Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao

Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati

imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya

Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa

mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula

CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda

tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui

Sawa bwana
Watanzania ni walalamishi sana , Dkt Magufuli alizuia na kufunga mipaka mlilalamika na kumlaumu. Tuzoee tu soko huria
 
Kumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biasha upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida. Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Hao wakulima ndio huwa wakwanza kulia njaa mambo yanapobumbuluka
 
Unasema bei haijawahi kutokea bila hata utafiti

Je, unajua bei ya unga nchi jirani?

After all; uko mji gani uko wanakouza unga 2000?
 
Katiba itasimamia wizara ya kilimo ifanye maamuzi KWA ajili ya ustawi wa Taifa letu!!
Itasimamia masoko ya bidhaa ya kilimo KWA faida ya watz!!

Kuliko ilivyo sasa Rais anapelekeshwa na wafanyabiashara nchini bila kujali mtumiaji wa Mwisho atafaidikaje!!

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!
 
Biashara ya mazao ni kitu cha aina yake waziri bashe kaa ofisini lakini nauhakika haujui lolote huku field nini kinaendelea maana hata uhakiki wa wakulima wenu hamjafanya ndio maana wageni hununua mashamba kama wazawa na kuanza kuchapa jembe kama kawaida lazima muwe na mipango ya kueleweka
Pale iringa yale mavihenge mawili yamechukuliwa na mkenya amejaza mahindi mle na anakobokoa kisha anapaki unga kwenda kuuza kwao!

Wanaofikri mkulima ndio anafaidika hawana akili! Mkulima hakuna chochote anachofaidika. Wanaofaidika ni walanguzi wanaoenda kulangua mahindi kwa wakulima kisha wao huuza kwa profit kubwa kubwa!

Hata mahindi yakiuzwa debe kwa laki 1 hakuna chochote mkulima wa jembe la mkono hapa tz atafaidi!

Njaa ikianza wakwanza kulalamika watakuwa ni hao wakulima.
 
Upumbavu wenu wasimulieni wake zenu..

Ukitaka bei rahisi kalime,au Lima harafu waambie serikali wafunge mipaka..

Ila kwetu awamu ya 6,kilimo ni biashara kama hardware and the likes..

Awamu ya 6 sio wapumbavu kama awamu ya 5,tumeingiza bil.954 hatuwezi acha zipotee tunataka zilete tija kwa kilimo kuchangia 10% ya Pato la Taifa..

Ushenzi wenu mtafanya mkijapata madaraka na kuwaongoza wajinga
Nani asiekujua chawa?

Hapo unajita awamu ya 6 utafikiri wewe ni miongoni mwao!

Muuonee huruma mamako kule kijijini kwa maisha anayoishi
 
Wanaouza mazao wakati huu wala mkulima hahusiki kabisa tena ni mapesa toka nje yaliyoingia kununua mazao na kuweka stock mazao kwa mfano kijiji cha gwarama kule kakonko. Wanyarwanda wamejenga magodown kupitia wafanyabiashara wa pale na kila mwaka huweka tani nyingi mno za mazao wakati kama huu husafirisha, haya pale nyakanazi kuna tajiri wa burundi anaitwa kamangaza ana magodown pale kupitia wazawa na hununua mahindi mengi sana na mtama, na huanza kusafirisha kwenye uadimu hali kadhalika wafanyabiashara wakenya huingiza pesa nyingi sana kule chunya na songea nakuweka store tani nyingi sana za mazao, kwahiyo tunaposema mfunge mipaka tunamaana mnufaika kwa sasa sio mkulima kama mnavojidanganya, mavuno yangekua mengi ni sawa lakini mnakaza vichwa huko serikalini wakati hamna hata taarifa za kutosha
Ufumbuzi wa hilo ni kufunga mipaka na/au kuzuia wanaouza nje?
 
Msitupigie kelele hapa ! Hutaki kununua kalime chakula chako .
Mkulima ahenyeke wewe unenepeshe makalio yako kununua Kwa bei ya bwerere inayomuumiza mkulima ,umelogwa nini ?
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Imeamua kwa makusudi kutuacha watanzania na kuangali maslai yao

Hali ni mbaya sana mtaani vyakula bei hazishikiki

Vyakula vinavushwa mipakani na kwenda nje ya nchi sisi hatupati

imefika hatua sasaivi mabwenyenye wananunua mzigo bado upo shambani wanavuna na kupeleka nje ya nchi, Kilimanjaro kuna njaa lakini mahindi yanapitia hapohapo kwenda kenya

Sasaivi unga wa sembe kilo moja 2000 hii haijawai kutokea kabisa

mchele 2400 kilo

Serikali ipo kimya tu wao wanahela za kula

CCM imeamua kutusaliti, sasaivi sokoni hatuoni mahindi yanatoka kwenye stock yanawekwa kwenye maroli yanavuka boda

tukisema hivi wanaona kama tunatania maana wao hali ya mtaani hawaijui

Sawa bwana

Mkuu nenda na ww ukalime ili upate chakula. Zile enzi za kumbana mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya faida umepita. Ww kalime chakula chako usisafirishe nje ili uuze hapa hapa kwa bei ndogo ili kuzuia njaa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh

Usipige kelele sana wasije wakastuka na kufanya mipozo yao ya kuigiza.

Acha wananchi wenyewe wapate funzo, pengine huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kuingiwa na akili kichwani na kuamua kuleta mageuzi chanya.
 
Pale iringa yale mavihenge mawili yamechukuliwa na mkenya amejaza mahindi mle na anakobokoa kisha anapaki unga kwenda kuuza kwao!

Wanaofikri mkulima ndio anafaidika hawana akili! Mkulima hakuna chochote anachofaidika. Wanaofaidika ni walanguzi wanaoenda kulangua mahindi kwa wakulima kisha wao huuza kwa profit kubwa kubwa!

Hata mahindi yakiuzwa debe kwa laki 1 hakuna chochote mkulima wa jembe la mkono hapa tz atafaidi!

Njaa ikianza wakwanza kulalamika watakuwa ni hao wakulima.
Ufumbuzi ni kukataza wakulima kuuza mazao yao kwa anayewapa bei ya juu zaidi? Au ni kuwakataza wasiuze kabisa mazao yao? Ifike mahali wakulima wawe treated kama watu wanaoweza kujiamulia wenyewe. Nani kakuambia wanaouza hawajajiwekea akiba? Kama itabidi wapate njaa ndiyo wajifunze basi na iwe hivyo.
 
Mkuu nenda na ww ukalime ili upate chakula. Zile enzi za kumbana mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya faida umepita. Ww kalime chakula chako usisafirishe nje ili uuze hapa hapa kwa bei ndogo ili kuzuia njaa.
Hapana, si hivyo.

Nadhani hukuelewa alichomaanisha yeye. Hajakataa wakulima kuuza kwa faida kwa yeyote yule iwe ndani au nje ya nchi. Lakini hili halifanyiki holela tu. Hakuna serikali popote duniani inayoruhusu namna hiyo ya ufanya biashara.

Kama wakulima wenyewe wanaouza mazao yote, hata akiba ya chakula chao, njaa ikiingia nchini, hilo siyo janga?
 
Tulishauri mwaka huu mavuno ni kidogo wafunge mipaka kwani hata soko la ndani tu linatosha wakashupaza vichwa vyao, mavuno yakiwa mengi watu wauze nje ni sawa lakini mwaka wenye mavuno kidogo nao wauze nje kipindi chote hapana, Burundi kuuza mahindi, maharage, mtama na muhogo ni uhujumu uchumi kwa sasa, uganda kazuia hakuna kuuza chochote nje isipokua ni ruhusa kununua, na kuingiza ndani, Rwanda kazuia kabisa hakuna kutoa hata kiazi, wizara ya kilimo ipo ipo tu imekalia siasa, hakuna usalama kama nchi haina chakula cha kutosha na mkumbuke dunia nzima mavuno kwa mwaka ulioisha yalikua hafifu sana, viongozi hawachukui maamuzi simply sababu wao na familia zao njaa haitowakumba.

Mkuu viongozi wachukue hatua wamemsaidia mkulima yoyote kulima? Wakulima wamenunua mbolea hadi 130,000 kwa mfuko, ni wapi serikali imewasaidia wakulima kununua hiyo mbolea? Wakulima wamegeuka kuwa kada masikini hapa nchini ili watu waendelee kufuga vitambi. Acha wakulima nao wakauze sehemu itakayowalipa.
 
May 2020 unga wa mahindi kilo moja ilikuwa 2500. Unasemaje haijawahi kutokea?
Watu wasahaulifu sana...ila mkuu wakati wa Magufuli alikua anachukua hatua za haraka sana.
 
Mwingine kaacha mashamba kwao kaenda kuuza chupi kwa muhindi zinazotoka china anataka aliyelima apangiwe bei ili yeye ashibe.
 
Hapana, si hivyo.

Nadhani hukuelewa alichomaanisha yeye. Hajakataa wakulima kuuza kwa faida kwa yeyote yule iwe ndani au nje ya nchi. Lakini hili halifanyiki holela tu. Hakuna serikali popote duniani inayoruhusu namna hiyo ya ufanya biashara.

Kama wakulima wenyewe wanaouza mazao yote, hata akiba ya chakula chao, njaa ikiingia nchini, hilo siyo janga?

Mfuko wa mbolea umepanda hadi 130,000+, ni wapi serikali imesaidia kwenye hilo? Huyu mleta uzi ni wapi amewanunulia mbolea wakulima ili waogope kuuza nje kwa faida?
 
Watu wasahaulifu sana...ila mkuu wakati wa Magufuli alikua anachukua hatua za haraka sana.
Kwa kuzuia mazao kuuzwa nje kwa bei ya faida? Kwann asingenunua kwa bei ya soko na kugawa kwa wenye njaa? HAKUWA SAWA. Imagine watu wote wasilime walalamike serikali izuie mazao kutoka.
 
Back
Top Bottom