Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Hii hapa saa ya mama yetu mama wa mfano ,

Pesa hizo ni madarasa 12 ya Shule hapa Tanzania nchi maskini ila yenye rasilimali za kutosha

Mama anaupiga mwingiView attachment 2911553
View attachment 2911572
Kumbuka,
Ni Rais unaemzungumzia πŸ’

hata hivyo hata PhD yake pia ulinung'unika, kualikwa kwake Rome na Pope, ulinung'unika, kusafiri kwake ng'ambo mara kwa mara manung'uniko, kuchangia mamilioni kwenye club zinazoshiriki mashindano ya kimataifa kuwatia hamasa manung'uniko, kusafiri na wasanii kwenda india manung'uniko, kuingilia katika kwake matibabu ya viongozi na wananchi manung'uniko, akisifiwa manung'uniko, na kwahiyo nung'uniko hili nalo litapita πŸ’
 
Well defended...
Ila mi nisaidie tu
.. what's wrong with 'serpenti'!?
 
Mkuu unajua hata Rais angevaa saa ya bei rahisi,hilo nalo lingekua ni mjadala pia,ujima umewaharibu sana vichwa hawa watu.
 
Sio sawa kwa rais wa nchi ambayo akina mama wanakosa maji salama au kujifungulia chini ya miti kuvaa saa ya mamia ya mamilioni!!!
Kwa mawazo haya uliyonayo,itakuchukua miaka mingi sana kuja kuelewa nilicho kiandika,endelea tu kuishi maisha ya kijima.
 
Kwa mawazo haya uliyonayo,itakuchukua miaka mingi sana kuja kuelewa nilicho kiandika,endelea tu kuishi maisha ya kijima.
Usifikiri kuwa ufahari katika nchi maskini zinazoomba omba kila ukicha ni sawa lazima tuwe na ufahamu mzuri wakati mwingine tunachekwa na wafadhili wetu. Hivi kweli hiyo misafara mirefu ya magari 50 unaona sawa tu?! Hatuna mambo ya msingi lazima tuwenayo kwanza ufahari baadaye. Viongozi wetu wanatembelea magari ya kifahari kuliko viongozi wa Uingereza au Japan yanapotengenezwa magari hayo, na ni nchi wafadhili wetu, sawa kweli?
 
Umerukia kwenye magari tena? Kwahiyo hutaki tena kujadili sasa aliyovaa rais wa nchi? Au umesha sahau mada inahusu nini hapa?
 
Tangu awe kiongozi wa nchi, Makamu mpaka Rais, pamoja na hayo, ana mume, hivi milioni hizo atakosa? Hata akiamua kukopea mshahara?
Mkuu hawa watu waliotawaliwa na fikra za kijima hua wanafikiri kuishi kimasikini ndio uzalendo,

Ndio maana hua wanawachukia matajiri,

wakiona watu wanatumia hela zao hua wanawaona wanachezea hela,

Fikra za kimasikini ni mbaya sana,huwezi kuendelea,utajikuta kila siku wewe upo pale pale tu na kazi yako kubwa ni kulaumu watu.
 
ina nini cha ziada Tofauti na saa nyinginezo?
Extravagance lives !
Ni kawaida katika third Countries !
Jamaa aliandika humu kwamba huwa tunaenda kuwaomba misaada wale ambao usafiri wao huwa ni wa Treni huko makwao ! Sisi waombaji usafiri wetu ni mavieite !!
That’s life ! Ponda mali kufa kwaja !!
πŸ˜…πŸ™πŸ™πŸ™
 
Nikijipiga na ka show-off kwa wife naweza kumpatia potelea mbali nidaiwe miaka 4
Sasa ina maana mme wake hawezi kumzawadia Valentines?

Kuna mshkaji wangu yeye na saa saa na yeye ana moja hiyo ya Β£40,000 kwa sasa ni Omega speedmaster professional
Na ni wa kawaida sana
Roho ikitaka na hela zipo fanya
Mimi sio mpenzi wa saa ila zina heshima yake
 
Ukiwa nazo zitumie ukizikosa zijutie !
Mambo ya Ujamaa tulishayatupilia mbali huko Chumbe ! Miaka ileee !!
Wahenga wenzangu wanalikumbuka Azimio letu !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…