Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Uwalimu una pande mbili naona wanadiri na moja na kuacha nyengine ila taaluma nyengine zina pande moja tu.

Pande mbaya ya uwalimu
1/Maslahi madogo
2/Hauna posho na marupurupu
3/Masingira mabaya ya kazi

Pande nzuri ya uwalimu
1/Ajira kwa wingi bila interview

Sasa wanacholalamika watu sio hatutaki interview bali kwanini wanadili na pande moja ambayo ni faida ya uwalimu lakini huu upande mbaya wa maslahi hawadili nao wawwkw maslahi, posho na marupurupu waone Kama Kuna mtu atalalamika sio huu upuuzi.

Taaluma nyengine zina interview na hazina Mass employment lakini zina maslahi, posho na mishahara minene pia uwalimu uwe na hivi vitu wakitaka kuwe na interview.

Walimu ni muda na nyinyi kuandika walaka, kuwa wamoja ikiwezekana muamke ujinga umezidi Sana.
 
Mbona hizo kada nyingine unazosema zina maslahi, posho na marupurupu kwanini isiwe kwa walimu.
Wapi kuna maslahi? Unajua mshahara wa Mhasibu wa Halmashauri wewe? Shida yenu hamjikubali mnahisi kama mnalipwa kidogo.
Walimu ni moja ya watumishi wanaolipwa mishahara mikubwa nchi hii.
 
Na hapa kwenye hizi interview walimu wa kike wajipange



Wajifunze kugangamala [emoji123] watie akili na kuwa huru .

Wakisubiri huruma kufikiriwa itakuwa ni udhaifu mkubwa Udhaifu wao utatumika kuwaumiza kufanywa vyovyote.

Ukijitambua na ukawa na akili kubwa utaheshimika popote.
 
Nakumbuka mwaka flani walimu tulifanya mtihani flani kwa ajili ya kazi za serikali na 99%tulipiga daraja A wachache sana walipata daraja B
Kati ya watu wako vema ni walimu tz serikali ishughulikie vitu serious kama mishahara promotion madeni miundo mbinu ya shule na vifaa vya kufundishia waone kama watu hawatapiga kazi to the fullest
Hiyo mitihani alisahihisha nani?
 
Hii kitu aiwezi kudumu walimu wakianza fanya mtihani ajira zijazo za 2024 basi ndo mwisho 2025 awatofanya huu utakuja kuwa mtaji wa kisiasa Kuna mgombea urais hatakuja na sera ya kupinga huo mtihani wa usaili kwa walimu na wagombea wenzake wataunga tela ni vema mkenda wekeza nguvu na pesa kwenye vitu vya msingi hicho unachokianzisha akitodumu na utaandika historia ya mawaziri waliopita bila ya legacy
 
Utaratibu huo, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda utahusisha, ili uajiriwe kuwa mwalimu utapaswa kufanya mtihani wa kupima uwezo wako.
Uwezo wa mwalimu ni jambo moja katika mengi yanayotakiwa kufanyiwa maboresho,
  1. Mazingira ya kazi magumu mpaka leo hii kuna shule hazina ofisi za walimu wala madawati madarasani
  2. Lishe kwa wanafunzi
  3. Vifaa sahihi na bora vya kufundishia na kujifunzia
  4. Mtaala unaokwenda na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
  5. Umbali anaotembea mwanafunzi kutoka nyumbani mpaka ilipo shule
  6. Ushirikiano wa mzazi kwa Mwl
  7. Kusimamia vilivyo kalenda ya masomo
  8. Motisha kwa walimu
  9. Siasa kutoingilia wataalamu
  10. Kuyumba kwa maadili ambapo serikali haitilii mkazo sheria kuzingatiwa eg bar kukesha mahali walipo wanafunzi
 
Ule mtazamo kuwa taaluma ya ualimu ni chaguo la mwisho baada ya kukosa fursa nyingine unakaribia ukingoni, baada ya Serikali kutangaza utaratibu mpya katika ajira za taaluma hiyo.

Utaratibu huo, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda utahusisha, ili uajiriwe kuwa mwalimu utapaswa kufanya mtihani wa kupima uwezo wako.

Kwa sasa, ajira ya ualimu inahusisha kutuma maombi katika tovuti maalum ya maombi ya ajira, kisha anayepata nafasi hufanyiwa usaili kisha kupangiwa eneo la kazi.

Mwananchi
kama waziri anataka kada ya ualimu iwe na heshima, anatakiwa awe
1. anawapa mtihani wanaoomba kujiunga na course za ualimu
2.anachagua wenye division one au hata division two basi iwe wenye certificate, diploma na hata watakaoomba kujiunga na masomo ya chuo kikuu kwa course za ualimu/elimu.

vile vile asihusishe waliomaliza 2015, 2016, 2017 na hadi 2022. hii ni kwa sababu hatawatendea haki kwa kuwa vile wenzao walipata/wamepata ajira bila mtihani.
mwisho. Tanzania mbona nchi ya ajabu sana? yaan waziri anashindwa kuwa mbunifu
 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ametangaza utaratibu mpya wa ajira za Ualimu unaoelekeza Walimu kufanya Mtihani wa Kuwapima uwezo kabla ya Kuajiriwa, lengo likiwa ni kurudisha hadhi ya taaluma ya ualimu, isitazamwe kuwa chaguo la mwisho baada ya kukosa nyingine

Utaratibu wa ajira hizo kwa sasa unahusisha kutuma maombi katika tovuti maalum ya maombi ya ajira, kisha anayepata nafasi hufanyiwa usaili kisha kupangiwa eneo la kazi.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda, utaratibu huo utaanza kufanyika katika ajira mpya za taaluma hiyo, na hautafuta mchakato wa usaili, akisisitiza utaendelea kama kawaida ili kupata walimu

Amesema, "Wakati wa kutangaza nafasi mpya za ualimu, wakitaka kupata kazi, watafanya mtihani haijalishi tayari umesoma, kwanza itatuondolea matatizo. Kuajiriwa kuwa Mwalimu utafanya mtihani, utaona matokeo, tutaangalia idadi inayohitajika tutachukua waliofaulu tutawaajiri,"


Chanzo: Mwananchi
hata walioko kazn wawe wanapigwa paper kila baada ya miaka miwili. Hii ihusu watumishi wote wa umma ikiwemo na huyo waziri .
 
kama waziri anataka kada ya ualimu iwe na heshima, anatakiwa awe
1. anawapa mtihani wanaoomba kujiunga na course za ualimu
2.anachagua wenye division one au hata division two basi iwe wenye certificate, diploma na hata watakaoomba kujiunga na masomo ya chuo kikuu kwa course za ualimu/elimu.

vile vile asihusishe waliomaliza 2015, 2016, 2017 na hadi 2022. hii ni kwa sababu hatawatendea haki kwa kuwa vile wenzao walipata/wamepata ajira bila mtihani.
mwisho. Tanzania mbona nchi ya ajabu sana? yaan waziri anashindwa kuwa mbunifu
Mbona kada zingine walipoanza kufanya usaili hawakuangalia wale walioajiriwa kabla ya huo utaratibu? Walimu mna shida gani na huu utaratibu? Acheni kudekezwa nyie vipi bhana? Fanyeni usaili ndipo muajiriwe, mbona kada zingine tumefanya usaili?
 
Which means hawana imani na wakufunzi huko mavyuoni...!!!
Anaetoka chuo ni mwalimu kamili.. ila wanatofautiana uwezo. Nadhani ni sahihi kuchuja upya ili kupata walio bora zaidi kwa ufanisi wa kazi.. kama wanavyofanya private schools
 
Walimu wenyewe wanamashaka makubwa sana na uelewa huyo waziri wao maana nae anaonekana hana uwezo mzuri.
Lazima utakuwa una tumbo la Kuhara!

Hivi unayajua machapisho ya Huyu Mwamba?

Waalimu ni Academicians...ni lazima wapimwe intellectual capacities zao!

Huo unaitwa usaili.

Kwa wale waliojiunga na Chuo kikuu kama Matured age entry walifanya kitu kinaitwa Matriculation.

Hakuna cha ajabu hapo ni kwa Sababu tu watu wako busy na kupinga kila kitu..!
 
Lazima utakuwa una tumbo la Kuhara!

Hivi unayajua machapisho ya Huyu Mwamba?

Waalimu ni Academicians...ni lazima wapimwe intellectual capacities zao!

Huo unaitwa usaili.

Kwa wale waliojiunga na Chuo kikuu kama Matured age entry walifanya kitu kinaitwa Matriculation.

Hakuna cha ajabu hapo ni kwa Sababu tu watu wako busy na kupinga kila kitu..!
Kuna kitu hukijui bwana mdogo machapisho kila mtu na uwezo wa kuandika kulingana na field aliyopo hata ukimchukua muuza karanga ukampa akills za kuchapisha ataweza kuchapisha kilingana ma field yake mimi sio theory worshipper mzee, machapisho watu wanaandika kwa kunukuu content za wa watu wengine kwani hulijui hilo

Machapisho mengi ya waswahili hawa yamebeba karibu 45% ya theories zilizo chapishwa na waingerez , wafaransa, wamarekani pamoja na wajeruman na waitaliano kwa mbali halafu wao ndio wana associate na mazingira ya africa

Tunapima intelligence ya mtu kwa uwezo wake kwanza kubaini tatizo halisi na kutafuta suluhu halisi inayo fit kutatua tatizo husika kulingana na mzingira halisi ya tatizo hilo na sio hayo ya kukopa kutoka kwa wafilipi na kutaka kulazimisha ya fit kwa mtanzania wa kitumbini ambaye kwanza tangu azaliwe hajawahi kukamilisha milo mitatu achilia mbali miwili na hajui chochote kuhusu balanced diet.
 
Mashule mengi ya msingi na sekondari yamejaa walimu wababaishaji na wakaguzi wa elimu hawalijui hili. Unakuta mwalimu anakwepa kufundisha madarasa fulani anajijua ni mtupu kichwani...
Idara ya elimu kwa ujumla kumejaa wababaishaji.

Nimewahi kuwa na uhusiano na watu wa idara ya elimu ( mwalimu mkuu msingi,mwalimu sekondari, mkaguzi,afisa elimu wilaya na mkoa + mkufunzi wa chuo cha ualimu),kusema ukweli ni watupu mno kwenye taaluma yao na kiuwezo kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom