Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Watanzania ni walalamishi sana , Dkt Magufuli alizuia na kufunga mipaka mlilalamika na kumlaumu. Tuzoee tu soko huria
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Hao wakulima ndio huwa wakwanza kulia njaa mambo yanapobumbuluka
 
Unasema bei haijawahi kutokea bila hata utafiti

Je, unajua bei ya unga nchi jirani?

After all; uko mji gani uko wanakouza unga 2000?
 
Katiba itasimamia wizara ya kilimo ifanye maamuzi KWA ajili ya ustawi wa Taifa letu!!
Itasimamia masoko ya bidhaa ya kilimo KWA faida ya watz!!

Kuliko ilivyo sasa Rais anapelekeshwa na wafanyabiashara nchini bila kujali mtumiaji wa Mwisho atafaidikaje!!

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!
 
Pale iringa yale mavihenge mawili yamechukuliwa na mkenya amejaza mahindi mle na anakobokoa kisha anapaki unga kwenda kuuza kwao!

Wanaofikri mkulima ndio anafaidika hawana akili! Mkulima hakuna chochote anachofaidika. Wanaofaidika ni walanguzi wanaoenda kulangua mahindi kwa wakulima kisha wao huuza kwa profit kubwa kubwa!

Hata mahindi yakiuzwa debe kwa laki 1 hakuna chochote mkulima wa jembe la mkono hapa tz atafaidi!

Njaa ikianza wakwanza kulalamika watakuwa ni hao wakulima.
 
Nani asiekujua chawa?

Hapo unajita awamu ya 6 utafikiri wewe ni miongoni mwao!

Muuonee huruma mamako kule kijijini kwa maisha anayoishi
 
Ufumbuzi wa hilo ni kufunga mipaka na/au kuzuia wanaouza nje?
 
Msitupigie kelele hapa ! Hutaki kununua kalime chakula chako .
Mkulima ahenyeke wewe unenepeshe makalio yako kununua Kwa bei ya bwerere inayomuumiza mkulima ,umelogwa nini ?
 

Mkuu nenda na ww ukalime ili upate chakula. Zile enzi za kumbana mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya faida umepita. Ww kalime chakula chako usisafirishe nje ili uuze hapa hapa kwa bei ndogo ili kuzuia njaa.
 
Reactions: Tsh
Usipige kelele sana wasije wakastuka na kufanya mipozo yao ya kuigiza.

Acha wananchi wenyewe wapate funzo, pengine huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kuingiwa na akili kichwani na kuamua kuleta mageuzi chanya.
 
Ufumbuzi ni kukataza wakulima kuuza mazao yao kwa anayewapa bei ya juu zaidi? Au ni kuwakataza wasiuze kabisa mazao yao? Ifike mahali wakulima wawe treated kama watu wanaoweza kujiamulia wenyewe. Nani kakuambia wanaouza hawajajiwekea akiba? Kama itabidi wapate njaa ndiyo wajifunze basi na iwe hivyo.
 
Mkuu nenda na ww ukalime ili upate chakula. Zile enzi za kumbana mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya faida umepita. Ww kalime chakula chako usisafirishe nje ili uuze hapa hapa kwa bei ndogo ili kuzuia njaa.
Hapana, si hivyo.

Nadhani hukuelewa alichomaanisha yeye. Hajakataa wakulima kuuza kwa faida kwa yeyote yule iwe ndani au nje ya nchi. Lakini hili halifanyiki holela tu. Hakuna serikali popote duniani inayoruhusu namna hiyo ya ufanya biashara.

Kama wakulima wenyewe wanaouza mazao yote, hata akiba ya chakula chao, njaa ikiingia nchini, hilo siyo janga?
 

Mkuu viongozi wachukue hatua wamemsaidia mkulima yoyote kulima? Wakulima wamenunua mbolea hadi 130,000 kwa mfuko, ni wapi serikali imewasaidia wakulima kununua hiyo mbolea? Wakulima wamegeuka kuwa kada masikini hapa nchini ili watu waendelee kufuga vitambi. Acha wakulima nao wakauze sehemu itakayowalipa.
 
May 2020 unga wa mahindi kilo moja ilikuwa 2500. Unasemaje haijawahi kutokea?
Watu wasahaulifu sana...ila mkuu wakati wa Magufuli alikua anachukua hatua za haraka sana.
 
Mwingine kaacha mashamba kwao kaenda kuuza chupi kwa muhindi zinazotoka china anataka aliyelima apangiwe bei ili yeye ashibe.
 

Mfuko wa mbolea umepanda hadi 130,000+, ni wapi serikali imesaidia kwenye hilo? Huyu mleta uzi ni wapi amewanunulia mbolea wakulima ili waogope kuuza nje kwa faida?
 
Watu wasahaulifu sana...ila mkuu wakati wa Magufuli alikua anachukua hatua za haraka sana.
Kwa kuzuia mazao kuuzwa nje kwa bei ya faida? Kwann asingenunua kwa bei ya soko na kugawa kwa wenye njaa? HAKUWA SAWA. Imagine watu wote wasilime walalamike serikali izuie mazao kutoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…