine.
 
Tunajua michezo Ina umuhimu wake Kwa Taifa na mtu mmoja mmoja kiafya, na pia motisha ni muhimu. Na nikiwa kama mwanasimba nimefurahi Jana tumezichota haswa...

Lakini....kama pesa zipo...why zisipelekwe NHIF kwenye mfuko wa Bima ya Afya Kwa watoto isaidie watoto huko!?

Au niache kimbelembele...!?
Kabisa mkuu,acha kimbelembele,
 
nchi ya kipumbavu sana
majasho ya walala hoi yanateketea kwa mambo ya kipumbavu kabisa
ukizaliwa Afrika wewe umelaaniwa
Ungeanza kwanza kuwalalamikia mafisadi ndio wanaokula nyingi,inaonekana mpira unauchukia sana
 
Akakope nje ili alipie magori ya simba na yanga, wananchi watatozwa kodi kulipia madeni
 
Mama ana uchu wa madaraka, kaanza kampeni mapema na kutoa rushwa kimtindo. Atueleze kama hizo pesa ni za mfukoni kwake au za umma?
Sizani kama kuna ubaya wowote rais akiamua kutoa motisha kwenye michezo nivile tu mentality za kimasikini zimetujaa sana kupenda kuweka hila za kisiasa katika kila Jambo.
 
MACHADEMA na sukuma gang yanaona wivu yaani yanaharisha tu Mama alivyoshika kasi.
 
Sizani kama kuna ubaya wowote rais akiamua kutoa motisha kwenye michezo nivile tu mentality za kimasikini zimetujaa sana kupenda kuweka hila za kisiasa katika kila Jambo.
Lazima kuwepo na nidhamu ya matumizi ya pesa za umma hili linpofumbiwa macho linachangia viongozi kujichotea
 
Lazima kuwepo na nidhamu ya matumizi ya pesa za umma hili linpofumbiwa macho linachangia viongozi kujichotea
Shida hutokea pale rais au kiongozi ku violate law of natural justice yaani kupendelea upande mmoja na kupuuza mwingine kila sehemu ina haki sawa nyingine japo kwa uziti tofauti, kwa mfano rais anapotoa motisha kwenye michezo ni ufujaji( misuse ) ya hela za umma.

Ifike wakati tuache mind za ujamaa zinatuharibia uelewa kwenye michezo kuna hela nyingi, kuna investors hivyo hata ajira hutengenezwa pia. Kila mmoja ana haki sawa na wenzake wanafunzi, wanamichezo, wakulima, na kada zote wana haki sawa
 
Hizo pesa zingepelekwa kununua madawati na madawa.

Hao wachezaji kufunga ndio kazi yao na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

Huo ni ufujaaji wa fedha za uma.
Hela za madawati na hosptl zipatikane kwa kuuzwa V8 na mashangingi yote ya serikali
 
😂😂😂😂😂😂, watu mna utani mbaya 😂😂🤣🤣🤣🤣
 
Enzi za magu watu walilalamika Rais anachezea hela,kwa huyu wanachekelea wakati vitu daily vinapanda bei duh aiseeee
 
Unadhani rais mjinga, wenzako wanazitumia hizo timu kuitangaza nchi kwenye medani za kimataifa return yake kiuchumi na kisiasa ni zaidi ya hiyo milioni 5,niambie ni rais gani ambae hakujihusisha na michezo kuanzia Nyerere aliyejenga viwanja vya mpira kwa mgongo wa ccm nchi nzima,mwinyi na kichwa cha mwenda wazimu,mkapa na uwanja wa kimataifa, kikwete na "mnashinda kwa maarifa sio ndio maana mkienda nje.."magufuli simba na yanga leteni kombe la afrika na sasa Samia.
Kutoa milioni 5 ndio kuitangaza nchi.

Kadanganye wenzako huko mchamba wima.
 
Acha cheap politics Mh. Rais anafanya jambo zuri kumotisha timu zetu wewe pia unaweza changisha fedha za madawati.
Wewe na yeye ndio mnafanya cheap politics.

Sasa unatoa pesa kwa mtu anayelipwa kwa kazi hiyo haalafu unakopa ili ujenge vyoo.

Hiyo ndio siasa ya bei rahisi Sasa.
 
Back
Top Bottom