Rais Samia: Nimeona utani baada ya Simba kushinda 7-0, waambieni fedha bado zipo tupieni magoli wavuni

RAIS wetu Msikivu tunakuomba THAMANI YA MAGOLI YA SIMBA IWE 10M kwakuwa wapo Champions League na YALE ya yanga wape 5M maaana wako kombe la Loosers hivyo Workload ni tofauti katika ushindi wao. Hongera kwa kupitia maoni yetu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo ameviambia vilabu vya Simba na Yanga viendelee kufunga magoli kwani pesa bado anazo na ataendelea kuwapa ili kuendelea kutoa motisha kwa timu hizo katika mashindano ya Kimataifa.

" Pesa zipo msiwe na wasiwasi, maana jana niliona utani mtandaoni eti nikimtaka Msigwa amwambie refa amalize mpira, huo ni utani tu. Wachezaji waongeze bidii ya kuweka mpira nyavuni ili waendelee kupata pesa" aliongeza Rais Samia.

My take:
Rais Samia ongeza dau kuelekea hatua ya robo fainali walau kila goli liwe milioni 15 au 20
 
Hizo pesa zingepelekwa kununua madawati na madawa.

Hao wachezaji kufunga ndio kazi yao na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

Huo ni ufujaaji wa fedha za uma.

Pesa za wadau akina Rostam Aziz, sio za serikali punguza makasiriko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…