Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Unaweza ukampata mmoja ukaona amekamilika,ukajiambia huyu naona sasa.kumbe nae kakusoma nkaona humfai anaenda zake.
Bado kazi Iko palepale
Duhhh mapenzi ni changamoto sana, wale ninaowataka siwapati, ila wale ambao siwataki ni simple kuonekana, ni hivyo hivyo kwa upande wa pili.
 
Sasa katika harakati za kutafufa Ma mtu org unatakiwa upigwe tukio Moja takatifu ili kongosho ichanganyikane na bandama utokwe na kamasi zito hapo ndo akili ya kumpata ma mtu itajidhihirisha
. zipo za kuachika ila machozi hayawezi kutoka mkuu... 😅😅😅,

. Unapenda Kiasi gani mpaka unafika hatua hiyo mkuu??
 
Kama anatafuta malaya/wadangaji yaani chapa ilale ni sawa kutanguliza hela, ila mke ukitanguliza hela ushabugi. Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi na hasa changamoto za uchumi ndizo huwakimbiza wanawake.

Kipimo kimoja wapo unacho takiwa kumpima mwanamke ,akili yake kupitia fedha unayo mpa (tena mpe na ziada) na ustahimilivu wake wakati unapopitia changamoto za uchumi, hapa unaweza hata kumuigizia umuone heshima yake kwako itaendelea kuwa vilevile.
Changamoto ya kiuchumi unapoteza mke sasa , anaweza kuondoka kabisa .
 
. zipo za kuachika ila machozi hayawezi kutoka mkuu... 😅😅😅,

. Unapenda Kiasi gani mpaka unafika hatua hiyo mkuu??
Oi wengne wanapenda had wanajinyonga ww unashangaa kutokwa na kamasi zito 😂😂😂😃😃
 
Hapana bro siyo hivyo

Mwanamke siku zote anataka mwanaume mwenye pesa hata kama asipopewa pesa na huyo mwanamume

Lakini lazima hela kwanza uwe nayo umpe au usimpe hayo ni juu yako

Kapuku kupata mke mwema ni changamoto sana
.tuache kudanganyana
Sawa sawa muinjilist , ila hata ukiwa ni mtu mwenye mafanikio ya kawaida , mke anaona kama leo mna nyumba mwaka mmoja mbele umenunua gari au shamba basi hapo anaona huyu kweli kidume , ila ukikaa stationary hakuna prgress jiandae atakimbia tu .
 
. Yes umeongea Point mkuu, ngoja nizidishe maombi zaidi, pengine naweza bahatisha aliye sahihi..

. Sura, rangi, kimo, siyo pendekezo namba moja kwangu, bali natafuta mke aliye sahihi ( nahisi hawa viumbe wa Aina hii wameadimika sana l
Nina ndugu yangu ametulia sana na anajielewa yupo single 25 ila amekosa kigezo cha shape.
 
Nina ndugu yangu ametulia sana na anajielewa yupo single 25 ila amekosa kigezo cha shape.
. Shape yake ikoje mkuu 🙂🙂🙂,??

. Mlete Mtoto huyo niongee naye mezani
 
Maisha ya mapenzi yamejaa comedy na stress kwa wakati mmoja, Naona ni ngumu sana kumpata mwanamke mzuri wa kuoa, Tayari ni takribani miaka miwili na miezi minne tangu nianze kuamua kutafuta mtu wa kuoa lakini bado sijafanikiwa.

. Safari hii imekuwa ya mizunguko na drama kibao hadi sasa, na kwa kweli naona kabisa nimeanza kuchoka kutafuta mke wa kuoa . Nahitaji mke ambaye tunalingana kitabia na kimtazamo kwa kiasi fulani. Sitaki mtu mwenye hasira za haraka au mwenye ukaidi au asiye na kifua( kilopo lopo). Nahitaji mke mwenye Uelewa wa maisha, mtunza siri za maisha na anayeweza kulea familia kwa ufasaha ikiwezekana kabisa asiwe anacheza VIKOBA.

. Kila uhusiano nitakaogusa naona kabisa huyu hafai kuwa mke bali anafaa kuwa mwanamke katika upande wa kiburudisho tu, ni ajabu sana aise,

. Cha kuchekesha kwa sasa ni kwamba nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi na rafiki yangu wa kike ambaye tumedumu naye kwenye mambo kadhaa ya biashara lakini bado naona hafai kuwa mke bali naona anafaa kuwa mwanamke tu. Wakati mwingine najihisi mjinga kwa kujaribu kuwa naye.

WanaJF, Inakuwaje kuwaje mpaka unafika hatua ya kusema yes huyu ndiye anafaa kuwa mke/mume wangu..??? 🤔🤔🤔
Dah pole sana kaka .
Lakini ukweli ni kuwa nakupongeza kwa uwezo wa kujitambua kiasi cha kuamua kutafuta mwenza kwa kuweka mipaka yako kadha wa kadha .
Walio wengi ndoa uwa inakuwa kama ajali isiyo na mipango ya awali .
Utampata wa kufanana naye,endelea kutafuta yupo ila atachelewa kwa kiasi chake .
 
Ni kweli mkuu, na jitahidi kutafuta mke kwa utaratibu zaidi, maana changamoto ya sasa inayowakumba vijana wengi ni kutafuta mke asiye sahihi, hii ndo chanzo cha mifarakano ndani ya familia, na inaweza kufika mbali zaidi kushinda kufanikiwa kwenye maisha.
 
Nahitaji mke ambaye tunalingana kitabia na kimtazamo kwa kiasi fulani. Sitaki mtu mwenye hasira za haraka au mwenye ukaidi au asiye na kifua( kilopo lopo). Nahitaji mke mwenye Uelewa wa maisha, mtunza siri za maisha na anayeweza kulea familia kwa ufasaha ikiwezekana kabisa asiwe anacheza VIKOBA.
Umetumia maelezo marefu kufafanua juu ya kiumbe ambacho hakipo.

Badala ya hayo maneno yote hapo ungesema tu kuwa:-

'Natafuta Tomboy'

Huyo pekee ndo anakuwa na sifa hizo, vinginevyo utasubiri sana broh
 
Umetumia maelezo marefu kufafanua juu ya kiumbe ambacho hakipo.

Badala ya hayo maneno yote hapo ungesema tu kuwa:-

'Natafuta Tomboy'

Huyo pekee ndo anakuwa na sifa hizo, vinginevyo utasubiri sana broh
TOMBOY ndo wanasifa hizo??. Maana sina experience na hao watu.
 
Kwa utafutaji huo wa mke inaonyesha unataka mkamilifu, wakati ukamilifu upo mbinguni..kila mwanadamu ana upungufu wake kwa hiyo tafuta mwanamke umpendaye kwa kuwa na vigezo vichache vyenye kuufurahi Moyo wako uwapo karibu yake na yeye awe ni mwenye kukuheshimu yaani mwe ni wenye kuelewana..mengine ni kuvumiliana maana hakuna mkamilifu zaidi ya hapo utakuwa unamtafuta malaika.
Mkuu agiza bia hapo
 
Ni kweli mkuu, na jitahidi kutafuta mke kwa utaratibu zaidi, maana changamoto ya sasa inayowakumba vijana wengi ni kutafuta mke asiye sahihi, hii ndo chanzo cha mifarakano ndani ya familia, na inaweza kufika mbali zaidi kushinda kufanikiwa kwenye maisha.
Mkuu toka mwezi May bado hujapata tu ?
 
Back
Top Bottom