Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Nimejaribu kujiuliza huyu jamaa anasema idadi ya wachina kuja kutalii imeongezeka. Inamaana hatuioni hatari ya hawa watu kutuletea Corona?

Mamlaka ziko wapi kudhibiti influx hii? Inawezekanaje watanzania walioko China wamezuiwa kurudi ilihali wachina kutoka China wanaruhusiwa kuingia Tz? tunachukulia vitu kimasihala sana.

Msikilize huyu jamaa

Kuna ongezeko la wageni ambao ni wachina, limeongezeka kwa kasi nchini. kutoka wale wa kawaida mabo walikuwa 40 - 50 kwa sasa wanapokea wageni 100 hadi 150 kwa siku.

Ongezeko hilo inasemekana ni kwa sababu kuwa kwao ni msimu wa sikukuu lakini pia, ni kwa ajili ya kuepuka ugonjwa wa corona unaoikabili China kwa sasa.
Your browser is not able to display this video.
 
Tuna kinga bora kuwazidi
Jr[emoji769]
 
Jamaa anasema wanawaregister Sasa labda rejister inagundua ugonjwa. Afu kasema wanashuka wamejiprotect labda na mitaani wanapita wamevaa protector. Jamaa anaongea kizembe as if ni kitu cha kawaida sana
 
Unadhani Tanzania kuna serikali inayojali watu?
Hilo ni Genge la vibaka wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa ni Mnyalukolo na ni mdesi kama jina lako lilivyo. Mbona kuna wanafunzi wa Kitanzania wengi tu wamerudi? Kuhusu wachina kuingia nchini hilo kwa kweli sifahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Tungekuwa na corona virus China wasingeruhusu yeyote kuingia
Tusubiri Trump naye ajitokeze na 'virus' yake. Hiyo tutaipa jina la Trumpiloma corona; halafu tusikie dunia inasemaje.

Virus hawana adabu kabisa, hata uwe makini vipi, wakiibuka lazima utoke jasho.

Nadhani ikitokea huko, hapo ndipo tutakapoona tofauti ya 'superpower' na sisi wengine katika maswala ya 'public health, na njia za kuzuia magonjwa ya milipuko.

China wamejitahidi kwa kiasi chao, ingetokea hapa Afrika tungeimba sokomoko!

UZURI - ni vizuri hawa watu nao wakumbushwe kwa matokeo kama haya. Yangetokea Afrika sasa hivi wimbo ungekuwa hatujui kutunza usafi, tabia zetu mbaya, n.k; n.k.

Lakini hata wachina nao bado hawaaminiki kwa tabia zao za usafi.
 
Unadhani hii imetokea wapi ndugu mpaka kusambaa kwa kasi ya ajabu nchi za Asia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…