Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Wenzetu Ulaya wana shule bora kuanzia level ya Kata.

Huku kwetu badala wazazi mji commit muboreshe mazingira ya shule zilizo jirani na makazi mnakimbilia kujaza ma bus ya watoto kuwasafirisha makilometa ya umbali bila sababu ya msingi.

Mtoto anakaa Chanika anasoma Olympio! Wa mbagala nae unalazimisha asome Olympio. Unategemea ataamshwa saa ngapi kupanda school bus?
True
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Yaani wanatia hadi huruma,mimi nitakapokuja kuwa na mtoto,siwezi kukubali haya ya saa kumi na moja na nusu shule
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Elimu ikishageuzwa biashara hayo ni kawaida kutokea

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Noma sana...na kwenye hizo school bus watoto wanajaza kama maharage kwenye gunia...ukiwa unampokea mtoto mlango ukifunguliwa usipokuwa makini mtoto anaweza dondoka chini
 
Mkuu pole sana kwa taarifa yako hao watoto sio miaka 4 kama unavyosema hao ni watoto wa miaka miwili na nusu hadi mitatu na minne na walipaswa kupelekwa kwenye day care lakini wanapelekwa mashuleni wakafundishwe.

Wazazi wa siku hizi hawana akili hawajali tena usalama wala lishe bora kwa mtoto wanachotaka ni mtoto afundishwe tu yaani mtoto akijua tu kuongea basi anakimbizwa kwa mwalimu.

Huko mwanzo watoto wa miaka 2 hadi 4 walikuwa wanashinda kwenye day care yaani vituo vya kulelea watoto mchana ili wapate uji na chakula na pia wapate muda wa kucheza kidogo au malezi changamshi mwisho wapate muda wa kulala .

Cha ajabu wazazi hawajui hilo tena wanawatesa watoto kuwapeleka kwenye mashule ya mbali huku wengine wakishinda njaa mashuleni na kubebeshwa mabegi ya madaftari huu ni ukatili kwa mtoto.

Siku hizi si ajabu tena unakutana na watoto wa miaka miwili eti wametoka shule za vichochoroni wengine wanajiita tuition wakati ni darasa kabisa lenye ubao.kibaya zaidi mtoto wa kike bado anajipupulia sasa mwalimu ni wa kiume anamtawazaje huyo mtoto?

Je siku mwalimu akiamua kumbaka? Ukweli hali ya sasa inatisha shule zimekuwa nyingi mno chekechea vituo ni vingi kuliko hata hizo day care na hizo chekechea au nursery nyingi hazina usajili na zipo katika mazingira hatarishi.

Kuna haja ya wizara ya elimu na wizara ya Ustawi wa jamii kukaa pamoja na kutenganisha hawa watoto kwa umri wajulikane wa shule ni kuanzia umri gani tusipokuwa makini baadaye watoto wetu watadumaa akili na mwili au kupata madhara Mkubwa ya kiafya huko mbeleni kwakuwa watoto wadogo hawapati lishe bora tena kwakuwa wanaamshwa asubuhi na mapema kuwahishwa shuleni.

Hivi mtoto wa miaka miwili kwenye school bus ya SAA 12 asubuhi anaenda kusoma nini shuleni? Huyu sialipaswa ashinde nyumbani na msichana wa kazi au kwenye day care?

Serikali ifuatilie hili jambo huu ndio mwanzo wa msingi mbovu wa elimu.

Asante
Wakati mnalaumu kumbukeni pia kuna sababu ambazo zinamlazimu mtoto kukaa mbali na wazazi bila kupenda. Kwa Mimi shida ni MTU wa kumwachia mtoto ilibidi nikapeleke day care na 1.5 yrs hakuna msichana anaweza kukaa mtaani kwetu yaani inabidi MTU uwaze Mara 2 ukiwaza kuzaa either uache kazi ulee sasa hiyo kazi ndio tegemeo LA kumtuza huyo mtoto. Hata ukimpeleka shule ya kuwahi kurudi huko nyumbani atakaa na nani na wewe unachelewa kufika. Yaani kuna watu wako na kazi ya kuharibu mabinti wa kazi ili waone unavyoteseka na watoto wako suluhisho waende wakashinde shuleni tukutane usiku hamna namna. Wengine imebidi wapeleke boarding sio kwa kupenda ni shida
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

🇹🇿 Nyie acheni yenu yaanze shule yakiwa mavijeba sisi tunawapeleka

🇹🇿 Nyie endeleeni kuyadekeza ya kwenu fainali kwenye soko la ajira

🇹🇿 Nyie endeleeni kuwaachia ma house girls waendelee kucheza nao sisi wa kwetu bora wakacheze shuleni

🇹🇿 Nyie wa kwenu waacheni waendelee kuangalia ma katuni sebuleni sisi wa kwetu acha wakajifunze alphabet shuleni
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Wakikusikia utasikia "kama vipi muhamishe"

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Wazazi wanazaa halafu hawataki kulea, wanajidai wanapeleka watoto shule ila sio kweli! Wanachofanya ni kuwanasukumia watoto kuepuka majukumu ya malezi

Kuna wakati unakuta vitoto vidogo miaka 2 na nusu, 3, 4, 5 boarding au kwenye school bus alfajiri unapata huruma hadi unatamani kumwomba Mungu awanyime wazazi wao hiyo pesa ya kuwapeleka huko.

Ukisikia pesa inakutumia badala ya wewe kuitumia ndio hapo
Hili suala si la kulijadili kilevilevi..

Ukiwa emotional utakuta unaroporopo tu.
 
Ni afadhari huko daslam kuna joto kuamka sio kwa mbinde sana.

Huku kwwtu baridi ni kali na kuna muda unakuta kuna kimvua halafu katoto saa 11 kanaamshwa. Aisee mi mwanangu ataenda shule saa 1 mpaka afike miaka kadhaa sio hiyo mi3 au 4 katoto kanaamshwa saa 12 ni MATESO.
 
Nyie mnashangaa wa saa 11 wakati kuna sehemu nilikua naenda kazini alfajiri kubwa mno nilipita sehemu na kiusafiri changu nikakutana na mtoto amekaa barabarani hana hata wa kumsimamia ilikua majira ya saa 10 alfajiri yupo njiani peke ake... Huwezi amini niliingiwa na hasira kama mimi ndo mwenye mtoto nilimbeba huku nikitafakari je sitafuti kuja kupewa kesi ya ubakaji wa mtoto huyu? Nilitamani siku moja nimuone tena ili anipeleke nyumbani kwao ila sikuwahi kukutana nae njia hiyo hadi leo.
 
Huu upuuzi niliukuta wakati dogo aanza Grade 1. Saa 11.30 gari inampitia halafu shule ipo km 10 tu kutoka home. Nikaongea na wazazi kadhaa wakaniambia hawana jinsi ndio utaratibu. Mbishi nikaingia front,nikatafuta wazazi 20 tukatishia kuhamisha watoto. Leo hii gari inapita saa 1 asbuhi shule ileile
 
Back
Top Bottom