Serikali: Watumiaji wa Daraja la Tanzanite, Barabara ya haraka Kibaha - Morogoro, Igawa - Songwe -Tunduma kuanza kulipia ushuru

Serikali: Watumiaji wa Daraja la Tanzanite, Barabara ya haraka Kibaha - Morogoro, Igawa - Songwe -Tunduma kuanza kulipia ushuru

Watanzania wenzangu, ifikie wakati tuungane na kukiondoa hiki kirusi kinachoitwa ccm! Haiwezekani fedha zilizotumika kujengea hayo madaraja, zimetokana na kodi zetu! Au mikopo ambayo tutatakiwa kuilipa na vizazi vyetu!

Halafu leo tunatakiwa kulipia! 2025 tuwaondoe madarakani hawa mafisadi. Kodi zenyewe wakipata kwa sehemu kubwa, wanazitumia kwa manufaa yao tu.
Maskini unaende kwenye toll road kufanya nini? Pita ya zamani..

Na kwa taarifa yako hiyo barabara Itajengwa kwa EPC
 
Tofauti na madaraja mengi ya namna hii barani Afrika, Watumiaji hawatalipa tozo yoyote pindi watumiapo daraja hili (TOLL FREE). Pia, Daraja hili lenye uwezo wa kuhimili tani 180 za uzito litaweza kusafirisha watu wapatao 55,000 kwa siku
Hii ndio ilikua ahadi
 
Hii ni sawa na kuendelea kumbebesha mzigo mlipa kodi. Maana hata kama zinajengwa kwa mikopo toka ka wahisani, bado mikopo hiyo italipwa na sisi wenyewe walipa kodi.
 
Tuseme tu ukweli Dr. Madelu ni kiumbe mwenye roho mbaya sana. Tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Fedha, amekuja na kodi lukuki za kuwaumiza tu watu wa chini na wale wa kati!

Wale matajiri wenzake amegoma kabisa kuwagusa. Yaani ana tofauti kubwa sana ya utendaji kwenye hiyo Wizara, na mtangulizi wake Dr. Phillipo Mpango.

Cha kushangaza na Bi Mkubwa anamkubali kweli! Muhimu tu asije kumtafuta mchawi pale jahazi lake litakapo zama 2025! Maana siamini kama kuna mtu atakubali kumchagua kupitia sanduku la kura, eti kwa sababu tu amejenga madarasa kupitia mkopo kutoka IMF.
Una mwonea bure tu mkuu.
Nchemba hana ubavu wa kuanzisha lolote isipokuwa ana baraka za mama na baraza la mawaziri.
Hili ni boya tu wapo wanaoliongoza
 
Hii ya Kibaha-Mlandizi-Morogoro express way ni ipi? Au ndio watajenga? [emoji2] [emoji2]
Itajengwa mkuu, michoro na fidia kwa wanachi zineandaliwa.
Road toll zipo hata Kenya wamejenga fly over ya 27km hiyo ni ya kulipia
 
Afadhali,na sio kuwe na tozo halafu matrafiki wanazagaa kila kona kukusanya wanaozidisha speed,itakuwa haina maana...
Hii barabara ya express way huwa hakuna vizuizi ni kujiachia tu, nafikiri mtu halazimishwi kulioia kwani ya bure itaendelea kuwepo
 
Hii ni sawa na kuendelea kumbebesha mzigo mlipa kodi. Maana hata kama zinajengwa kwa mikopo toka ka wahisani, bado mikopo hiyo italipwa na sisi wenyewe walipa kodi.
Mzigo gani? Hiyo barabara Itajengwa kwa na private sector, yaani kiufupi ni uwekezaji wa private sector kwenye barabara..

Hapo mlipakodi hubebeshwi chochote ila ukiamua kupita lazima aliyejwnga akutoze gharama..

Watzn ni Washamba Sana ndio maana mnashangaa kila kitu..

Hii inatukima Afrika kote.
 
Make kwanza nicheke, hapo hawatakula hata cent 5, daraja lenyewe anasa kwa week naweza pita mara moja tu. Lile daraja lilijengwa mahasusi kwa mabalozi.

Impact yake tutegemee foleni kubwa sana hakuna mtu atayekubali kulipa huo ushuru wakati anaweza pitia salenda ya zamani mtu ataona bora avumilie tu.

Hii nchi tukisemaga tulipigwa upande wa Rais kuna watu wanakupinga anyway[emoji23][emoji23]
 
Tulisema hapa hata kama hayati Magufuli alikuwa anakopa haidhuru kwa sababu matunda ya mikopo ile inaonekana dhahiri

Sitashangaa kusikia Fly over ya Kijazi nayo ikawa ya kulipia

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Hilo halina shida na wala sio jambo geni kwa sababu hata daraja Nyerere kigamboni magari yanayo pita pale yanalipia.

Ila kwa barabara ya Dar~kibaha~mlandizi~chalinze, ikijengwa barabara yenye hadhi pia hakuna shida watu watalipia tu, Serikali itakusanya mapato ya kutosha.

Nchi haiwezi kujengwa kwa maneno bila kukusanya kodi/tozo,
fedha zetu na za wawekezaji ndio zitakazo lijenga Taifa letu.

tusidanganyike ni misaada, tusipende vya buree tutalemaaa .

Umeongea point ila inaonesha wewe ni walewale walamba asali, ukiweza tuambia zile tozo za miamala ya simu zinafanya kazi gani mpaka sasa utakua umetisha. Sio tunatozwa mwisho wa siku watu wanaendelea kuza vitambi maendeleo hayaonekani
 
"Ya magufuli"? Mbona na yeye alikuta vyanzo vya mapato vilivyoundwa na wengine ndo akapata jeuri ya kujenga hayo
 
Back
Top Bottom