#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Katika kitu ambacho hakitakiwi kufanyiwa masihara basi ni ulinzi wa Rais. Hii ni kawaida sana kwa nchi zote duniani toka enzi na enzi, sio Tanzania tuu. Na endapo likitokea la kutokea basi watu wa karibu kabisa na Rais ndiyo huwa prime blamees. Hamtaweza kuepuka lawama kwani usalama wa Rais uko mikononi mwenu na sio mikononi kwake...
Hakuna ujumbe hapo ni wingi wa sentensi, zinazopingana.
 
Kumbe Lissu alikua sawa kuacha Muhimbili na kwenda kutibiwa Nairobi Hospital.

covid.jpg
scratch2reveal.PNG
 
Mabibi na mabwana ni kwa masikitiko kuwa tumeondokewa na mtanzania mwenzetu ambaye pia alikuwa rais wetu.

Tulimpenda sana rais wetu ndiyo maana hatukuchoka kumwelezea kutoridhishwa kwetu na jinsi alivyokuwa akishughulikia gonjwa lile.

Ni masikitiko zaidi kuwa huyu katutoka na baadhi ya waliokuwa wakimhimiza kutokutusikia wamebaki.

Huu mama ni ushauri tu, tena wa bure kwako.

Una mengi sana ya kushughulikia likiwamo la msiba huu.

Pamoja na yote hili lilikuwa la muhimu zaidi kuliko yote:

"Chonde chonde gonjwa hili mama."

Anza nalo sasa. Kila dakika inayopotea ni maisha yanapotea. Hayuko aliye salama.

Kwa gonjwa hili hata wewe hauko salama.

Kwa kuanzia, ni vyema shughuli yote ya mazishi na ikazingatie uwepo wa ugonjwa huu hatari. Mabarakoa na umbali wa mtu hadi mtu.

Haisaidii kuukimbia ukweli. Kwamba nini kimemwua mpendwa wetu huyu?

Hatuna hata haja wala ya kuendelea kudanganyana. Kwani haisaidii.

Akapumzike kwa amani John Pombe Joseph Magufuli.

Ninawasilisha.
 
Katika kitu ambacho hakitakiwi kufanyiwa masihara basi ni ulinzi wa Rais. Hii ni kawaida sana kwa nchi zote duniani toka enzi na enzi, sio Tanzania tuu. Na endapo likitokea la kutokea basi watu wa karibu kabisa na Rais ndiyo huwa prime blamees. Hamtaweza kuepuka lawama kwani usalama wa Rais uko mikononi mwenu na sio mikononi kwake...
Aisee
 
Nimeamini kweli nchi yetu haina Corona, wanaotaka serikali itangaze in Corona ni wale wasiitakia mema nchi yetu, na wameungana na mabeberu kutaka kutuangamiza kama taifa, na kujitengenezea soko lao kwa ajili ya chanjo. Na chanjo hatuagizi basi.
 
Naandika kwa kifupi tu kuhusu huu ugonjwa hatari wa Covid 19 Corona. Dunia Nzima,Narudia Dunia Nzima inahangaika na vifo,kuuguza, kuagiza chanjo,kuchanja wananchi wake n.k Mie nauliza viongozi wahusika hasa Wizara ya Afya, Mganga Mkuu wa serikali Na Wengineo Hivi Mwenyezi, Mungu Muumba wa kila kitu Duniani na Akhera, Muumba Mbingu na Ardhi, Katujaalia sie Watanzania TU Tusiwe na Huu Ugonjwa? Jibu ni HAPANA.

Tunateketea Kimya Kimya.Sisi tunaishi katika sayari iitwayo Dunia (Earth) hivyo hatuna tofauti na binadamu wote wa nchi zingine.Ombi Langu kwenu Wahusika Tangazeni haraka Hatua Za Lazima Za Kujikinga na huu ugonjwa.Kutopeana mikono peke yake Hakutoshi.

Jamani tuache upuuzi huu wa kuwaita wenzetu sijui mabeberu n.k.Leo Dunia Hii aliyoiumba Mtukufu wa Milele Mwenyezi Mungu ni kama kijiji. Tuanze Leo,Tusije Kuangamia.Nakuambieni Ahsanteni na Sio Shukrani, kwani neno Shukrani ni la Mtukufu Mwenyezi Mungu Pekee.
 
Naandika kwa kifupi tu kuhusu huu ugonjwa hatari wa Covid 19 Corona.Dunia Nzima,Narudia Dunia Nzima inahangaika na vifo,kuuguza,kuagiza chanjo,kuchanja wananchi wake n.k Mie nauliza viongozi wahusika hasa Wizara ya Afya,Mganga Mkuu wa serikali Na Wengineo Hivi MwenyeziMungu Muumba wa kila kitu Duniani na Akhera,Muumba Mbingu na Ardhi, Katujaalia sie Watanzania TU Tusiwe na Huu Ugonjwa?Jibu ni HAPANA.Tunateketea Kimya Kimya.Sisi tunaishi katika sayari iitwayo Dunia (Earth) hivyo hatuna tofauti na binadamu wote wa nchi zingine.Ombi Langu kwenu Wahusika Tangazeni haraka Hatua Za Lazima Za Kujikinga na huu ugonjwa.Kutopeana mikono peke yake Hakutoshi.Jamani tuache upuuzi huu wa kuwaita wenzetu sijui mabeberu n.k.Leo Dunia Hii aliyoiumba Mtukufu wa Milele Mwenyezi Mungu ni kama kijiji.Tuanze Leo,Tusije Kuangamia.Nakuambieni Ahsanteni na Sio Shukrani,kwani neno Shukrani ni la Mtukufu Mwenyezi Mungu Pekee.
Kwani kuna mtu kakuzuia kujikinga?
Mbona mnaleta hoja kila siku za kijinga?
Mbona gest mnaenda kimya wenyewe bila condom au na condom?

Huwa kuna mtu akulazimisha?
Ukipata ukimwi ni shauli yako kwa kutotumia.

Kama umeweza kujua kuna ugonjwa kwani unakatazwa kubaa barakoa na kutumia visafiaha mikono?

Hivyo vitu viko madukani vimekosa wateja, sasa anza kuvitumia tupate biashara.
Mtu ak8kupa mikoni achana nae vau vaa gloves kaa distance uone kama kuna mtu atakuuliza.

Wewe unataka watu walazimishwe ili ufulahi?

Hayi ni mawazo yangu tu
 
Kwani kuna mtu kakuzuia kujikinga?
Mbona mnaleta hoja kila siku za kijinga?
Mbona gest mnaenda kimya wenyewe bila condom au na condom?

Huwa kuna mtu akulazimisha?
Ukipata ukimwi ni shauli yako kwa kutotumia.

Kama umeweza kujua kuna ugonjwa kwani unakatazwa kubaa barakoa na kutumia visafiaha mikono?

Hivyo vitu viko madukani vimekosa wateja, sasa anza kuvitumia tupate biashara.
Mtu ak8kupa mikoni achana nae vau vaa gloves kaa distance uone kama kuna mtu atakuuliza.

Wewe unataka watu walazimishwe ili ufulahi?

Hayi ni mawazo yangu tu

Huu ugonjwa ungekuwa kama AIDS isingekuwa tatizo. Shida kubwa hata kama unajikinga mwenzako akiwa mzembe asilimia.za huyo mzembe kukuambukiza ni kubwa mno!

Bila wote kujali wote tutapata tu! Ndo maana ni muhimu kila mtu kumlinda mwingine! Kama unajilinda jirani yako hajilindi ni kazi bure!
 
Kufa kwa corona ni uzembe wako mwenyewe.

N sawa na Quran kusema nguruwe ni haramu lakini quran hy hy ikasema ukifa kwa njaa ni ujinga wako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom