Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Duh! Hii imetulia kweli kweli. Fikiria kama kila ziara amekaa siku mbili, hii ina maana ya jumla ya siku 634; chukulia kuwa kila safari anakwenda na mlinzi wake, waziri mmoja na katibu mkuu mmoja tu - yaani msafari wa watu 4 peke yake. Kisha waza kuwa yeye analipwa posho ya Shs 500,000 kwa siku, Waziri posho ya Shs 375,000/siku, katibu mkuu alipwe posho ya Shs 325,000/siku na mlinzi wake alipwe posho ya Shs 250,000/siku. Kumbuka hizo posho ni makadirio tu.

Kwa muda wa siku 634 hawa waheshimiwa 4 watakiwa wametumia jumla ya Shs 919,300,000 [(Shs 500,000+375,000+325,000+250,000)/siku*634siku].

Hii ni sawa na visima vya maji 61 kwa wastani wa bei ya Shs 15m kwa kila kisima (shs 919.3m/15m); hivyo ndani ya miaka 4 kama mkulu angeamua kupunguza safari angeliweza kuwajengea wana Igunga wastani wa visima 2 kila kata (61visima/26kata).

Ninawaza tu kama mpita njia.
 
Hii ni hatari! Ina maana katika kipindi chake cha kuwa madarakani mpaka kufikia sasa, ametumia karibu miaka mi2 akiwa nje ya nchi. Hivi kweli tuna rais! badala ya kutumia muda huo kuhamasisha maendeleo ya wananchi mijini na vijijini......yaani ziara za nje ni mara 10 zaidi ya ziara za ndani! ama kweli jk ni mtalii.
 
Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005

UPDATES

Mpaka leo tarehe 23/8/2011 tayari amesha safiri safari 315 tangu aingie magogoni octoba mwaka 2005
Hii ni rekodi ya kipekee duniani ambayo watz tunatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele maatako nyuma

UPDATES

Kesho tar 9/9/2011 rais atasafiri kuelekea Kenya kwa ziara ya kikazi
Hiyo ni safari ya 316 tangu rais aingie madarakani mwaka 2005!

UPDATES:

Safari ya 317 kwa rais wangu kipenzi!
ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa hasara.mia

Jamani kwa wale wenye data ya siku ambazo Mzee wa Magogoni Mjomba wetu aliishi nje ya nchi waweke hapa jamvini ili tuone ni miaka mingapi Mzee ameishi nje ya nchi. Si ajabu ukaona anajumla ya miaka minne tu kuwepo nchini tangu aingie pale Magogoni 2005. Mungu Ibariki Tanzania wabariki viongozi wake ...............
 
Ondoa hofu mkuu hayo yote yataainishwa na kila kitu kitakuwa wazi! Hii ni nchi yetu na JK ndiye rais wetu!
 
huyu jamaa jana alikua anaishauri serikali juu ya suala la umeme! hii ni kali kwani inaonesha yeye hayupo kwenye serikali.Kuna mwinginwe anayetakiwa kutoa maamuzi ya Tatizo na taswira ya mathara ya umeme
 
Hivyo ni sehemu tu ya vituko vya rais wetu kipenzi!
 
Rais wetu kusafiri hakuna ubaya wowote kwa sababu ya vikao mbalimbali vinavyomhusu sharti ahudhurie na aiwalikilishe nchi yetu itakuwa ni aibu kama nchi inakosa mwakilishi wakati Rais yupo na ni mzima wa afya, pia kuna mialiko kutoka kwa marafiki zetu, ubaya kama anaenda kufanya matanuzi. Tusibakie kuhesabu vikao ila tuangalie na sababu za safari zake
 
Hamjui kuwa jamaa yetu wa magogoni ni Dakta magumashi! Yupo kwenye safari za utafiti aandike pepa kwaajili ya promosheni.
 
tanzania bana tunkoelekea sio kwema cjui umhimu wa hizo safari mbona mseven kibaki na nchi zingine hawasafiri kiasi hicho na nchi zao zinapiga hatua ktk maendeleo ce nyuma tunarudi
 
Anatumia kodi yetu kwa manufaa yake badala ya kutuhudumia na kutueleza eti maendeleo bila ya wawekezaji haiwezekani!
 
Anatumia kodi yetu kwa manufaa yake badala ya kutuhudumia na kutueleza eti maendeleo bila ya wawekezaji haiwezekani!
Nimesoma makala moja kwenye blog ya yerickonyerere.wordpress.com hakika nimeipenda hii hapa!

From: @YerickoNyerere
Sent: 15 Oct 2011 21:45

Serikali ya Madalali na Vishoka Pamoja na Sera za Kuuza Nchi: Soma zaidi http://t.co/8YNtbNnR /via @wordpressdotcom
 
Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005

UPDATES

Mpaka leo tarehe 23/8/2011 tayari amesha safiri safari 315 tangu aingie magogoni octoba mwaka 2005
Hii ni rekodi ya kipekee duniani ambayo watz tunatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele maatako nyuma

UPDATES

Kesho tar 9/9/2011 rais atasafiri kuelekea Kenya kwa ziara ya kikazi
Hiyo ni safari ya 316 tangu rais aingie madarakani mwaka 2005!

UPDATES:

Safari ya 317 kwa rais wangu kipenzi!
ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa hasara.mia
Usimhangae sana huyo JK anakwenda kwatafuta wa kubadilishana madini yetu na neti zenye sumu
 
"Safari ya Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 16 na 23 Septemba, 2011 nilifanya ziara ya kikazi nchini Marekani. Nilikwenda kuhudhuria Kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na shughuli zake. Pamoja na hayo nimehudhuria mikutano mingine kama vile Mkutano wa Open Government, ulioitishwa na Rais Barrack Obama wa Marekani,Mkutano wa Umoja wa Marais wa Afrika wa kupambana na malaria ,Mkutano wa Tatu wa Watanzania Waishio Marekani (DICOTA 3) na mkutano kuhusu Wanawake na Lishe ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hilary Clinton. Aidha, mimi na Waziri Mkuu, Stephem Harper wa Canada tulipata nafasi ya kuwasilisha taarifa ya Tume ya Afya ya Mama na Mtoto aliyoiunda Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambayo tulikuwa Wenyeviti wenza. Nafurahi kwamba taarifa yetu imepokelewa vizuri na kuelezwa kuwa itakuwa msingi mzuri wa kutatua matatizo ya vifo vya kina mama na watoto duniani.
Katika hotuba yangu kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nilieleza jinsi nchi yetu ilivyoshiriki katika shughuli za Umoja wa Mataifa katika miaka 50 ya Uanachama wetu ambayo pia ndiyo miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 47 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Nchi yetu inayo historia iliyotukuka kwamba, pamoja na udogo na umaskini wetu, tumetoa mchango muhimu katika shughuli za Umoja wa Mataifa za kudumisha amani na usalama wa dunia na kuleta maendeleo. Tunayo fahari kwa mchango tuliotoa mpaka sasa. Niliwaahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa na kuendelea kutoa mchango wake ipasavyo." Ikulu Mawasiliano: HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WANANCHI, TAREHE 30 SEPTEMBA, 2011

==+++===+======++====+++===================

Jamani mi nilikuwa napita tu, CV ya Rais ya mwezi mmoja mi sawa na maisha yangu yote hapa Tanzania. Kwanini nisiachane na UALIMU au UDAKTARI, UKULIMA na PROFESSIONAL ZINGINE nikimbilie UBUNGE kama unavuta salio kiubua namna hii.....
 
Nasikia safari nyingine inaandaliwa kwenda Australia, Perth nazanii hii atahitaji wapambe wengi sijui ni ya CHOGAM hata sijui ndo nini hio lakini inahusu nchi zilizo tawaliwa na uingereza yani badoo tuu tunawaabudu hawa makaburu.
 
Safari ya 318 ya baba Riz moko!

JK anaondoka leo kuelekea Australia kwenye mkutano wa jumuiya ya madola...wakuu huku taifa likiwa katika mtindio wa upukutishaji hazina, Ikumbukwe kuwa mishahara ya wafanyakazi wa serikali itachelewa kutokana na hazina kuwa nyeupeeee labda pesa ya marehemu Gadafi tufanikiwe kuizima japo Membe anaitolea macho ile mbaya!
 
Yaani mkutano unaanza Ijumaa mwisho wa wiki yeye ameondoka tangu Jumatatu mwanzo mwa wiki..haya ni maajabu ya dunia!!
 
Back
Top Bottom