Regional Per Capita GDP: Hii ndio Mikoa 7 ambayo Wananchi wake wana kipato cha Uchumi wa kati Tanzania Bara

Regional Per Capita GDP: Hii ndio Mikoa 7 ambayo Wananchi wake wana kipato cha Uchumi wa kati Tanzania Bara

Production iko kubwa sana ukichukua mifugo yote ya mkoa wa mwanza ngombe,mbuzi ,kuku ,samaki wote nk ukigawa kwa population ya mwanza per capita utakayopata ni kubwa sana
Acha porojo tuwekee hapa takwimu za mchango wa sekta ya mifugo kwenye pato la Mwanza tuone vinginevyo unajifariji tuu hapa lakini hii sio mara ya kwanza Mikoa hiyo ya kanda ya ziwa kuwa ya mwisho .

Hata kwenye makusanyo ya halmashauri ukitoa mwanza jiji kwingine kote ni hamna kitu sasa wewe haiwezekani kila parameter inawapitia kushoto
 
... Kagera kwa climate yake haikutakiwa kuwa kwenye list ya umasikini! Achana na kahawa, ndizi za kila aina, n.k. hadi vanilla inalimwa kule wanakuwaje maskini?
Mtu akilima ka nusu eka ka vanila eti tayari ni mkulima hodari,aisee mtaogelea sana kwenye umaskini

Hata msihangaike tembeeni Mikoa tajwa afu uje kuringanisha na kwenu utapata majibu
 
uko sahihi .Iringa na njombe hamna kitu kule sijui wameziwekaje
... zaidi ya 70% ya mbao zinazotumika nchi hii zinatoka Njombe na Iringa tena wakulima wadogo. Parachichi pendwa Ulaya na Marekani ndio kwanza ina-take off; 5 to 10 years to come watakuwa level nyingine; TRA wahamie kabisa huko wakawatie umasikini. Je, chai? Kahawa? Wattle? Sijazungumzia mazao ya nafaka!
 
Mkuu @Oppurtunity Cost ngoja @instanbull aje akunange 😂😂
Unannangaje mjumbe? Akawanange NBS mimi nafikisha taarifa tuu.Toka nimeanza kutoa takwimu hapa hakuna hata siku moja Mikoa ya nyanda za juu imekosekana sasa unajiuliza inapendelewa au ndio uhalisia? Watu wanazaana hovyo hovyo wanarundikana kwenye vijumba vyao vya mabati ya masufuria saa ngapi watafanya kazi?
 
Unannangaje mjumbe? Akawanange NBS mimi nafikisha taarifa tuu.Toka nimeanza kutoa takwimu hapa hakuna hata siku moja Mikoa ya nyanda za juu imekosekana sasa unajiuliza inapendelewa au ndio uhalisia? Watu wanazaana hovyo hovyo wanarundikana kwenye vijumba vyao vya mabati ya masufuria saa ngapi watafanya kazi?
Hahahaha anakwambia Njombe na Iringa zinapendelewa. Pesa ipo Misungwii 😂😂
 
... sijawahi kuishi Moshi Mkuu; hebu dadavua kidogo.

Moshi ndizi mkungu mzima ni wakulima wanauza 1500Tsh, ukienda arusha mji unaofuata ndizi kichane kimoja ni 4000Tsh, ndizi nzima infika mpaka 40,000Tsh, sjawahi kusafirisha mzigo kutoka moshi mpaka arusha ila nauli ya mtu mwenyewe kutoka moshi mpaka arusha ni 1500 tu kwa lisaa moja! mengine ni maswali ambayo hata mm sielewi wakulima wa moshi wanafeli wapi

1620203009673.png


ukija dar sahani moja ya ndizi ni 2000 tsh kwa mama ntilie, na treni kutoka moshi mpaka dar ipo na kwenda arusha ipo! na mbunge mbowe alikuepo na alipinga treni
 
... zaidi ya 70% ya mbao zinazotumika nchi hii zinatoka Njombe na Iringa. Parachichi pendwa Ulaya na Marekani ndio kwanza ina-take off; 5 to 10 years to come watakuwa level nyingine; TRA wahamie kabisa huko wakawatie umasikini. Je, chai? Kahawa? Wattle? Sijazungumzia mazao ya nafaka!
Achana na hilo jinga lipiga pambio la hayati Jiwe limekaa tuu sehemu moja lindhani Tzn ni lumumba pale.Kwa kukuongezea tuu mazo ya nyanya,mbogamboga,matunda anuai,viazi,pareto na nafaka za kila aina nk yanazalishwa kwa wingi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Saa ngapi tutakuwa maskini? bado utalii,madini,mifugo na biashara za kuvuka border havijawa fully utilised,siku vikichanganya hakutakamatika huku.Huko usukumani madini yanazidi kuisha na ardhi ni jangwa kutabakia magofu miaka 20 ijayo.
 
Uwe uchumi wa kati ushindwe kupandisha mishahara na madaraja ya watumishi kwa miaka 6??
Uwe uchumi wa kati ushindwe kuajiri kwa miaka 6??
Uwe uchumi wa kati ushindwe kumaliza miradi ya kimaendeleo kwa wakati??
Uwe uchumi wa kati utumie mabavu na mitutu ya bunduki kukusanya Kodi kwa wananchi??

Ni taahira pekee ndo ataamini kuwa Tanzagiza ipo uchumi wa kati.

hivi ndo viashiria vya uchumi wa kati? ivi uko timamu?
 
Moshi ndizi mkungu mzima ni wakulima wanauza 1500Tsh, ukienda arusha mji unaofuata ndizi kichane kimoja ni 4000Tsh, ndizi nzima infika mpaka 40,000Tsh, sjawahi kusafirisha mzigo kutoka moshi mpaka arusha ila nauli ya mtu mwenyewe kutoka moshi mpaka arusha ni 1500 tu kwa lisaa moja! mengine ni maswali ambayo hata mm sielewi wakulima wa moshi wanafeli wapi

View attachment 1774034
Huo mkungu wa 1500 uliuziwa lini? Tafadhali punguza kamba..

Pia nauli 1500 ya lini hiyo? Acha uongo ndugu..
 
Hata Kagera? Mkoa uliobarikiwa kila aina ya mazao; evergreen everywhere unakosaje kuwa kwenye list ya 10 bora?
Wenye mkoa wamewekeza kwenye elimu na hawaishi mkoani hapo. Wapo mikoa mingine kama Dar ( mlimani, wizara ya M ya nje, Kairuki, Muhimbili n.k) , Arusha (wakikuza utalii, na kukuza bodi ya kahawa n.k)

Kifupi mchango wao kwenye hiyo mikoa 10 bora ni mkubwa sana.

Mikoa kama nyanda za kusini wananchi wamejikita sana kwenye rasilimali za mikoa yao kama kilimo n.k na hivyo mikoa hiyo kustawi. Hongera nyanda za juu.
 
Habari zenu wadau!

Mwaka 2020 tulitangaziwa Tanzania kusajiliwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake wamefikia kiwango cha Uchumi wa Kati wa chini yaani Lower Middle Income Country.

Hesabu hiyo huwa inazingatia GNI per Capita Income ambayo ina range Kati ya $1'036-$4,045 ,,ambapo kwa Tanzania hapa ni mikoa michache Sana ambayo wananchi wake ndio wako Uchumi wa Kati,yaani wenye kipato kuanzia milioni 3 kwenda juu.

Ifuatayo ni orodha ya mikoa 7 ambayo wananchi wake Wana mapato yaliyofikia hicho kigezo cha Uchumi wa Kati, pato la kila mwananchi kwenye mkoa husika limeanishwa.

Regional Per Capita GDP at Current Market Prices,Tanzania Mainland, financial year 2019.Figures in Million TZS

1. Dar es Salaam (4,529,876)

2. Iringa (3,868,283)

3. Mbeya (3,675,999)

4. Kilimanjaro (3,302,915)

5. Ruvuma (3,288,252)

6. Arusha (3,198,260)

7. Njombe (3,073,361)

Sambamba na hiyo kuna Mikoa 5 iliyopo mkiani ambayo hali ya vipato kwa wananchi wake ni mbaya sana,mikoa hiyo ni;

1. Shinyanga (1,857,610)

2. Tabora (1,740,554)

3. Dodoma (1,677,901)

4. Singida (1,578,040)

5. Kagera (1,143,992)

MY TAKE;

Hongera Sana wachapa Kazi wa Nyanda za Juu Kusini.

ANGALIZO,

Kwa kweli hali za sisi wananchi ni mbaya, Serikali ijitahidi kuwekeza kwenye uchumi wa watu la sivyo tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya maana na kasi ya kuzaliana ni kubwa mno. Ikumbukwe Tanzania ni kati ya nchi 5 zenye idadi kubwa ya watu na pia zenye idadi kubwa ya maskini barani Afrika.

SOURCE-TANZANIA IN FIGURES 2019.(pg 50-53)

CREDITS-National Bureau of statistics,Ministry of Finance and planning, 2020.
View attachment 1773908
Sisi mtwara na Gesi yetu asilia top 7 hatumo?? Na Tanga je??
 
Birth rate ikiwa kubwa soko nalo linakuwa kubwa vile vile GDP inapanda
Population isiyo na kipato ni hopeless kama ilivyo sehemu kubwa ya wasukuma.

Robo ya population ya dunia ipo China na robo nyingine ipo India lakini China inakuwa regarded kama 'potential world market' sababu ya hali nzuri kiuchumi, India hakuna mtu ana time nao sababu ni masikini kwa sehemu kubwa.
 
Wenye mkoa wamewekeza kwenye elimu na hawaishi mkoani hapo. Wapo mikoa mingine kama Dar ( mlimani, wizara ya M ya nje, Kairuki, Muhimbili n.k) , Arusha (wakikuza utalii, na kukuza bodi ya kahawa n.k)

Kifupi mchango wao kwenye hiyo mikoa 10 bora ni mkubwa sana.

Mikoa kama nyanda za kusini wananchi wamejikita sana kwenye rasilimali za mikoa yao kama kilimo n.k na hivyo mikoa hiyo kustawi. Hongera nyanda za juu.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] napokea pongezi kwa niaba yao
 
Mwanza ndio mkoa pekee Tanzania ambao utajiri uko kuanzia mijini hadi vijijini

Mijini kuna biashara nyingi sana ukienda vijijini kuna samaki na pamba na mifugo mingi na migodi kibao ya dhahabu
Tofautisha kuwa na rasilimali na kuwa na utajiri. Rasilimali zinaweza kukuletea utajiri if and only if zinatumika katika namna inayoleta tija kiuchumi.

Mfano mzuri ni Tanzania yetu ambayo ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa utajiri wa rasilimali lakini kwa kuwa 'maboga' yanatawala, nchi imebaki kuwa ombaomba huku wananchi wake wakiishi under extreme poverty for years.
 
Back
Top Bottom