Bila hata kusikia sauti unaweza kumwelewa mtu jinsi alivyo. Maana Biblia inasema: “Yamjazayo mtu ndiyo yamtokayo” – yaani, tabia za kweli za mtu hazifichwi, huonekana kupitia kile anachosema na hata kuandika. Kwa comment chache tu, mtu anaweza kujionyesha kama ni mlevi, mzinzi, mwenye hasira, mwongo au mchochezi.
Ndugu zangu, maisha ni mafupi. Leo tunacheka cheka tu kwenye comments, kesho tunaweza kulala bila kuamka. Kama bado hujatubu dhambi zako na kumpokea Yesu, leo ndio siku ya wokovu. Acha mizaha ya ulimwengu huu, mgeukie Mungu kabla mlango wa rehema haujafungwa. Yesu anakuita sasa,
Ufu 3:20
"Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami."
Mathayo 3:2
"Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."