Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

True
 
Yaani wanatia hadi huruma,mimi nitakapokuja kuwa na mtoto,siwezi kukubali haya ya saa kumi na moja na nusu shule
 
Elimu ikishageuzwa biashara hayo ni kawaida kutokea

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Noma sana...na kwenye hizo school bus watoto wanajaza kama maharage kwenye gunia...ukiwa unampokea mtoto mlango ukifunguliwa usipokuwa makini mtoto anaweza dondoka chini
 
Wakati mnalaumu kumbukeni pia kuna sababu ambazo zinamlazimu mtoto kukaa mbali na wazazi bila kupenda. Kwa Mimi shida ni MTU wa kumwachia mtoto ilibidi nikapeleke day care na 1.5 yrs hakuna msichana anaweza kukaa mtaani kwetu yaani inabidi MTU uwaze Mara 2 ukiwaza kuzaa either uache kazi ulee sasa hiyo kazi ndio tegemeo LA kumtuza huyo mtoto. Hata ukimpeleka shule ya kuwahi kurudi huko nyumbani atakaa na nani na wewe unachelewa kufika. Yaani kuna watu wako na kazi ya kuharibu mabinti wa kazi ili waone unavyoteseka na watoto wako suluhisho waende wakashinde shuleni tukutane usiku hamna namna. Wengine imebidi wapeleke boarding sio kwa kupenda ni shida
 

🇹🇿 Nyie acheni yenu yaanze shule yakiwa mavijeba sisi tunawapeleka

🇹🇿 Nyie endeleeni kuyadekeza ya kwenu fainali kwenye soko la ajira

🇹🇿 Nyie endeleeni kuwaachia ma house girls waendelee kucheza nao sisi wa kwetu bora wakacheze shuleni

🇹🇿 Nyie wa kwenu waacheni waendelee kuangalia ma katuni sebuleni sisi wa kwetu acha wakajifunze alphabet shuleni
 
Wakikusikia utasikia "kama vipi muhamishe"

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Hili suala si la kulijadili kilevilevi..

Ukiwa emotional utakuta unaroporopo tu.
 
Ni afadhari huko daslam kuna joto kuamka sio kwa mbinde sana.

Huku kwwtu baridi ni kali na kuna muda unakuta kuna kimvua halafu katoto saa 11 kanaamshwa. Aisee mi mwanangu ataenda shule saa 1 mpaka afike miaka kadhaa sio hiyo mi3 au 4 katoto kanaamshwa saa 12 ni MATESO.
 
Nyie mnashangaa wa saa 11 wakati kuna sehemu nilikua naenda kazini alfajiri kubwa mno nilipita sehemu na kiusafiri changu nikakutana na mtoto amekaa barabarani hana hata wa kumsimamia ilikua majira ya saa 10 alfajiri yupo njiani peke ake... Huwezi amini niliingiwa na hasira kama mimi ndo mwenye mtoto nilimbeba huku nikitafakari je sitafuti kuja kupewa kesi ya ubakaji wa mtoto huyu? Nilitamani siku moja nimuone tena ili anipeleke nyumbani kwao ila sikuwahi kukutana nae njia hiyo hadi leo.
 
Huu upuuzi niliukuta wakati dogo aanza Grade 1. Saa 11.30 gari inampitia halafu shule ipo km 10 tu kutoka home. Nikaongea na wazazi kadhaa wakaniambia hawana jinsi ndio utaratibu. Mbishi nikaingia front,nikatafuta wazazi 20 tukatishia kuhamisha watoto. Leo hii gari inapita saa 1 asbuhi shule ileile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…