Kwa nyakati tofauti mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikionya wananchi wake kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na Covid 19 kwani ugonjwa huu upo nchi jirani. Unapo zungumzia Ugonjwa wa Corona nchini Tanzania huwezi kuachilia mbali maneno Kama nyungu na kujifukiza mbinu mujarabu iliyotiliwa mkazo na mamlaka katika kuhakikisha Taifa linakuwa salama dhidi ya maradhi haya ya hewa.
kumeripotiwa vifo vingi kwa wakati huu. Kutokana na hofu ya mamlaka Basi inahisiwa wengi hawawezi katu kusema vifo hivyo vinatokana na Corona licha ya kuwa wengi wamekuwa wakihusianisha. Tanzania inaingia kwenye kundi la nchi zisizo na Covid 19 kwenye kundi lake zikiwemo pia Burundi na Korea ya Kim jong Un licha ya kuzungukwa na nchi zenye kiwango kikubwa Cha maambukizi pande zote
swali ambalo ninaomba tujadiliane Ni iwapo nchi yetu ipo salama kweli? Nitawapeni kisa Cha kweli. BBC Swahili Leo wameripoti kisa Cha mkazi mmoja wa Dar es salaam aliyefariki kwa kile familia inaeleza kukosa tahadhari. Aidha wameripotia kufungwa kwa shule ya kimataifa Moshi baada ya mwanafunzi mmoja kuugua maradhi hayo kitendo kilichopelekea shule kuomba radhi. Mamlaka imekuwa kimya kuzungumzia usahii wa taarifa za ugonjwa wa kiongozi wetu Maalim seif khatib Hamad visiwani zanzibar.
Katika wilaya X ya Kijiji K Cha mpakani mkoani mbeya wiki mbili zilizopita ulitokea msiba. Maiti iliwasiri kutoka mkoani mbeya muda wa maziko. Ibada iliendeshwa pasipo mwili kushushwa kwenye gari. Baada ya ibada gari lilisogea kabisa kaburini, vijana wanne walio kingwa na kuvishwa mavazi maalumu ndio walio husika na mazishi hayo ya ghafra mno. Swali ninalo jiuliza kwanini haya hayasemwi? Tujadiliane shuhuda basi za ugonjwa huu Wana JF.
Je, ni chukizo kwa mamlaka kuzungumzia ugonjwa huu?
Ninapo hitimisha mjadala huu nisisite kuipongeza mamlaka pia kwa kuwa na msimamo kwa mambo kadhaa, masuala Kama chanjo na barakoa za nje hazituhakikishii Sana usalama wetu.
Juzi zimeenea picha za kiongozi fulani wa nchi za ughaibuni akipata chanjo kwa uongo. Kitendo Cha Tanzania kukataa chanjo kimewachachafya Sana wakubwa. Je Nini hasa maana na sababu ya Covid 19 bado Ni fumbo..........