Duh hatari na ndio Diamond kaimba "usiniguse usinishike tusalimiane kwa miguu... coronaa coronaa"

Kutokana na huo wimbo tuchukue tahadhari.
 
Mkuu mie nina mtazamo tofauti kabisa sipo kwa wanaoamini ipo au wanaoamini Tz hakuna.
 
Kabisa bro. Vipo bado vinaendelea na kuna watu wanakutwa na ugonjwa. Sampuli zinachukuliwa nchi nzima, huwa anachakata pale mabibo TMDA, ndipo ilipo maabara. Ila matokeo ya vipimo hivyo yanabaki serikalini, labda kwa wale wanaosafiri nje ya nchi, wao hupewa cheti ili wasafiri wakiwa wanajua hali zao.
Kwa hiyo, mpaka muda huu, serikali inajua status ya nchi kwenye corona na takwimu wanazo ila hawa publish. Sisi sio kisiwa, tunasafiri na tunapokea wageni toka nchi zilizoathirika, kwa hiyo wagonjwa tunao, ingawa rate si kama tunavyoambiwa kwenye nchi nyingine.
 
Nahisi kuna ka movement cha wafanyabiashara na mabeberu wanaotaka kuirudisha covid 19 kwa kasi ili wapige hela.
SIO KWA TANZANIA YA LEO...WATAKWAMA
Umeandika kama vile Watanzania ndiyo watu werevu kuliko wengine duniani ........!!
 
Kwahiyo mkuu unasema kuwa serikali inazo takwimu za corona tofauti wengine wanavyosema hatupimi corona hivyo hatujui hali ya corona nchini?

Na vp kuhusu hizi tuhuma za kwamba watu wanakufa kwa corona ila inasemwa ni matatizo ya kupumua tu?
 
Kabla corona haijaingia afrika kila mtu aliona kuwa ikiingia afrika hali itakuwa mbaya zaidi ila corona ikaja kuingia ila hali haikuwa mbali kama watu tulivyofikiri,ila mwanzo hakuna ambaye aliweza kuliona hilo kuwa corona ikija afrika hali haitokuwa mbaya kama kwa sehemu zengine.
 
Kwahiyo wagonjwa wakifikishwa hospitali hupimwa hadi corona na ndio hao madktari wanajua kuwa watu wanakufa sana kwa corona?
Hongera mkuu ujafikiwa na hii kitu na omba sana isibishe odi nyumbani kwako. Nakuombea pia isiwe hivyo...ILA WENZIO TUMENUSURIKA .
MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE
 
Kila mtu na mtazamo wake au anavyoamini,wengine huona majirani zetu kwao hali ya corona ni mbaya sana tofauti na Tz pia wapo ambao huona Tz hali ndio mbaya zaidi kuliko majirani zetu sababu sie hatuzingatii taratibu za kujikinga na corona.

Kila mtu anasema lake.
 
Hongera mkuu ujafikiwa na hii kitu na omba sana isibishe odi nyumbani kwako. Nakuombea pia isiwe hivyo...ILA WENZIO TUMENUSURIKA .
MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE
Nimeuliza tu swali nia ni kutaka kujua,sasa kama labda sitakiwi kuuliza bora useme.
 
Kwahiyo mkuu unasema kuwa serikali inazo takwimu za corona tofauti wengine wanavyosema hatupimi corona hivyo hatujui hali ya corona nchini?

Na vp kuhusu hizi tuhuma za kwamba watu wanakufa kwa corona ila inasemwa ni matatizo ya kupumua tu?
Nadhani umenielewa. Serikali inajua status. Wanapima
 
Kwa hili la Corona na mengineyo ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania kuna serekali!
 
Serikali haiwezi kutangaza kama Corona ipo, na walichoharibu zaidi ni kipindi kile kukataza watu kujikinga ila ukweli ni kwamba corona ipo, sisi mchungaji wetu alitutangazia live ibadani, akatusihi tuendelee kuchukua tahadhari, so take care for yourself and your beloved ones
 
Ninapowapendea WaTZ ni hapa tu, ubishi na ukweli anaujua!!

Tanzania si kisiwa kwamba usiingie, kasema alikuwa na dalili kama....!! Mtu anauliza hakuna magonjwa mengine!! [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Na kila siku tunapokea wageni sijui ndio wanaitwa watalii kutoka nchi za nje. Mungu azidi kututunza kwa uwezo wake
 
Hii ya kudiscourage watu kujikinga, kufanyia mizaha barakoa, kila mara kutangaza kuwa korona haipo iliwafanya wananchi wengi washushe guard zao na wengine waamini moja kwa moja korona haipo!. Sasa ikipiga tena inawakuta wananchi wamerelax hawana habari!.

Bado najiuiza kulikuwa na haja gani kila mara raisi anapiga vijembe barakoa, mara aziote zinafanana na titi la mwanamke lililokatwa, mara aziite mavitambaa ya puani, mara awasifu wale wanaozivua katika mkusanyiko wa watu wengi!

Msimamo sahihi ingekuwa ni kuwatangazia wananchi kuwa korona imepungua, lakini bado ipo na wananchi waendelee kuchukua tahadhari, Hii ingesaidia kama wimbi la pili au la tatu ingepiga wananchi wawe aware!

Kuna watu wanadhani majority ya wananchi wana ufahamu na wako aware na masuala haya kama wao kumbe ni vice versa, hawa wanahitaji nguvu ya serikali kuwaelewesha kuchukua tahadhari
 
Well said mkuu

Mapambano ya covid-19 hapa TZ yameachwa kwenye ngazi ya familia. Tujilinde!
 
Jamani kwenye hili swala la Corona nipo na Magufuli. Nyie mnaolalamika mmekatazwa ku take precautions? mmeambiwa msinawe mikono au kuna mtu amekatazwa kuvaa barakoa? Hebu kama mmepewa neema ya kutougua na hamuugui why kelele kelele kila siku mara ooh ugonjwa upo,Yess ugonjwa upo lakini una impact kubwa kama mnavyosema?.mnataka aitangazie nchi kuna corona watu wafe kwa presha?.watu wakose amani na kujifungia? sasa kwa taarifa yenu watanzania tuna survive kwa sababu ya huu muingiliano tunaopata kila kisu kati ya watu na watu tuna exchange virus tunaugua mwili unajenga immunity zake. Hizi shughuli za kila siku tunashinda juani ni tiba tosha. Hatuna hofu hii ni tiba kubwa kabisa kuliko ku declere kuna janga na kuleta mtafuruku. My take:; Kirusi hakifi kirahisi dawa yake ni kuufanya mwili wako uweze kupambana nacho tule vyakula vya kuongeza kinga mwili.
 
Mimi ilinpg December week 3 mfululzo

Hiii Hali isikie tuu kwa mwenzako tuuu ila la msing usilale endelee na shughuli za mwili jilazmshe San

Ukilala lala itakul kwak0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…