#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Hivi kama gharama za kupima covid ingekuwa ni 20000/ ingekuwa rahisi na kila mtu angepima kwa hiari na kuchukuwa tahadhari mapema na si kusubiri kuumwa..

Ugonjwa ulipotoweka mkapandisha gharama,, ili muendelee kuwakamua wanainchi wanaosafiri..

mkaweka sh 230000/ matokeo yake ndy hayo sasa..
Watu wanaogopa zaidi hizo gharama za kupima kuliko covid 19 yenyewe.

,,sasa mgeni karudi kwa kasi na gharama za upimaji bado zipo juu ,

, mtapandisha au mtashusha gharama ?
 
Anajibu yote.ni wewe na Imani yako tu kwake binafsi Sina Shaka nae

"Nchi hazina dini bali watu wake wana dini." Maneno ya hekima kabisa tokea kwa hayati Baba wa taifa (rip).

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana hatukuhoji wewe na mustakabala wa maisha yako. Bali tuna hoji nchi na mustakabala wa maisha yetu.

Waiona tofauti hiyo jombi?

Ulokole na uswalihina wenu msitake kuushinikiza na kwa wengine. Ndiyo maana kwa hilo mna makanisa na madhehebu zenu na hakuna anayewabugudhi huko.
 
1.Ningehakikisha watu wanakua na awareness kuwa ugonjwa huu upo.

2.At least partially lockdown, at least watu wa mkoa mmoja wasiende mkoa mwingine mpaka hali itakapotengamaa.

3.Ningefunga mipaka au ningeweka strict restrictions kwenye hio mipaka
All well and good in paper. Kwahiyo wafanyabiashara wote wanaonunua mazao mikoani, wakulima wanaotegemea soko la Dar wote wanafungiwa.

Angalia familia zao, extended families, jamii zao zitakavyotaabika.
 
Kwa mshikaji bora umuue lakini sio kuadmit kuwa kuna hii kitu. Maana kwa yeye anaona hii ndio the biggest achievement yake, sasa akirudi akubali kua kuna hiyo kitu ni kukubali udhaifu.

Kwa mshikaji ni bora wote tufe hata akiwemo yeye lakini sio akiri kua ameshindwa ama hii kitu ipo. Bora afe.

Hizi ndio akiri za viongozi wa kiafrika.
Kibaya ni pale anapoambiwa ukweli af anakuja nq sweeping statement kwamba wametumwa na MABEBERU??? yani kama toto dogo
 
kwanini kila siku unataka upewe takwimu za Corona na sio malaria?
Lini utakuja kuulizia takwimu za wagonjwa wa Kansa?.
una agenda gani na CORONA?

Takwimu za magonjwa yote na vyote vinavyopelekea vifo zikiwamo malaria, ujauzito, ajali, kansa nk zote zipo isipokuwa kwa Corona.

Uwepo wa takwimu za malaria ndiyo unaopelekea kwa kampeni endelevu za matumizi ya vyandarua.

Uwepo wa takwimu za kansa za shingo ya uzazi ndizo zinazopelekea kampeni endelevu za chanjo za chanjo kwa ugonjwa huo nk.

Takwimu za corona pekee ndizo eti kwamba zimepigwa marufuku. Hizo ndizo pekee ambazo hazipo.

Tunahoji takwimu ambazo hazipo. Tuhoji vipi takwimu zilizopo?

Hivi kuna agenda gani katika kuficha takwimu za ugonjwa wa corona? Kutokujiuliza kwako swali hilo la msingi ni dalili ya wazi za kiwango chako cha elimu kilipo.

Alipenda kusema hayati Baba wa taifa (rip), "elimu ni uhuru." Sasa kama elimu zetu ni zile zile za madarasa pekee, tutaelewana na utauona umuhimu wa takwimu kweli?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
All well and good in paper. Kwahiyo wafanyabiashara wote wanaonunua mazao mikoani, wakulima wanaotegemea soko la Dar wote wanafungiwa.

Angalia familia zao, extended families, jamii zao zitakavyotaabika.

Mi huwa simkubali jiwe kwa mambo yake, lakini nakupongeza wewe unajibu maswali vizuri kwa lengo la kuelimishana mpaka mada imekuwa nzuri.

Japo sipo pamoja na wewe
 
"Binadamu ana uwezo wa ku-adapt and survive?"

Takwimu za kuonyesha uelekeo huo waja ziko wapi?

Kwa nini jitihada kubwa mno ya kuhalalisha kutokuchukua hatua yoyote dhidi ya ugonjwa huu ni option bora zaidi kwa mijamaa ya chama fulani?
Tuchukue hatua binafsi. Tuwaelimishe ndugu, marafiki, jamaa zetu.

Binadamu ku-adapt!, ushahidi ni kwamba hadi leo bado tupo, upo duniani. Despite majanga kibao.
 
Taratibu? Pana dharura panapo maamuzi sahihi pana maisha mengi ya kuokolewa. Wajibu nambari moja wa serikali ni kulinda maisha ya watu.

Kushindwa au kutoonyesha jitihada za kutosha katika kuyalinda maisha ya watu kwa sababu yoyote ile ni kujikosesha uhalali wa kuwapo madarakani wewe mwenyewe.

Tuna ugonjwa unauwa. Tukubali hilo na tukubaliane kuukabili. Wataalamu wa afya wapo. Hakuna aliye bora kuwazidi wataalamu wa afya katika hilo.

Tatizo liko wapi hapo?
Kulinda maisha, kiuchumi, kiafya, vipato vyao familia zao, their mental health, indeed ni wajibu wa serikali yoyote.

Unajua Maralia inaua zaidi. Ila mbona hatuipi umuhimu kama Corona?
 
Sioni chochote alichokifanya zaidi ya kuwadhulumu wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi haki zao za mabilioni kama siyo matrilioni, kauwa Watanzania wengi wasio na hatia yoyote ile pia kawabambikia kesi Watanzania chungu nzima na kuwapora vijisenti vyao kwa kisingizio cha kuwatoza faini za kesi FAKE. Ni janga la Taifa huyo na ndiyo sababu Watanzania wengi wanamchukia sana hata kumuombea mabaya.
Nobody is perfect, kila mtu ana madhaifu yake. Hata wewe ungekuwa Rais kuna sehemu ungekosea.
 
Corona ipo, ila haiuwi kivile. Kati ya watu 100 mmoja atakufa. Kuna zaidi ya 99% survival rate.

Ukiwatia hofu watu, ukiwafungia ( lockdown), wengi watakufa kwa hofu, chakula kuilisha familia, polisi, stress, depression, lonelyness. (Death rate inaweza kufika 90%).
Hakuna rekodi ya wagonjwa wala vifo vinavyotokana na Corona Tanzania.Hizo data zako kwamba kati ya watu 100 anakufa tu mtu mmoja umezitoa wapi?
 
Kuna chizi kasema eti Msugwa mkurugenzi kapata changalamoto la upumuaji, eti ana nimonia! Kazi kweli kweli!
 
Tuko corona free na hii itathibitika very soon wakati bunge litakapoanza,hawatavaa Barakoa.
 
I am not talking about perfectlion even Baba wa Taifa was not perfect, but this guy is a DISASTER and DISGRACEFUL for the country as he is unfit to lead anything under the sun.
Nobody is perfect, kila mtu ana madhaifu yake. Hata wewe ungekuwa Rais kuna sehemu ungekosea.
 
Kulinda maisha, kiuchumi, kiafya, vipato vyao familia zao, their mental health, indeed ni wajibu wa serikali yoyote.

Unajua Maralia inaua zaidi. Ila mbona hatuipi umuhimu kama Corona?

Hizi ngonjera mbona mwisho wake hauko mbali?

Burundi ilikuwa hivi hivi hadi lile jabali lenyewe lilipoukwaa.

Nani asiyejuwa kuwa vita rasmi dhidi ya corona Burundi ilianza baada ya bwana Nkurinziza kusalimiwa?

Kwamba malaria tofauti yake na corona hujui? Ama kweli stajaabu ya Mussa. Kama hujui tofauti ni kuwa, "yawezekana kujilinganisha 100% dhidi ya Malaria lakini si dhidi ya corona."
 
Braza.....huu ndiyo Uhuru...covid19 ni maambukizi tu kama ilivyo kwa H I V. Kwenye HIV ulipewa elimu kisha uamuzi ukaachiwa mwenyewe...ama ule raha au uwe mgumu...hakuna sehemu serikali ilifungia watu wasigegedane au kushurutisha watumie ndom..ilikuwa ni uamuzi binafsi
Hata kwenye covid19 ...ni uamuzi binafsi ...jilinde na covid19 au ufe kwa covid19 au ufe na njaa... Tusipelekeshane [emoji2960]
 
Back
Top Bottom