Shadeeya kwakweli mmetuweza. Lakini lawama zinatuhusu sisi wenyewe, hasa muwekezaji wetu na viongozi wengine pia
Kwa namna kunavyokua na urasimu na kusitasita katika kutoa pesa za usajili, hayo ndio matokeo yake na haikuanza leo na haitakua mwisho
Tangia enzi za kina Stephano Azizi Kii, Pacome na hata huyu Okello Simba imekua ya kwanza kuanzisha mazungumzo lakini wanajivuta kutoa pesa
Lakini ukitaka kumlaumu sana Mo utakutana na suala jingine. Kuna wakati pesa zilikua zinatolewa kwa wepesi ila sasa wahusika wakawa wanampiga Mo kwa kutuletea magalasa kina Mukwala, Mutale, Mugalu, na wengine kibao
Tena kwa mbwembwe zao wanaanza kuongea na watu wa vijarida vya michezo wanawapamba hao magarasa kiasi mnadhani wanakuja watu wa kuoigania vikombe vya Afrika kumbe dizain kama zile mlizokutana nazo nyinyi za kina Yikpe