Ruble ya Urusi inazidi kuchanja mbuga kwa kuongezeka thamani

Ruble ya Urusi inazidi kuchanja mbuga kwa kuongezeka thamani

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Leo ijumaa pesa ya Urusi Ruble imezidi kupaa kwa thamani ikilinganishwa na fedha zingine kama dola na Euro. Kwa sasa dola moja ni ruble 57.67.

Ikumbukwe kuwa kabla ya vita dola moja ilikuwa sawa na ruble 82, na mwanzoni mwa vita baada ya Urusi kuwekewa vikwazo lukuki vya kiuchumi, fedha yake iliporomoka hadi kufikia dola moja sawa na ruble 150.

Lakini baada ya Urusi kuanza kuuza gesi yake kwa ruble pesa yake ilianza kupanda kwa kasi na leo hii imefikia dola 1 = ruble 57.67.

Ruble smashes four-year high against US dollar​

The Russian currency strengthens ahead of upcoming tax payment.

The Russian ruble reached its strongest position against the US dollar in over four years and reached a seven-year high against the euro on Friday. The ruble is being propelled by recently introduced capital controls, Russia’s new ruble-based gas payment scheme and looming tax payments for corporations pushing up demand for the currency domestically.

The exchange rate reached 57.67 rubles per dollar at 08:13 GMT, its firmest against the US currency since March 2018, according to data from the Moscow Exchange. The ruble also gained nearly 5% on the euro, with the exchange rate now below 60 rubles per euro, hitting a seven-year high.
 
Mwanzo alaikua anawakopesha sawa hawa ulaya, anawapiga tafu sana, yaani anawabeba kwa nishati, baada ya chokochoko kumuekea vikwazo kaanza kuwalipisha inavyotakiwa haswa, yaani hamna mkopo wala nn, lipa hela nakupa gas/oil kwa hela ninayotaka mm
 
how long will this sustain in the market,
Hilo ni kama teke la kuku!! There is no turning back!! Thamani ya pesa hubebwa na thamani ya bidhaa ambazo nchi huuza kwenye soko la dunia!

Thamani ya ruble inabebwa na thamani ya gesi na mafuta na uhitaji wa bidhaa hizi kwenye soko la dunia. Na kwa sasa ili uzipate kwa nchi za magharibi ni lazima uitafute ruble!! Watasubiri sana kudhani ruble itashuka thamani!

Ukisusia mafuta na gesi ya urusi kuinunua moja kwa moja toka urusi lazima utainunua kupitia nchi ya tatu kwa bei ya juu zaidi!!
 
Kila siku mnasema hivyo lakini Kila siku inasonga mbele. Ujue kuimarika kwa fedha yake kunatoa nafuu kwa wateja wa vitu mbalimbali wa ndani na pia inaongeza uwezo wa kununua wa fedha yake.
Hata hao EU wenyewe watakuwa wanaitafuta hiyo Ruble kwa udi na uvumba ili waweze kununua bidhaa kama gas, mafuta na nafaka. The effect ni kuongezeka kwa purchasing power ya Ruble.
 
Hii inawatia hasira Sana US na NATO
Wanakasirika MNO halafu kwa hasira hiyo wanaweka vikwazo bila kufikiri kwa undani na mwisho wa siku vikwazo vinawaumiza wao zaidi!

Kinachowauma zaidi ni Muungano wao wa nchi 30+ dhidi ya nchi 1 halafu inawatoa jasho!! Kwa mfano wakati Marekani inaiwekea vikwazo urusi, iliwapiga marufuku warusi kutumia dola kwenye miamala yoyote ISIPOKUWA kama wanalipa madeni!! Walidhani kuwa Urusi itashindwa kulipa madeni baada ya pesa zake kwenye benki za nje kuzuiwa!

Baadaye wakashangaa urusi inalipa madeni yake bila shida yoyote!! Sasa wameamua watamzuia kutumia dola hata kwa kulipia madeni hata kwa wadai wa Marekani yenyewe!! Sasa Urusi ikacheka na kusema kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi, hiki kikwazo ni nafuu kwetu na hasara kwa Marekani yenyewe!!
 
Back
Top Bottom