Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Mkuu kwani kuna nini?
Mm sijakuelewa kabisaa! Naona unalalamika tu. Serikali inajenga sanamu kwa ajili ya nani?

Naomba unijibu ili nianze kutapika nyongo.
 
Tupo uchumi wa kati.

Tumeongeza tozo za Petrol ili tuharakishe ujenzi wa sanamu.

20210704_191334.jpg
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Mkurugenzi wa TanTrade Rutageruka Sabi amesema kuwa, ujenzi wa sanamu hilo unalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa Hayati Dkt Magufuli katika kuinua uchumi.

Naona wamekurupuka wangejenga Chato au Dododoma. Vilevile brand ya Magufuli haikuwa biashara ni ujenzi na uzalendo hivyo sijui itasaidia vipi sabasaba!
 
Tunalo tatizo la elimu nchini, hatuna madawati yakutosha, hatuna waalimu wa kutosha, hatuna vitendea kazi ikiwemo vitabu then yupo mtu amekaa wizarani huko amesoma sanaa na utamaduni anawaza kuidhinisha M420 kwa ajili ya sanamu kweli...
Aahahaha CCM bhana wanataka tena kuusimamisha sanamu ya mfalme Nebuchadnezzar
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Mkurugenzi wa TanTrade Rutageruka Sabi amesema kuwa, ujenzi wa sanamu hilo unalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa Hayati Dkt Magufuli katika kuinua uchumi.

Aahahaha ccm bhana wanataka kusimamisha sanamu ya mfalme Nebuchadnezzar tena
 
Back
Top Bottom