Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Huyu jamaa bwana! Wakati anaanza nilimchukulia kama mtu wa mzaha ila kadiri alivyoendelea nikawa nazidi kuamini na kukubaliana na anachokiandika

Hongera sana mkuu kwakweli umenikosha kwa bandiko hili japo mwanzo mwanzo kule umezingua
 
Uwezo wa Mungu hauna mipaka. Ila uwezo wako wewe mwanadamu ndio una mipaka ambayo Mungu mwenyewe ameiweka kupitia universal laws . Na emeiweka kiagano..Mungu huheshimu maagano yake . Hawezi kuvunja agano lake.

# " Stop telling God how to run the world". Bohr
 
haya ndo mapokeo. Yesu alisema tusifuate. tufuate maandiko
watu walivyo waongo hivi unaanza kufanya masimulizi ya watu kuwa ndo muongozo wa kuabudu. nasisitiza tufuate maandiko, kama Yesu aliyokuwa akimjibu shetani ' imeandikwa' siyo imesimuliwa sijui na Fatima. una uhakika gani kuwa waikutana na malaika
 

Kula sukhur (daku) ni sunna (Mtume naye alikula daku). Pamoja na kutakiwa kufunga from dawn to dusk lkn tunaruhusiwa kula daku ili kukusudia kutokuwa dhaifu mchana kutwa wakati tunapofanya shughuli zetu za kutafuta rizk. Na kila unapokula chakula kdg, mathalan tende na maziwa au tende na maji basi ndio unakuwa na energy na uchangamfu zaidi. Kwani kula sana alfajiri kunasababisha energy nyingi kutumika kudigest chakula hivyo mwili kama mwili huwa dhaifu.

Wanaoshindilia chakula kingi hao ni walafi na waoga wa kufunga.

Concept ya saumu hasa Ni kuzidisha afya na kama utakula portions ndogondogo utahisi hasa kama mwili unakuwa mwepesi pasi na kuwa dhaifu.

Kuna watu hawaamki hata kula daku na next day wanafunga fresh tu.

Sijui bibie unaishi katika mazingira yepi labda ndio unaona watu wanafanya hivyo unavyosema. Au pengine mkiskia tunaruhusiwa kula usiku wa Ramadhan ndio naona sie kucha tunakula tu!!!!!!
 
Cause and effect haisemi chanzo cha uumbaji kuwa ni Mungu, ila Mungu anasema ndiye chanzo cha uumbaji wa vitu vyote katika mafundisho yake.

Hoja yako ya kuwa kuna miungu wengi ni ya kweli, mfano wapo miungu baal, jua, kuna miungu wa uponyaji, wafu, vita, n.k kwa kadiri ya watu wanavyoamini wao... Kati ya hao na wengineo wengi kuna hata mmoja aliyesema kuwa ameumba kila kitu kilichopo kinachoonekana na kisichoonekana?

Mungu wa Biblia ndiye wa kweli kulingana na habari zake katika mafundisho yake kwakuwa hizo nazo ni za kweli na kila mtu kama akitaka anaweza kuzihakikisha, na mifano ipo mingi.

Mungu anafundisha upendo kwa kila mtu na jirani yake. Mungu kama hakimu, anasema atatoa hukumu kwa wale wote wanaotenda yasiyo haki... Je, unadhani watu kama Hitler na wengineo wengi wanaoua, wanaobaka, wanaoiba n.k kuachwa tu kulingana na mabaya waliyoyatenda bila kuhukumiwa ni jambo linalofaa?

Ni kweli Biblia imeandikwa na watu, lakini ukweli na uhalisia wa habari zake unaweza kuthibitishwa kama mtu akitaka uthibitisho.

Kwanza nikurekebishe, Biblia haina contradictions, na kama unadhani zipo wewe msomaji ndiye usiyeielewa. Waweza weka hapa hizo unazodhani kuwa ni contradictions tukazijadili pia.

Tukija kwenye kuamini kwangu katika Mungu kwa sababu ya kutokujua vizuri Quantum Physics ninakubali... Na kwa uelewa wangu mdogo kuhusu Quantum Physics ni kwamba haikanusushi "Causality" na infact principal ya causality ni moja kati ya ambazo QP inaifuata na kuirespect na hivyo causality kusaidia kuhitimisha kuwa QP na relativity haziko inconsistent kivile..

Quantum field theory ambayo ndio bora mpaka hivi sasa inakubaliana na "cause and effect" katika level zote za ki microscopic na macroscopic. Si hivyo tu, process mbalimbali za QP zinahitaji energy au energy conditions kadha wa kadha ambazo tunachukulia kama causes ambapo bila hizo process za QP zisingetokea

Bado theory ya QP ni dhaifu sana kupinga theory ya cause and effect kama msingi wa uumbaji kwasababu inaitegemea.

Japokuwa wanasayansi wamefanya experiments zilizothibitisha kuwa causal order imekuwa disproved hakuondoi ukweli kuwa sababu ya vitu kuwepo ni uumbaji maana haitoi alternative na majibu ya keleweka juu ya uwepo wa vitu na ufanyaji kazi wake ila Biblia ndiyo inayotoa majibu ya kueleweka.

Kwa upande ulioongelea kuhusu time reversibility hakuna aliyewahi ona hicho kitu kikiwa in real world operation...

Hivyo siku zote athari zitatanguliwa na causes zake...na speculations zingine zote zilizobaki zinazopingana na ukweli huo ziko kwaajili ya kuleta confusions na kuzuia watu wasimwamini Mungu including you my friend...
 
Umeongea ukweli kabisa... Hawa watu wanapotea kwasababu hawajitahidi kijitafutia ukweli kwa kuyasoma maandiko na kuyaelewa

Kwa mfano wanalitukuza jina la Mariamu kuliko Jina la Yesu ambaye ndiye aliyekuja kwaajili yao

Inasikitisha
 
Msamaha kwa mtu hupataikana kwa kukiri yeye mwenyewe kwa kinywa chake, sio kwa kuombewa

Soma maandiko
 
Mungu amesema yeye ni chanzo cha uumbaji wapi?

Na unahakikishaje kasema Mungu, si watu tu wamesema Mungu kasema?

Unasema Biblia haina contradictions, niziweke hapa uzipangue moja baada ya nyingine?
 
Nakubali hoja yako juu ya kufunga. Wasio waislam wafunge kama waislam au hata water fast inafaa?
 
"Sisi tunakula saana usiku" ulitushuhudia bibie, au unazungumza kile unachosikia..

Mtu kula saana ni juu yake lakini nimekueleza kuwa dini haitufundishi kula kupitiliza hilo moja..
Pili jaribu kifunga siku moja, kisha ufuturu uone kama utakuwa na jeuri ya kula saana, ukila futari pale hutamani kula tena, na kula daku usiku mwingi ni sunna(kuna baraka nyingi ndani yake)

Nimefuturu saa 12-1(jioni kwa usiku) baada ya hapo sili(sina hamu ya kula) nakuja kula daku saa 8 usiku baada ya hapo sili tena mpaka alfajiri inapoingia na kuianza swaumu unasemaje hapo nimebadili ratiba,unasemaje hapo ninakula saana!?[emoji848]
 
Unaona sasa ndugu yangu, hapo ndio tatizo lilipo mnasoma kwa mihemko(unasoma ukiwa na jibu lako kichwani) umeenda kukopi sehemu, wewe walichokiandika umekibeba kama kilivyo umejaribu kumtafuta sheikh akuelezee walau kidogo ndugu yangu!? maswali yoote hayo sijui nikujibu lipi na na lipi kufuta hizo contradictions unazozisema wewe..

Elimu ya dini ya kiislaam ni pana saana, kama(ama zaidi) unavyoziona elimu nyingine.

Mtoto wa darasa la kwanza ukiwambia 2-4 anakujibu haiwezekani sababu ndio elimu yake imeishia hapo, ila ukisogea mbele anakwambia ni -4.
Sasa hii tunaita contardiction?
2/4(2÷4) atakwambia haiwezekani (ama hakuna jibu[emoji23]) lakini akisogea mbele jibu lipo akitaka ataisimplfy, ataweza kuweka ktk asilimia, ataweka katka decimal nakadhalika.

Mtoto wa form 1 akifundishwa density ama umeme anaona ndio kamaliza ila kadri akisogea mbele madude yanakuja tu..

Tujitahidi kusoma hali hatuegemei upande nitajaribu kukufahamisha taratibu kadri nitakavyojaaliwa kaka.

Tuseme inshaallah.
 
Nakubali hoja yako juu ya kufunga. Wasio waislam wafunge kama waislam au hata water fast inafaa?
Waislam Tunafunga sababu ya kiimani, lakini ndani yake kuna faida kedekede(somo oana kidogo), kwakuwa mola aliyetuumba ndio katuamrisha hivyo tunafunga kwa sababu yake yeye(kasema)tuwe wenye kufaulu kupata yale aliyotuahidi, lakini mtume anasema fungeni mtapata afya, kumbe ndani ya kufunga kuna faida moja wapo ya kupata afya, hivyo kwa asiekuwa muislam akifunga hatapata malipo kutoka kwa mola, ila anaweza pata faida za kiimani(mfano anapokaa na njaa hali anauwezo(ana mchele ndani na kila kitu/pesa ya kununulia msosi wa nguvu) wa kununua chakula lakin hanunui sababu kafunga basi anaweza kupata imani(kuwaonea huruma) wale ambao huwa hawali sio sababu wamefunga la hasha ni kwa sababu hawana chochote cha kukila, anapokamatwa na kiu na hanywi maji sio kwamba hana buku jero ya kununua Kilimanjaro la hasha ni sababu kafunga, anaweza kupata imani kuwaonea huruma wale ambao huwa wanashindwa kunywa maji sio hawana kiu ni vile hawawezi kuyapata maji(hivi ndivyo dini inataka, tuhurumiane, ndio msingi wa dini)

Na mwishoni ni huko kupata afya ya kimwili, ukifunga mchana kutwa kisha jioni, ufuturu glas ya maji, ule hata vijiko kadhaa vya tende ama chakula chochote.. Kisha aidha baadae ule daku/ama usile kisha kesho uendelee na swaumu kuna faida ya kiafya.. Hi ni kwa muislam na ambae si muislamu.

Kuna sunnah ya kupiga mswaki, kuna faida ya kiimani na ya kiafya, ukiacha utapata madhara ya kiafya na unakosa vitu fulani kiimani.. Ukipiga afya unaoata na kiimani kuna mambo yanaenda sawa sawia..

Nadhani nimejitahidi kukujibu ndugu yangu
 
Jibu maswali acha longolongo, hakuna Sheikh wa kuweza kujibu hayo maswali zaidi ya kukuambia elimu ya Quran ni pana sana na wewe huwezi kuielewa kwa sababu huelewi Kiarabu.

Yani hiyo habari ya elimu ya Mungu kuwa complicated na kushushwa kwa lugha fulani tu inaonesha huyo Mungu hayupo, katungwa na hao Waarabu.

Angekuwepo, wala tusingehitaji kitabu kumjua kwa uhakika.

Elimu ya uwepo wake ingekuwa hardcoded kwenye DNA kwa kiasi ambacho asingeweza kupingika na mtu yeyote.

The fact kwamba mnahitaji vitabu kumuelezea Mungu inaonesha huyo Mungu katungwa na watu tu, hayupo kiuhalisi.
 
Kwanza kabisa thibitisha Mungu yupo kabla ya kusema uwezo wa Mungu hauna mipaka.

Ili tujue yupo na hiyo habari ya "uwezo wa Mungu hauna mipaka".

Nimekutaka uthibitishe Mungu yupo.

Umelialia na kutaka vigezo vya uthibitisho.

Nimekupa vigezo 10 vya kuthibitisha Mungu yupo.

Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.

Acha longolongo za maneno ya hadithi tupu yasiyo na uthibitisho.
 
Mkuu hivi unajua hata nyie waislam kuaminiana wenyewe kwa wenyewe ni shida. You can't even come to the agreement about lini muanze kufunga mnapishana kuhusu tarehe na mambo mengine
 
mkuu asante kwa somo zuri.. Kwahiyo mimi nikiamua kufunga mwezi mzima lakini sio mwezi wa ramadhani (kwa mfano niamue kufunga mwezi mzima mwezi july mwaka 2021) sitapata hizo health benefits?
 
Kwanza kabisa Mwili haujui mwezi wa Ramadhani Shaaban wala mwezi wowote ule, hayo ni maswala ya miezi wala hayana msingi wowote katika mwili wako

Kwahiyo kuhusu kufunga kwa sababu za kiafya mtu anaweza kufunga wakati wowote ule na akapata benefits husika,

Kuhusu hayo mengine uliyosema sioni haja ya kuyajadili sababu hayahusiani na swala la kufunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…