GE2025 Sekeseke lililotokea wakati wa kuchukua Fomu ya Ubunge katika Jimbo la Bumbuli

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii nchi hata ungekuwa ww ndo Mbunge hakuna Ambacho ungebadilisha kwakuwa mifumo alioacha Nyerere haijawahi kubadilishwa Ila inaendelezwa.
Sijui ulikuwa unalenga kitu gani hapa; lakini kusema CCM hii ndiyo aliyoiacha Nyerere, sijui kama umelitafakari vyema hili!
Jina, SAWA. Muundo. SAWA. Lakini matendo ni mbalimbali kabisa; 'actually', ni kinyume moja kwa moja.
 
Sema hili la Makamba kuwa mtoto wa kufikia ni uongo, huyo ni mtoto halali wa Mzee Makamba na halina hata ubishi kwa wanaomjua na ni kutafuta tu mada ya kujadili kumuita mtoto wa kufikia. Mengine ni kweli kabisa huyu hajakulia huko kwasababu hata baba yake alikuwa haishi huko kutokana na shughuli zake za Uongozi.
January alipelekwa Bumbuli kulipiza kisasi kwa Mzee Shelukindo baada ya Makamba Sr kushindwa kila alipojaribu kutia nia jimbo hilo ndio akamuapia Shelukindo kumletea mtoto ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kijana wa Ikulu na mpika fitina mzuri wa JK.
Kwa kifupi jamaa haijui Bumbuli na wala hana mzuka nayo kabisa ni vile tu ndio tiketi yake rahisi ya kupata ubunge.
 
Upumbavu mtupu. Jimbo la Bumbuli sio private property ya familia ya Makamba!
Mbona wakiambiwa reforms wanakataa? Nchi inahitajika reforms ili kila mtu awe huru kugombea nafasi yoyote bila vitisho. Huyo Makamba amekaa miaka 15 lakini ni kama popoyo anayejaza nafasi bungeni. Nchi inauzwa yeye kimya. Hii ni kwa sababu anajua wananchi siyo wanaoamua.
 
Mtoane tu macho,tujue nani mlafi zaidi ya mwingine,hapo ni fomu ikifika kwenye kura?Je vipi na ikifikia kampeni.?Yetu Macho.
 
Majimbo yenye wabunge wazawa yanalizidi nini jimbo la Bumbuli?
 
Atakuwa amezidi ujeuri huyo January! Ameshindwa kujenga hata vyumba viwili na sebule vya kuzugia. Unajua majimbo ya vijijini waapenda wamuone mbunge ana mji jimboni kwao?

Kwahiyo January akienda Bumbuli huwa anafikia hotelini au kwa baba yake?
 
Atakuwa amezidi ujeuri huyo January! Ameshindwa kujenga hata vyumba viwili na sebule vya kuzugia. Unajua majimbo ya vijijini waapenda wamuone mbunge ana mji jimboni kwao?

Kwahiyo January akienda Bumbuli huwa anafikia hotelini au kwa baba yake?
Anafikia Hotelini mhuni huyu
 
Lakini kweli January siyo msambaa, leo ndio nimejua, zile sifa, kujisikia, much know kumbe mhaya? Ila wasambaa wamezubaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…