RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

Kada wa CCM mbunge Mariam Ditopile Mzuzuri azungumzia maoni kuhusu mkataba wa bandari

Kwamba wewe mumeo ni mwarabu?
Wewe vipi wewe, upo Tanzania ua Zambia?

Dsr, Pwani, Tanga, Morogoro, Singida, Shinyanga, Mwanza , Tabora, Simiyu, sijuwi Kagera huko, hakuna ambae hana shemeji, mjomba au shangazi wa Kiarabu, japo wa mbali.

Hivi wewe unataka kunambia japo kwa mbali huna shemeji wa Kiarabu?
 
Wewe Ajuza Endelea kula ugoro tu!!...
 
Eti waarabu wajomba zake..si akaishi nao sasa..tuacheni rasilimali zetu hatavizazi vyetu vitatakuja kusahihisha pale mlipo shindwa
Wacha kudandia hoja, kwanza soma vizuri andiko na msikilize, hakusema Waarabu wajomba zake, ila kasema sio wajomba zetu
 
Nimemsikia ila hakuna popote aliposema mkataba wa DPW ni mkataba mbovu!.

Alichosema ni tuwe makini ili tusipigwe, kwasababu huko nyuma, tulipigwa!.

Msimchonganishe Malima na Samia!. Serikali yetu inafanya kazi kwa mtindo wa a collective responsibility, serikali ikiisha sema ndio, Bunge likasema ndio, chama tawala, chama cha Mapinduzi, CCM, kikasema ndio, hawezi tena kuibuka mserikali yeyote akasema sio, huko kutakuwa ni kwenda kinyume cha kanuni ya collective responsibility.

Kwenye kanuni hiyo ya a collective responsibility, ukiamua kutofautiana na uwajibikaji wa pamoja ni unajinyamazia kimya!. Ukijiona huwezi kunyamaza, kwanza ana resigns ndipo unapinga!.

Hivyo mleta mada umepotosha!, usimlishe maneno Adam Malima.

Ps
Kaka yangu Paschal nakuheshimu saana na upo sahihi maana mtu anaweza itwa huko sijui kwenye Part Caucus lakini collective responsibility yenye nia njema ni jambo jema lakini collective responsibility ya kuuza nchi ni muda muafaka wa watu kutumia akili na uzalendo binafsi na siyo kumsikiliza mwenyekiti na ukumbuke kuwa hapa Tz kwa katiba yetu hakuna collective responsility ila kuna MWENYEKITI RESPONSIBILITY na ukionekana unampinga mwenyekiti kuna uwezekano wa kupelekwa jando bila ganzi
 
Akizungumza katika kipindi cha Good morning Wasafi FM, Malima ambae marehemu baba yake aliwahi pia kuwa waziri wa fedha kipindi cha Nyerere, amesema Kinachopingwa sio ufanisi wa bandari bali ni vipengele vya mkataba, na huko nyuma, 1998 Tanzania iliwahi Ingia mikataba mibovu ya madini, na alipokuwa waziri wa nishati miaka kumi baadae wakaikataa .

Akafafanua zaidi amesema kwamba Waarabu sio wajomba zetu na hivyo muhimu ni kuangalia vifungu vyenye shida virekebishwe kwa maslahi ya taifa na si vinginevyo.

Msikilize mwenyewe 👇

View attachment 2684047
Asante ustaadh Malima umemfunga mdomo bibi FaizaFoxy anayedai kuwa Kuna UDINI
 
Wewe vipi wewe, upo Tanzania ua Zambia?

Dsr, Pwani, Tanga, Morogoro, Singida, Shinyanga, Mwanza , Tabora, Simiyu, sijuwi Kagera huko, hakuna ambae hana shemeji, mjomba au shangazi wa Kiarabu, japo wa mbali.

Hivi wewe unataka kunambia japo kwa mbali huna shemeji wa Kiarabu?
Sina
 
Asante ustaadh Malima umemfunga mdomo bibi FaizaFoxy anayedai kuwa Kuna UDINI
Sasa anifunge mdomo kwa lipi? Malima kapinga nini hapo? Alichoongea ni msimamo wa serikali kwa 100%

Hivi hamuelewi mnachokisikiliza au mmezowea kufanya spinning?

Adam Malima yupo sahihi 100%.
 
Sasa hapo kaongea lipi jipya mbona huo ndio ushauri uliotolewa na bunge baada ya kuridhia makubaliano?
 
Yupo sahihi, wapo wengi wataamua kujitoa muhanga na kufunguka.
Hili swala la bandari ni mwanzo wa mambo mengi yajayo. Huu ni wakati wa watu kusimama ili wahesabiwe, huko tuendapo tusije kulaumiana tu.
Sasa hapo kaongea lipi jipya mbona huo ndio ushauri uliotolewa na bunge baada ya kuridhia makubaliano?
 
Back
Top Bottom