RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

Marehemu Kighoma Ali Malima hajawahi kuwa waziri wa fedha katika serikali ya Mwalimu Julius Nyerere.
 
A set up ?! Nobody knows !
 
Ila hapo kuhusu kusema eti Waarabu siyo wajomba zetu, karusha jiwe gizani. Kuna ka ukweli fulani ambako kanaweza kumgharimu cheo chake.
 
Hizi Fikra kama za Malima ndizo zinazotakiwa. Kama kuna chochote cha kurekebishwa kwa manufaa ya taifa, kifanyike.
Sidhani kama kuna kiongozi wa serikali mwenye akili nzuri atasema kama kuna makosa yaachwe.
Kufanya makosa na kusahihisha ni jambo la kawaida.
 
Kabisa !
 
Hivi alichokosema Malima kina tofauti gani na kinachosemwa na Watanganyika?
Umelishwa nini wewe babu?
 
Aaah, mie wajomba zangu na mashemeji zangu hao. Lakini kwenye biashara hakuna mjomba wala shangazi, ndiivyo nilivyomuelewa Malima.
FaizaFoxy ndugu yangu hakuna apingaye wawekezaji popote pale watakapotoka hewala. Hadhari ni muhimu ili tusiingie mikataba tu ya hovyo kama ambavyo imekua historia. Tuna hati chafu juu ya mikataba tuliyopata kuingia hapo kabla. Mie sina chuki hata mwekezaji atoke Bahrain, Lebanon, Qatar au Israel. Tunachotaka serikali iache udalali kwenye mikataba.
 

Hakuna mkataba wa kuendesha bandari kwa yeyote mpaka sasa. Au upo?
 
Nyie kweli ni kima!! Sasa sisi tulikua tunapinga nini na nyinyi mnaongea nini sasa hivi? Loud and clear huu mkataba wa DP World ni mpumbavu peke ake anaweza kuukubali.
 
Kumbe huko CCM bado kuna watu wenye akili zao. Big up Malima.
 
Kama mkaataba sio mbovu kwa nini anasema tuwe makini tusipigwe? Mkataba ungekua mzuri wala asingeweka tahadhali

Ameongea indirect kuwa mkataba haufai, umeshindwa hata kumuelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…