Naandika kwa kifupi tu kuhusu huu ugonjwa hatari wa Covid 19 Corona.Dunia Nzima,Narudia Dunia Nzima inahangaika na vifo,kuuguza,kuagiza chanjo,kuchanja wananchi wake n.k Mie nauliza viongozi wahusika hasa Wizara ya Afya,Mganga Mkuu wa serikali Na Wengineo Hivi MwenyeziMungu Muumba wa kila kitu Duniani na Akhera,Muumba Mbingu na Ardhi, Katujaalia sie Watanzania TU Tusiwe na Huu Ugonjwa?Jibu ni HAPANA.Tunateketea Kimya Kimya.Sisi tunaishi katika sayari iitwayo Dunia (Earth) hivyo hatuna tofauti na binadamu wote wa nchi zingine.Ombi Langu kwenu Wahusika Tangazeni haraka Hatua Za Lazima Za Kujikinga na huu ugonjwa.Kutopeana mikono peke yake Hakutoshi.Jamani tuache upuuzi huu wa kuwaita wenzetu sijui mabeberu n.k.Leo Dunia Hii aliyoiumba Mtukufu wa Milele Mwenyezi Mungu ni kama kijiji.Tuanze Leo,Tusije Kuangamia.Nakuambieni Ahsanteni na Sio Shukrani,kwani neno Shukrani ni la Mtukufu Mwenyezi Mungu Pekee.