Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Usiwaamini wahenga... Wengi wao waongo na hawakusoma
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi yaVWachini wanaikimbia nchi yao na kuja kwetu kwa kisingizio cha utalii kumbe wanajiepusha na kuambukizwa COVID -19. Ni maoni yangu tu!
 
Hata marekani wana quarantine raia wao waliotokea maeneo hayo. Raia wengine wanashikiliwa kwenye kambi ya jeshi nk. Kwa ujumla wengine wako serious sijui kuhusu sisi.
 
Ni nani vile anayetusaidia kujenga chuo cha chama Kibaha? Tusije tukajiharibia.
 
Ugonjwa wa Corona umezidi kusambaa kwa kasi na kuingia kwenye nchi nyingi duniani licha ya tahadhari kubwa na teknolojia ya hali ya juu ya kuchuja wageni


Baada ya kuona ugonjwa huu haudhibitiki kirahisi sasa imepelekea nchi nyingi kukata mawasiliano kabisa na nchi zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huu kama China, Iran, Italia, Japan na Korea

Hata hivyo Tanzania haina habari, Tanzania imezidi kupokea watalii kutoka China huku ikijidai kuwa haijali raia anatokea wapi kwa kuwa ipo vizuri kwenye kujilinda

Hiki ni kichekesho ukizingatia facilities na teknolojia za Tanzania ukizilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zimefunga kabisa usafiri na nchi athirika kwa hofu ya kuenea ugonjwa huu,

nchi kama Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa China imepiga marufuku raia wote kutoka China sababu ya ugonjwa huu ambao aambukizi yake hayaonekani mpaka zipite siku 14, nchi nyingine zilizopiga marufuku kabisa raia wa China ni Australia, Singapore, Iran, Ufilipino, New Zealand n.k

Nchi nyingine zimefika mbali zaidi kwa kupiga marufuku kabisa hata raia wa nchi nyingine ambaye aliwahi kwenda China siku za karibuni

Nchi kama Saudi Arabia imesitisha ibada za Hijja ndogo kutokana na hofu ya maambukizi haya, na inaweza kupiga hata marufuku ya Hijja kubwa

Nchi nyingi za kiarabu pia zimekatisha kabisa safari zake na Iran ambayo ina waathirika ambao hawafiki hata 300 kwa hofu ya ugonjwa huu, lakini Tanzania inaruhusu watalii kutoka China kwenye maambukizi ya takribani 80,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…