Serikali: Watumiaji wa Daraja la Tanzanite, Barabara ya haraka Kibaha - Morogoro, Igawa - Songwe -Tunduma kuanza kulipia ushuru

Serikali: Watumiaji wa Daraja la Tanzanite, Barabara ya haraka Kibaha - Morogoro, Igawa - Songwe -Tunduma kuanza kulipia ushuru

Kuendesha gari Tanzania ni gharama sana aisee gari limewekwa kwenye kundi la starehe kila kukicha wanaliongezea mzigo magari yenyewe mtumba wanatusumbua na kodi lukuki ila Jamaa ana roho ngumu sana aisee maisha ya kupenda sifa na kuumiza wengine sio mazuri wacha tuendelee kumsikiliza...kaweka kodi kwenye simu hajui simu ni kitabu pia ssbabu anazotoa hazieleweki..
 
Blah blah blah.
Kama ujenzi wa barabara ya Moro kutoka Kimara mpaka Kibaha 19 km imechukua miaka mitano na bado haijaisha.
Reli ya SGR DAR MORO less than 200 km ulianza 2017 November mpaka Leo bado treni hazijaanza..
Unategemea Kibaha Chz Moro 158 km itaisha awamu hii ya tano?
Mwigulu ameongea maneno tu Kama watu wanavyoongea wakicheza bao.
Waswahili wanasema hayo ni maneno hata kwenye khanga yapo.
 
sijaelewa, igawa songwe tunduma kuna express way? au ndio ile ile barabara ya Zambia? au wanataka kujenga express way toka Igawa, waizunguke Mbeya wakatokezee Mkoa wa Songwe hadi Tunduma way to Zambia?
 
Blah blah blah.
Kama ujenzi wa barabara ya Moro kutoka Kimara mpaka Kibaha 19 km imechukua miaka mitano na bado haijaisha.
Reli ya SGR DAR MORO less than 200 km ulianza 2017 November mpaka Leo bado treni hazijaanza..
Unategemea Kibaha Chz Moro 158 km itaisha awamu hii ya tano?
Mwigulu ameongea maneno tu Kama watu wanavyoongea wakicheza bao.
Waswahili wanasema hayo ni maneno hata kwenye khanga yapo.
Mkuu kuwaga mwelewa na wewe! Maneno tunayoongeaga kwenye Mchezo wa Bao yana maana sana kuliko Maneno ya Mwigulu!
 
But huo mpango unakuaje uje ghafla,unajua nyerere bridge tulifahamu ni la kulipia toka kitu kipo under construction,iweje Tanzanite na kibaha highway ghafla tu mtu kakaa kwake na mkewe aamue ziwe za kulipia,tupunguze kupinga kila kitu na tupunguze kuunga mkono kila kitu hata kama mmepuyanga,wewe kila siku tunawacheka wakenya kule kulipia express way kwenye ule uzi,huku unakuja kuunga mkono!wewe jamaa .....
Serikali inatafuta Kodi wewe unasema ghafla..ghafla ndio maana yake nini?

Mimi sijawahi sema expressway kwenye toll road ni mbaya maana ni options.
 
Hilo halina shida na wala sio jambo geni kwa sababu hata daraja Nyerere kigamboni magari yanayo pita pale yanalipia.

Ila kwa barabara ya Dar~kibaha~mlandizi~chalinze, ikijengwa barabara yenye hadhi pia hakuna shida watu watalipia tu, Serikali itakusanya mapato ya kutosha.

Nchi haiwezi kujengwa kwa maneno bila kukusanya kodi/tozo,
fedha zetu na za wawekezaji ndio zitakazo lijenga Taifa letu.

tusidanganyike ni misaada, tusipende vya buree tutalemaaa .
Upuuzi tuu, pesa yenyewe ni mkopo halafu unajifutua kama kifutu... Kwanza kwenye hizo Trilioni 41 za bajeti hivi unajua kwamba ni around 6 Trilioni tuu inayoenda moja kwa moja kutatua kero za jamii??
 
Hii ya Kibaha-Mlandizi-Morogoro express way ni ipi? Au ndio watajenga? [emoji2] [emoji2]
Hata Mimi nilihitaji kujua express way ya kibaha mlandizi morogoro, na ya IGAWA - SONGWE TUNDUMA, Cz nijuavyo kuanzia IGAWA kwenda MBEYA TUNDUMA ni mashimo mtindo mmoja
 
Nchi ya ajabu sana hiii, tuna mbuga, madini, gas, bandari lakn sasa mwananchi anakamuliwa
Hizo maliasili zote si wamezigawa kwa ndugu zao Waarabu na Mabeberu kutoka Ulaya, China na Marekani iki tu kupata 10%

Hawa watawala wetu kuna wakati unaweza kuhisi wamerogwa vile! Yaani hawana kabisa uchungu na wananchi wenzao! Wao wako busy kupigana vikumbo kwenye ufisadi na upigaji tu.
 
Serikali inatafuta Kodi wewe unasema ghafla..ghafla ndio maana yake nini?

Mimi sijawahi sema expressway kwenye toll road ni mbaya maana ni options.
Pesa hiyo ndio umkabe raia kila sehemu,miamala tozo,tena sasa wameanza kukata hadi kwenye malipo ya luku na dawasa,yan kila sehemu umminye raia na bado life mbovu,nenda nchi zilizoendelea wananchi wanalipa kodi sio tozo za ajabu ajabu na bado wanapata elimu bora,afya bora kwenye taasisi za serikali hamna rushwa,mnafosi kukata raia matozo then hapo hapo akiumwa panadol tu inabidi anunue
 
Madini na gesi hawaoni Kama ni source ya mapato.
Mimi nilisemaga asilimia 90 ya boda boda hawana leseni. Wakibanwa wachukue leseni @ 70,000 itakua zaidi ya bajeti ya wizara moja.
Yan mwigulu yeye njia yake ya kupata pesa ni kuwabana raia tu,raia huyo anaibiwa kwenye vifurushi vya simu n.k lakini hawana mpango wowote wa kushughulikia hiyo issue,wanakera!
 
Back
Top Bottom