Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Mkuu Jason bourneupdate juu pilot kwa sasa yupo Muscat anakula tende kwa siku 3..itakuwa safari ya 337 kama sijampunguzia....
 
Last edited by a moderator:
Nimemuona jana muscut akishangaa kinywa wazi jumba la kifalme,akiwa na b,membe safari ya 337 kwa miaka saba tu!
 
Hivi rais wa TZ angekuwa kama wa malawi halafu asafiri hivi mngesemaje?
 
sijawahi kumuona rais mshamba kama huyu. Yan utoto tu.
 
Aibu yetu watanzania, tutaibeba hadi 2015, hasara juu ya hasara anatupatia kama taifa, maskini ka p.a.y.e kangu ka kila mwezi kanatumika hovyo
 
Hii ni ya 338 kwa sababu Jason bourne haku-update safari ya 337 iliyokuwa ya Canada. Just kuweka record sawa sawa.
 
Kuna jamaa tayari ametaarifu jukwaa kwamba leo hii mkuu amegonga safari ya 337.

Kama taarifa hizi ni sahihi basi inamaana kiongozi huyu wa taifa letu masikini, lenye msingi wa kodi ya kuungaunga, atakua amebakisha safari nyingine kama 29 tu ili awe ametimiza mwaka mzima mawinguni.

usisahau nyingi ya safari uchukua si chini ya siku mbili kwa maana hiyo baada ya safari 29 atakuwa ametumia miaka 2 kati ya saba akiwa anaongoza nchi akiwa nje ya nchi
 
Mud naomba uitengenezee chati ya kupigia kura

Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005 (nimeinukuu kwa Jasson)
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amerejea Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya siku tisa katika mikoa minne ambako amekagua, kuanzisha ama kuzindua miradi 19 ya maendeleo na kutembea kiasi cha kilomita 2,770.

Wadau wa JF anastahili pongezi au????
 
Kwa hili anastahili pongezi kwa kweli. Anatakiwa afanye safari kama hizi nyingi zaidi ya alivyofanya sasa. Hebu jiulize tangu kachaguliwa hakuwahi kutembelea Arusha. Lakini USA kaenda mara ngapi na ndio mbali zaidi. Mkuu akumbushwe kuwatembelea wapiga kura wake na wasio wake mara nyingi kadiri inavyowezekana. Akumbuke kuwa yeye anapotembelea mahali huwa anakuwa chachu ya viongozi wazembe kufanya kazi.
 
Umbali sio hoja..Muhimu ni yale alokwenda kuyafanya huko mikoani.
 
Hiyo ndio kazi yake si kudandia pipa kila kukicha na kuja na story kibao ohh nisinge safiri ohh wahisani nk... nchi yetu ina uwezo wa kujiendesha yenyewe kama rasilimali zitasimamiwa vema, hivyo ni vema akapambania humu humu ndani kuliko kuzurura huko nje kuomba ufadhili.
 
Katika Mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete alianzia ziara yake Oktoba 28, mwaka huu, miongoni mwa mambo mengine alikagua nyumba za wahanga wa maporomoko ya mwaka 2006 kwenye kijiji cha Goha na akafungua Kiwanda cha Kusindika Tangawizi kilichoko Mamba Miamba, Wilaya ya Same, na akafungua Shule ya Sekondari ya Kata ya Asha Rose Mingiro iliyoko mjini Mwanga.
 
KAMA HAITOSHI Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro alifanya uzinduzi wa barabara za Rombo Mkuu-Tarakea na Kwasadallah-Masama na akafungua Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (NAO) mjini Moshi.
 
Katika Mkoa wa Arusha, Rais Kikwete alizindua Hospitali ya Wilaya ya Arusha ya Olturumet, akazindua Mradi Mkubwa wa Uboreshaji wa Miji kwa kufungua barabara za Jiji la Arusha, akazindua Jiji la Arusha, akafungua rasmi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela na akatembelea Kiwanda cha Nguo cha A-Z. Kabla ya kuondoka Mkoani Arusha, Rais Kikwete alifungua Shule ya Msingi ya Sokoine na kuzindua ukarabati mkubwa wa Barabara ya Minjingu-Arusha.
 
Back
Top Bottom