Siasa imeingizwa kidini na kibaguzi tanzania. Kuna vuguvugu linatokota kwa kasi naliona. Na watanzania tulivyo na vichwa vyepesi kubebwa kama upepo, huko tunapokwenda ni giza.
1) Maaskofu na mapari wana fitinishwa na masheikh.
2) Masheikh nao wana fitinishwa na mapadri na maaskofu.
3) Waislamu wana fitinishwa na wakristo.
4) Wakristo wana fitinishwa na waislamu.
5) Watanzania bara wana fitinishwa na Wazanzibari.
6) Wazanzibari wana fitinishwa na watanzania bara.
7) Ubaguzi wa rangi na makabila unashika kasi.
8) Vyama vya siasa vinatoa vipeperushi kuwasemea Mapadri na Masheikh.
9) Wananchi ndio wanatumiwa kama kuni kuchochea moto.
10) Wanasiasa, wanaharakati, wanasheria n.k wanachochea moto.
Ni hatari tupu tunapokwenda! Mw. Nyerere aliona mbali kwenye ile speech yake ya "Mimi Mzanzibari/Mimi mtanganyika/Mimi Kabila Fulani".