Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

"Kwa Sasa wapinzani na upinzani umepokwa hoja zote kwa mh Rais kufanyia kazi Kero mbalimbali zinazokuwa zinawatesa wananchi, watu wanaona juhudi za mh Rais katika kuboresha maisha yao, watu wanaona Rais anavyokosa hata muda wa kupumzika ili watanzania wapate maji Safi na salama, Elimu Bora, umeme wa uhakika na Bei nafuu, huduma za Afya zilizo Bora"

Hayo maandishi hapo juu ni uongo wa hali ya juu.
Baba wa uongo ni shetani.
Wewe ni baba wa uongo.
Wewe ni ...
 
Chunga mdomo wako mkuu Tindo. Hayo machafuko yanaweza kutokea mimi na wewe tukishakuwa tumefukiwa ardhini.
 
Hizi Ni ndoto za usiku au mchana!? Yule aliyeuawa na kuteka hakupata kura zote. Huyu anapataje!?
 
Haya huwa mnaandika kumfuraisha nani? KWa nini mnapenda mdanganya uyu mama, na mnampoteza Sana ok , twende tu, ila mnampoteza Sana na sifa za ajabu ajabu
 
Ni ngumu mno tena ni vigumu sana kama ilivyoandikwa kwenye Biblia kuwa ni ngumu ngamia kupita tundu la sindano. Sababu ni kujiweka karibu na timu ya waliofeli awamu ya 4, na kibaya sana tena sana kujiweka mbali na awamu ya 5 na kibaya zaidi ni kuwa yeye hakuwa kwenye ile listi ya waliotakiwa kuja kuwa marais wa Tanzania. Asipochanga karata mapema basi inawezekana hata 2025 asifike maana hao wa awamu ya 4 wanamhujumu kila kona! Huku Mwigulu anaharibu uchumi, kule Makamba anahakikisha bei za nishati zinapanda ili kufanya maisha yawe magumu wananchi wamchukie. Yaani ni kama Kenya tu ya Uhuru na Ruto.
 

..hakuna serikali au utawala unaomaliza shida na kero zote za wananchi.

..hata ktk nchi za dunia ya kwanza ambako wamemaliza shida nyingi za msingi bado wapinzani wapo na wanachaguliwa.

..hata ndani ya Ccm wako wanachama ambao wanaona mapungufu fulani fulani ktk utendaji wa Rais Ssh.

..haiwezekani wapinzani wakakosa hoja za kushindana na Ccm na serikali yake. Hakuna utawala usio na makosa au mapungufu ambayo wapinzani wanaweza kuyatumia kuonbea kura.
 
Ndio maana nikasema hata hapo juu kuwa mapungufu madogo madogo mh Rais amekuwa akiyafanyia kazi, Jambo la kipekeee na lililowavuta wengi juu ya mh Rais Ni ule usikivu wake na moyo wake wa kuwajali Sana wananchi

Anajitahidi Sana na kufanya kazi kubwa Sana katika kero na shida za wananchi, kwake yeye Urais wake Ni kazi ya kiutumishi kwa ajili yetu watanzania, masikio yake yanamsikiliza kila mtu, macho yake yanamtazama kila mtu kuweza kumsaidia hasa mwananchi mwenye sauti ndogo

Mama Samia Suluhu Hassan Ni sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu, mama Anastahili Sana pongezi na faraja zetu watanzania, Tuendelee kumtia moyo na kumuunga mkono Rais wetu mpendwa

Anapambana kwa kadri ya uwezo wake kuwatumikia watanzania, amejitoa kwa ajili ya watanzania, Ni mama na kiongozi mwenye hekima busara na upendo, huwezi mkuta Wala kumsikia akimdhalilisha mtu au kiongozi hadhalani, Anajali na kuheshimu utu wa mtu yoyote bila kujari cheo chake

Tuna kila sababu ya kujivunia Rais huyu tulie Naye mh Mama Samia Suluhu Hassan
 
Naomba Tumwamini mama yetu mh mama Samia suluhu Hassani, kazi anayoifanya kuijenga nchi hii Ni kubwa Sana inayohitaji watanzania Tumuunge mkono na kumwombea kila wakati ili mwenyezi Mungu aendelee kumlinda wakati wote,

Anajitahidi kujenga uchumi utakao mgusa kila mtu, uchumi ambao hautamwacha mtu nyuma, uchumi utakao mnufaisha kila mtu, uchumi utakao toa nuru kwa kila mtanzania, utakao toa matumaini kwa kila mtu afanyaye kazi na kutumia fursa zilizopo hapa nchini

Ndio maana unaona mh Rais akitoa Hadi Ruzuku inapobidi ili kumsaidia mtanzania kuyamudu maisha, Nawaombeni watanzania wenzangu Tumuunge mkono Rais wetu, Tusichoke kumuombea, na tumshauri tunapoona panafaa maana mama Ni msikivu sanaa
 
Haya huwa mnaandika kumfuraisha nani? KWa nini mnapenda mdanganya uyu mama, na mnampoteza Sana ok , twende tu, ila mnampoteza Sana na sifa za ajabu ajabu
Ninaongee kitu Cha kweli, hivi hapa nipo na watu hapa wanamsifia mama balaa, hii Ni baada ya kuona shule moja huku kwetu iliyojengwa na mama Samia suluhu Hassani mh Rais wetu ikipendeza Sanaa
 
Ni sawa akipata kura za kutosha tena hata zote kama wananchi wanamkubali.Jambo la msingi kura zake ziwe zilizopatikana kwa misingi ya uwazi,uhuru na haki.
 
Nilitaka nishangae,usimtaje Magufuli!!!
 
Huko uliko Hakuna shule zilizojengwa na kuboreshwa? Huko uliko Hakuna zahanati na vituo vya Afya vinavyojengwa? Huko uliko Hakuna miradi inayogharamiwq na serikali ya mh Rais wetu? Huko uliko hamlimi? Kama mnalima hujasikia Ruzuku inayotolew kwenye mbolea Kias Cha billioni Mia moja hamsini itakayo saidia kushuka kwa mbolea Hadi elfu 79 kutoka huko kwa laki na 30 Hadi laki na 40

Au haupo Tanzania au unachuki zako tu au unataka uunganishiwe bomba la maziwa na asali Hadi hapo pako ndio utakuwa kazi inayofanywa na serikali hii
 
Ni sawa akipata kura za kutosha tena hata zote kama wananchi wanamkubali.Jambo la msingi kura zake ziwe zilizopatikana kwa misingi ya uwazi,uhuru na haki.
Ndio zitakavyo patikana maana kazi yake kubwa Ndio itakayo fanya watanzania kwa umoja wetu kwenda kumpigia kura kwa wingi, kwa sababu bado tunamhitaji mh mama Samia suluhu Hassani aendelee kututumikia sisi watanzania

Tumeridhishwa na utendaji kazi wake wa kutukuka, Ni mama Hadi 2030 ndio tutaanza kuulizana tufanye Nini
 
Siungi Mkono chama chochote naomba jeshi lishke nchi.
Mh mama Samia suluhu Hassani ndio Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama wa nchi yetu, tuna Imani na mh Rais, na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina Imani na Rais wetu Ndio maana vinaendelea kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama muda wote, ili kutoa nafas kwa mh Rais kuijenga nchi na kuwaletea maendeleo wananchi bila shida
 
Unamalizana na mimi harafu unanijibu 😬😬..

Niko humo jukwaani kabla yako na Kazi yangu ni kuweka sawa mada ngumu.
 
Ninaongee kitu Cha kweli, hivi hapa nipo na watu hapa wanamsifia mama balaa, hii Ni baada ya kuona shule moja huku kwetu iliyojengwa na mama Samia suluhu Hassani mh Rais wetu ikipendeza Sanaa
Nchi ngum Sana hii,nimejikuta nikicheka kijinga Sana, Sasa SSH ndo anajenga au Serikali ndo inajenga? yeye ni msimamizi katika ngazi ya juu ya serikali KWa niaba ya wenye nchi, Sasa mkisema anajenga hizo pesa anatoa mfukoni mwake?,
Alafu ni serikali ipi ambayo haikujenga shule,hospitali, reli, mabwawa ya umeme, stendi,n.k, nchi haijawahi simama ,vilevile hata yeye akiondoka 2025, serikali ijayo bado itaendelea kujenga tu,
Sasa sijui huwa mnasifia KWa kujua au kutojua ,acheni Mambo haya, kwani serikali yake kurudisha maendeleo KWa wananchi ambao ndo walipa kodi ni hisani au niwajibu ? Kama ndivyo sifa za ajabu za nini, badilikeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…