Serikali: Watumiaji wa Daraja la Tanzanite, Barabara ya haraka Kibaha - Morogoro, Igawa - Songwe -Tunduma kuanza kulipia ushuru

Ulitaka akabwe nani? Kodi zingine anakabwa nani? Kulipa Kodi sio optimal ,lipa Kodi dai huduma...

Wewe unacholipa unaona kinatosheleza kupata unayohitaji Kwa idadi na quality inayotakiwa?

Umesema Nchi zikizoendelea unadhani maendeleo yalishishwa na mvua? Walilipa Kodi na waliumia kweli kweli..

Unataka nani akujengee Nchi? Jenga Nchi watapata unafuu wajao ambao watakuta mambo mengi tayari yapo.
 
Kinachoonekana hapa pesa inakusanywa nyingi na inatafunwa nyingi kwa hiyo kila siku wanaona haitoshi na kuwaongezea wananchi mzigo wa kodi

Gali zote zinazotembea barabarani zinalipa kodi ya barabara ilikuwaga inalipwa kila mwaka sasa hivi imewekwa katika mafuta
 
Duh!... Umeamua kutabiri kabisa
 
Wanataka tulipie daraja x2? Tulipe tozo ya road fund kwenye mafuta na daraja tulipe?
 
kwanza hakuna chama cha kukiondoa ccm madarakani labda ifikapo 2090!! hilo pigia mstari kichwani.

Kodi lazima tulipe kwa maendeleo yetu sisi wenyewe, ilimradi tunaona maendeleo yanayo fanyika.

hakuna Taifa linalo weza kupiga hatua ya maendeleo bila kodi, na tunapaswa tuelewe kuwa kodi inalipwa na wananchi husika na wawekezaji.

jambo la msingi ni kuangalia matumizi na thamani ya fedha zinazo tumika ktk miradi inayo fanyika na kisha kufichua ubadhirifu kama upo.

Kodi tutaendelea kulipa kwa ustawi wa Nchi yetu.

Kodi ni uzalendo, Kodi na maendeleo yako na kizazi chako kijacho.
 
Nchi za wenzetu haya mambo ni ya kawaida sana...
 
Hii itasimamishwa mara moja na nyote mutashangilia kwa nguvu🤣
Wakere Wananchi kisha jitokeze Kuwahurumia ili uzidi kupata Sifa, Wakupende na mwaka 2025 iwe rahisi Kwako Kukumbukwa na Kuchaguliwa kuongoza tena Watanzania.
 
Nchi ya KISHAMBA SANA HII.

Yaani wajenge Barabara kwa kuwakamua wananchi kodi halafu tena wakitumia Barabara hiyo walipie?

Sisi ni WAKIMBIZI?

Huyu jamaa anamgombanisha Rais na Watanzania.
 
Ushamba tu. Sijui kisa ni lizuri kwa kibongobongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…