Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Watu wanapata makasiriko ghafla lakini ukweli usemwe tu usimung'unywe kinachofanywa kwenye kuajiri walimu kupitia TAMISEMI kinakatisha tamaa na kuvunja watu mioyo.

Kuna mtu alikuwa analia kwa machozi kabisa ,naye aliomba ajira za ualimu lakini yeye ambaye vyeti vipo vizuri hajapata lakini kuna mwenzake anamjua hana uwezo mzuri zaidi yake kapata.

Tusichee maisha ya watu, huu utaratibu utapunguza lawama kwa TAMISEMI na utafanya wenye uwezo wachaguliwe.

Napendeza zaidi ,kila anayeomba apewe nafasi ya interview wasifaniwe shortlisting wala nini. Kwanza, waombaji wote wafanye atleast online aptitude short hiyo ndio njia ya kushortlist ,watakaofanikiwa wanaenda kwenye written na watakaofanikiwa wanaenda kwenye practical. Unapewa darasa unafundisha, usipoeleweka ndio basi Tena.
 
Enzi hizo natafuta kazi nikaitwa kufanya interview matokeo yake wanajopo wakaniunganisha niwe miongoni mwao. Kuhoji waombaji wenzangu, nilidharau sana taasisi Ile...
images (3).jpeg
 
Watu wanapata makasiriko ghafla lakini ukweli usemwe tu usimung'unywe kinachofanywa kwenye kuajiri walimu kupitia TAMISEMI kinakatisha tamaa na kuvunja watu mioyo...
Hii kitu aiwezekani hata kwa taasisi zingine zenye waombaji wachache yaani online test puuuh, written test mara Tena darasa ukafundishe khaaa ukifuzu hapo Kwan unapewa nchi uongoze huo mlolongo wa Nini Sasa kuwakomoa au aje?
 
Tatizo la sekta ya elimu nchini si jepesi kama waziri anavyodhani.

Kwangu,naona hizo ni sarakasi tu.Ukiachana na walimu system nzima ya Elimu imeoza.

My opinions;
1.Wizara ya Elimu ijitegemee,na iendeshe taasisi zake zote za Elimu,TAMISEMI isiwe mpangaji&muamuzi wa masuala ya Elimu.

2.Elimu Bila Ada iondolewe,ada zilipwe kwa kiwango kilekile cha mwanzo,ili serikali iweze kuboresha mazingira ya kazi&maslahi ya walimu kwa kuwapa allowance monthly.

3.Siasa isiingizwe kwenye elimu kama ilivyo sasa,huu ni uharibifu.

Elimu iwe na wasemaji wake,na si kila kiongozi awe msemaji.

4.Tuna walimu wazuri,shida hatuna mikakati mizuri ya kuwatumia&kuwa thamini.

Mbona private schools wanafanya vizuri,na ni walimu hawa hawa?

Anyway ni mtazamo tu.
 
Walimu wanaofundisha Ilboru, st... Na private zenye majina na zinazofanya vizuri ndio hao hao wanaofundisha shule zetu za kata zinazochechemea.

Waziri asianze mbio na kivuli ajifunze hao wengine wanafanyaje? Mtunze mwalimu vizuri uone kama hawatafanya vizuri. Nyie mnakimbilia kujenga madarasa bila kuweka mazingira rafiki kwa mwalimu halafu mnataka matokeo.

Mtawapa mitihani bado watafaulu lakini matokeo hayatabadilika. Kwani waliopo walifeli mitihani ya vyuo? Kumbuka wengine tulifundishwa na wale wa crush program, upe na tukafanya vizuri kwenye masomo Yao.

Suala la ufundishaji linahitaji msukumo wa ndani... Na huo hujengwa kwa either kuwajali walimu, au kuwapa motisha ili waweze kutumia muda wao mwingi kuwasaidia wanafunzi. Mkajifunze kaizerege.... Nk
 
Tatizo la sekta ya elimu nchini si jepesi kama waziri anavyodhani.
Kwangu,naona hizo ni sarakasi tu.Ukiachana na walimu system nzima ya Elimu imeoza...
Wizara ya Elimu inaingiliwa kisiasa ndo maana kwa sasa husikii Zanzibar ikifelisha, ila kabla ya hapo.....

Kabla ya huyu Chato ilikuwa yaongoza Mitihani ya Kitaifa.

Wazazi wahusike katika kugharamia Elimu ya watoto wao na iwe lazima mtoto kwenda shule
 
Waziri wa Elimu Adolf Mkenda amesema ifikapo mwezi wa 9 sera mpya ya Elimu itawataka Walimu wanaoomba ajira kufanya kwanza mtihani na atakayefaulu ndiye ataajiliwa. Wadau hili suala mnalionaje. Binafsi naona ni vizuri ili kupunguza Walimu wenye uwezo wa chini kuajiliwa kwa kigezo tu Cha GPA
 
Watu wanaenda kupiga paper kila uchao pale Dom, kama hutaki uza karanga, lkn kufundisha watoto wetu bila Usaili iwe mwisho.
Huyo jamaa sijui yukoje anaona kada zingine cheti wamekipata bila ya mitìhani, coursework, assignment, test, presentation si ndiyo.
 
Usaili na mtihani ni vitu viwili tofauti
Ndio maana wanasema walimu waanze kufanyiwa usaili sababu ya akili kama hizi.

Mtihani ni sehemu ya usaili, kada zingine zote unazojua wewe kuanzia engineers, wahasibu, maHR, maafisa kilimo, maafisa ardhi n.k wanafanyiwa usaili kwa miaka mingi. Nadhani ilianza 2010

Mnaanza na Mtihani wa kuandika(written)
Alafu unafata usaili wa mahojiano(oral)

Kama huelewei haya kwa miaka yote hii basi kweli walimu mna upeo mdogo. Hamjui hata PSRS ni nini
 
Nakumbuka mwaka flani walimu tulifanya mtihani flani kwa ajili ya kazi za serikali na 99%tulipiga daraja A wachache sana walipata daraja B
Kati ya watu wako vema ni walimu tz serikali ishughulikie vitu serious kama mishahara promotion madeni miundo mbinu ya shule na vifaa vya kufundishia waone kama watu hawatapiga kazi to the fullest
Unaijua mitihani ya psrs? Watu huondoka na 0, Tena graduates wa vyuo vikubwa tu

Nashangaa inawezekana vipi Hadi leo walimu wengi hamuijui psrs, hamjui watu wengine wanaajiriwa vipi serikalini
 
Acha upumbavu wewe.
Usaili si sawa na mtihani.
Mtihani unapima knowledge na proficiency kuhusu somo husika. Wakati usaili ni si hivyo kabisa
Pengine buelewi kuwa Mtihani ni sehemu ya usaili.

Ngoja nikuulize, unajua sekretarieti ya ajira huwa inafanyia vipi watu usaili?
 
Nifanye mitihami miaka mi3 bado uje unipe Mtihani kuniajiri

None sense
Hakuna anayekulazimisha. Kuomba ni hiari. Watu wengi unaoona wameajiriwa serikali kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita jua walifanya mtihani
 
Usaili sawa lakini si kumfanyisha mitihani mwalimu
Huenda una tatizo lingine la ufahamu. Mtihani ni sehemu ya usaili

Sekretarieti ya ajira hutumia mitihani kuchuja mwanzoni, wanaobaki ndio wanaenda kwenye mahojiano ya ana kwa ana(oral interview)
 
Mhasibu,injinia,stoo kipa, afisa biashara, hakumu, woote wanafanya kwanini nyie mpate kazi km mnaswaga ng'ombe zizini fanyeni msilete mchezo.
Najiuliza hawa wanaosomea ualimu huwa hawajui hata utaratibu unaotumiwa na sekretarieti ya ajira? Huwa hawajui watu kule udom wanaenda kufanya nini?

Pia hawa walimu Ina maana wao hawajawahi hata kuomba kazi kwenye mashirika binafsi ambapo napo Kunakua na Mtihani wa online(aptitude test)? Nchi ina vilaza hii tena wengi ndio walimu wanaofundisha Watoto wetu
 
Back
Top Bottom